Vatican News
Kizazi kipya cha vijana kinaweza kubadili ulimwengu kwa mtazamo wa wakati ujao ulio bora Kizazi kipya cha vijana kinaweza kubadili ulimwengu kwa mtazamo wa wakati ujao ulio bora  (ANSA)

Wito wa Wcc kwa kizazi kipya cha vijana ili kuubadili ulimwengu!

Baraza ya Makanisa Ulimwenguni limetoa mwaliko kwa kizazi kipya cha vijana ambao wanayo maono ya kinabii kuwa na uwiano wa kawaida kwa ajili ya kubadili ulimwengu uweze kuwa bora zaidi.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Ikiwa Jumuiya imeweza kuweka Kipindi cha Kazi ya Uumbaji katika kalenda zao, maadhimisho ya mwaka huu katika wakati ambapo ulimwengu umekumbwa na mgogoro wa kiafya, uchumi na mazingira ambayo yanatetemesha ulimwengu mzima kuonya wakristo wote na wenye mapenzi mema kutafuta mbinu za kuishi zilizo na mzizi ya kweli mipya na ya kina. Ni mwaliko kutoka kwa Baraza la makanisa Ulimwenguni(Wcc), kwa namna ya pekee linalojikita katika jitihada za kuhamasisha matendo yote yote yaliyoanzishwa kwa mwezi huu maalum wa maombi na matendo ya kutunza nyumba yetu ya pamoja au mazingira.

Kwa mujibu wa muhimili huu wa kiekumene katika kuelekea kwenye uongofu wa kiekeoloja ili kubadili ulimwengu wanasema kuwa, inawezekana kweli kufika uongofu huo  hata kupitia kizazi kipya. Mwaka huu  kwa mfano Baraza la Makanisa Ulimwenguni (Wcc), wanakumbusha kuwa Kipindi cha Kazi ya Uumbaji kimeanza na huduma ya sala kwa njia ya mtandao inayoongozwa na vijana wenyewe. Kwa mujibu wa nafasi waliyo nayo ya kinabii, na  kwa njia ya kuwa na mitindo mipya ya kuhisi uwajibikaji huo, vijana wanashauri watu wazima wajikite ka nguvu zao zote na kwa haraka kwa ajili ya matendo ili kuokoa mtakabali wa maendeleo endelevu na amabo huko wazi.

Kwa kufafanua maana ya mwezi huu maalum Padre Ioan Sauca, mjumbe wa Kanisa ya kiorthodox wa Romania na Katibu Mkuu wa mpito wa Baraza la Makanisa Ulimwenguni WCC anaamini kuwa Kipindi cha Kazi ya Uuumbaji ni ni muafaka wa mfano wa roho ya kweli ya kiekumene katika kusali na kutenda kwa pamoja ili kukabiliana na changamoto za ulimwengu ambazo leo hii tunafanya uzoefu. Imani ni jambo msingi kwa ajili ya kubadili ulimwengu na kuufanya uwe endelevu na haki. Kwa mujibu wa mhusika wa Baraza la Makanisa ulimwenguni (Wcc) Mchungaji Henrik Grape, anasema ekolojia, uendelevu na haki ya tabianchi ni kile ambacho toleo la mwaka 2020 kinajikita nacho kwa namna ya pekee kwa wote, yaani Nchi zote ulimwenguni, ambazo kwa hali halisi tumekumbwa na Covid-19 kwa ghafla, na wote tunapaswa kubadilika na kwa walio wengi, pia  kwenda pole pole.

Katika sababu za mahitahi ya mabadiliko ya kweli ndipo mchungaji huyo wa Sweeden anawaalika wakristo kwa madhehebu mengine kukutana juu ya muhimu wa kutambua kuwa ni lazima pia kufanya jubilei maalum ambayo inasaidia kwenda pole pole na kubadilisha tabia zetu. Hata hivyo maelekezo kadhaa pia yanaonesha kwenye tovuti ya Wcc kutoka kwa Mkuu wa Kanisa la Kigiriki-Kiorthodox nchini Zimbawe, Askofu Mkuu Serafim ambaye anasema  ni lazima kufanya mazoezi hasa ya maisha ya heshima, lakini pia ya kujitolea, kujinyima, unyenyekevu na  kutafuta maadili ya jumla ili kuifanya dunia iweze kuwa nzuri zaidi  hasa tuliyopewa na ili hatimaye tuweze kuirudisha kwa Mwenyezi Mungu.

Hatimaye, anashauri kiongozi huyo wa kiorthodox kuwa haipaswi kusahau vitu vidogo vidogo kuwa ni muhimu na haipaswi kupuuzwa, kwa sababu mbele za Mungu, mambo yote ni muhimu. Katika kipindi chote cha tukio la Kipindi cha Kazi ya Uumbaji kitakachomalizika tarehe 4 Oktoba ijayo katika Siku kuu ya Mtakatifu Francis wa Assisi, mambo mengi sana yatafanyika hasa mikutano ya kidigitali kuanzia  Nanyuki nchini Kenya, mahalia ambapo itapandwa miti ya matunda ili kulinda msitu wa mazingira ulio katika hatari, hadi Rio de Janeiro, nchini Brazil, mahali palipo na msitu mkubwa wa Amazonia, vile vile kuelekea huko Wellington, New Zealand, mahali ambapo kikundi cha kiekumene kitajitahidi kufanya tafakari kuhusu historia ya uumbaji kwa mujibu wa Maandiko matakatifu ya ya Biblia ya Kitabu cha Mwanzo.

07 September 2020, 08:39