Assisi Jimbo linafuraha kubwa kuchaguliwa Padre Mauro!
Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican.
Furaha ni kubwa kwa uteuzi Kardinali Mteule Padre Mauro Gambetti Mfuransisikani Mkoventuali na Msimamizi wa Conventi Takatifu ya Assisi.Wanamshukuru Papa Francisko kwa ishara ya umakini na heshima na mapendo aliyopkea kwa kumteua kuwa Kardinali wa Kanisa takatifu la Roma. Ni katika barua ya Askofu Domenico wa Jimbo hilo. Katika barua hiyo inasema kuwa “Ni vizuri kuona mtoto wa Francis wa Assisi, ambaye kwa sasa ni Msimamzi wa Conventi Takatifu, kwa maana hiyo katika moyo wa maisha ya kifransiskani ulimwengunu kuitwa ili aweze kujikita katika shughuli yake karibu na Baba Mtakatifu , kwenye nafasi ya Baraza na msaada ambao ni wa Baraza la cha makadinali katika kuongoza Kanisa la ulimwengu. Padre Mauro alikuwa na anabaki, kwa muda mrefu iwezekanavyo, kama Kasisi wangu katika Kanisa kuu la Kipapa la Mtakatifu Francis. Pia katika nafasi hii nimekuwa naye kwa ushirikiano wa kiaminifu kwa miaka mingi katika Baraza langu la Maaskofu”.
Askofu Dominico wa Jimbo la Asisisi SSISI -Nocera Umbera-Gualdo Todino akiendelea na ufafanuzi kuhusu uteuzi huu amesema “Hitimisho la mamlaka yake kama Msimamizi wa Conveti Takatifu ulitarajiwa katika kipindi hiki, na kila kitu kilionesha uhamasishaji wake katika huduma ya Kanisa. Aina hii ya huduma muhimu sana na ya upendo ambayo Baba Mtakatifu amemwomba kwake yeye ni sababu ya heshima kwake na kwa familia za Wafransiskani, lakini pia furaha kwetu sisi sote, na kwangu mimi kwa njia fulani, kuunganishwa naye na hisia za mapendo na shukrani”, amesisitiza Askofu Domenico.
Chini ya uongozi wa Baba Mtakatifu Francisko, Kanisa leo hii linahisi hitaji kubwa la kufanywa upya kwa jina la “furaha ya Injili” na kusuka kwa upya roho ya familia, ya muungano na umoja. Katika hali ya tasaufi ya kifransiskani ya Padre Mauro ndiyo tumaini pia la uzoefu wake wa kichungaji katika Kanisa kuu hili ambalo linawaomba wazawa wa Mtakatifu maskini Francis kuwa katika kila aina ya huduma ya Baba Mtakatifu ambayo atapenda kuwapatia na iwe kwake msaada, faraja na msukumo kwake. Sala yetu kwa ajili yake imehakikishiwa. Lakini akumbuke kuwa Assisi kiukweli inabaki kuwa nyumba yake mara mbili .Mpendwa Kardinali mpya Mauro, tunakupenda. Na mkumbatio maalum kutoka kwa Askofu wako Domenico.