Mama Maria wa  Suyapa huko Honduras Mama Maria wa Suyapa huko Honduras 

Honduras-Mkurugenzi wa PMS:Ni muhimu kuelewa uhusiano kati ya hisani na uinjilishaji!

Katika fursa ya siku ya Kimisionari ulimwenguni tarehe 18 Oktoba 2020,Padre Bernardino Mkurugenzi wa(PMS)Amerika ya Kati amesema ni muhimu kujua uhusiano uliopo kati ya hisani na uinjililishaji ambao ni uzoefu wa uhai wa maisha ya watu wa Mungu.Ndugu maskini kwa kwawaida ushirikishana kile kidogo walicho nacho kwa maskini wenzao;ni kama mtindo wa jumuiya za kwanza za kikristo.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Kuna furaha kubwa na shauku katika pande zote za utume wa kimisionari kwa mwezi Oktoba. Hii ni fursa nzuri ya kuwaalika wote waliobatizwa ili kujua wito wao na kujitoa kwao katika  kushirikiana kwenye kazi kuu ya Mungu. Amesema hayo Padre Bernardino Lazo, Mkurugenzi wa Shughuli za kipapa za kimisionari  (POM) nchini  Honduras wakati akizungumzia juu maadhimisho ya mwaka huu katika mwezi wa kimisionari katika nchi za Amerika ya Kati, ambapo Dominika tarehe 18 imeadhimisha Siku ya kimisionari ulimwenguni.   Kwa mujibu wa Padre Bernardino amesema ni muhimu kujua uhusiano uliopo kati ya hisani na uinjililishaji ambao ni uzoefu hai wa maisha ya watu wa Mungu. Ndugu maskini kwa kawaida ushirikishana kile kidogo walicho nacho kwa maskini wenzao ni kama mtindo wa jumuiya za kwanza za kikristo. Makanisa mahalia na wachungaji wao, hata katika wakati mgumu wa janga, wamejikita kusaidia watu mahalia katika matatizo yao kulingana na umaskini huo,  kwa mfano katika huduma za kiafya zilizo duni kabisa, ukosefu wa ajira na uhalifu mwingi sana.

Katika ya shughuli zilizo anzishwa kwa ajii ya wahitaji, Padre Lazo amezungumzia uzoefu wa Jimbo Kuu la Tegucigalpa, uliotwa  “dharura ya kimisionari”. Mpango huo unatoa mahitaji ya vyakula, matibabu, kisaikolojia na kiroho. Kwa ngazi ya kitaifa, ameeleza kuwa wakati wa janga wameweza kuwasaidia waamini wengi katika matatizo, kwa kutoa hata mafunzo ya kisaikolijia na kiroho kupitia mitandaoni. Maparokia mengi, makuhani na watawa bado wanaendelea kutoa utume wao ili ndugu wasio na bahati waweze kuhakikishiwa mambo msingi katika maisha yao.

Akizungumzia shughuli za PMS huko Honduras, Padre Bernardino amethibitishwa kuwa wataendelea kujipyaisha katika mwendelezo wa tabia za ufunguzi wa kimisionari hasa katika kuelekea kwenye sehemu za pembezoni mwa  kijamii na kiutamaduni na maisha. Wabatizwa wote wanaalikwa kutoa mchango wao hasa ya kuwa na  dhamiri za kimisionari kwa watu wa Mungu. Ni lazima kuanza safari kupitia uchungu, maumivu na matumaini ili kujibu vilio vyao, maswali yao njaa na shauku ya Mungu. Na zaidi lengo lao na jitihasa lazima zijikitjuu ya majibu kama uwezekano wa uwajibikaji wa utume wa ulimwengu wa Kanisa katika maeneo yote ya nchi kwa sababu bado kuna watu wengi ambao hawajuhi Mungu, amesisitiza Padre Lazo.

17 October 2020, 15:23