2020.08.06 Misa takatifu nchini Bolivia. 2020.08.06 Misa takatifu nchini Bolivia. 

Bolivia:Kanisa la Bolivia la waalika wakatoliki kukuza wito wa kimisionari!

Utume wa kila mbatizwa kwa mujibu wa msimamzi wa Kichungaji nchini Bolivia,Padre Enrique Quiroga,unapaswa utimizwe katika mantiki ya sasa ya kijamii,kisiasa,kifamilia na kiutamaduni.

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican

Kanisa linawaalika wakatoliki nchini Bolivia kukuza miito ya kimisionari katika Mwezi Oktoba wa kimisionari kwa maana  Neno la Mungu  linawaalika watu wote kuwa wafuasi katika safari ya kimisionari na kupeleka Habari Njema kwa jamii na kueneza ujumbe wa matumaini na faraja katika kipindi cha janga la corona. Kwa mujibu wa Maaskofu wa Bolivia aidha wanaalika waamini wote kuwa na mshikamano kwa ndugu wengi walioko pembezoni mwa maisha na kwa wote wanaoteseka kwa sababu ya mgogoro wa kiuchumi.

Wakatoliki kwa miezi hii ni lazima watafute kubaki hai dhamiri zao kimisionari yaani katika ulimwengu wa Kanisa katoliki. Ni lazima kuanza upya katika hatua za mafunzo ya kimisionari katika maisha na huduma ya Kanisa. Ni lazima  kuweka  moyoni mwao lile tangazo la Injili  na kusisitiza juu ya uongofu wa kimisionari na uinjilishaji katika jumuiya zote, ili kufanya kukuza upendo kwa ajili ya utume ambao ni upendo mkuu wa Yesu na wakati huohuo hata upendo mkuu kwa ajili ya watu wake.

Utume wa kila mbatizwa kwa mujibu wa msimamzi wa Kichungaji nchini Bolivia, Padre Enrique Quiroga, anasema unapaswa utimizwe katika mantiki ya sasa ya kijamii, kisiasa, kifamilia na kiutumaduni; ni vema kuendeleza furaha ya Injili na kuhamasisha wito wa kila mmisonari kwa kuiga na kufuata watakatifu na Bikira Mara ambao wanaendelea kuwatia moyo waamini wote ili wapeleke mbele furaha ya Injili katika maeneo yote ya maisha na kijiografika kama apendavyo kuhimiza Papa Francisko.

13 October 2020, 13:30