Tafuta

Waamini nchini  Vietnam wanaendelea na matatizo ya kiuchumi na janga la virusi Waamini nchini Vietnam wanaendelea na matatizo ya kiuchumi na janga la virusi 

Vietnam#coronavirus:Kanisa kuwa karibu na waathiriwa Covid-19

Nchi ya Vietnam inaendelea kupitia kipindi kigumu cha mgogoro wa uchumi uliosababishwa na janga la kiafya,na serikali hiyo imetangaza mpango mwingine wa kusadia kifedha kwa wasio kuwa na fursa kufikia mwishoni mwa 2020.Na wakati huo huo Kanisa liko karibu na watu wenye matatizo ambao wamesahauliwa.

Na Sr Angela Rwezaula- Vatican

Jitihada za Kanisa zinaendelea kuwa karibu sana na waathiriwa wa covid-19 waliosahuliwa. Nchi inaendelea kupitia kipindi kigumu cha mgogoro wa uchumi uliosababishwa na janga la kiafya, na serikali ya vietnam imetangaza mpango mwingine wa kusaidia kifedha kwa wasio kuwa na fursa kufikia mwishoni mwa 2020. Mwezi Aprili mwaka huu, Waziri Mkuu Nguyen Xuan Phuc alikuwa ametangaza msaada wa dong trilioni 62 zenye thamani ya (euro bilioni 2.26), kulipwa kwa watu karibu milioni 20. Lakini kiasi kilichosambazwa, kilikuwa ni chini kuliko kile kilichotangazwa na kwa maana hiyo haikumnufaisha kila mtu, kwa sababu ya taratibu kuwa ngumu na ufisadi wa serikali za mitaa.

Sr. Marie Do Thi Quyen, wa Shirika la  Masista wapenda Msalaba Mtakatifu, katika wilaya ya Lai Chau, ameripoti jinsi wanakijiji wa Hmong walijikuta wamenyimwa kabisa riziki wakati wa shida, huku wakishindwa kwenda kufanya kazi mahali pengine au jirani na China. Mnamo Mei kwa mujibu wa  mtawa huyo amesema,  ​​wasichana watatu wa Hmong walikufa vibaya baada ya kula uyoga wenye sumu, wakati wazazi wao walikuwa mbali na nyumbani. Watu wengi, wakiwa wanangoja mavuno, kiukweli wanalazimika kukusanya matunda na mboga kwenye misitu ili kupata mlo. Kutokana na msaada mdogo wa kifedha kutoka kwa wafadhili, pia walioathiriwa na janga hilo, hata watawa hawa hawana chochote cha kuwasaidia watu hawa kupata chakula. “Mungu amalize ugonjwa huo hivi karibuni ili wafadhili waweze kuja kutembelea na kusambaza chakula cha msingi kwa wakazi wa eneo hilo”,  amesema  Sr. Quyen.

Naye  Padre Joseph Nguyen Tien Lien, mchungaji wa parokia ya Mai Yen, katika jimbo la Son La, ambalo lina makazi ya makabila mengi , amesimulia jinsi wagonjwa waliop katika hospitali za mitaa wanateseka kwa sababu ya ukosefu wa chakula na jinsi vikundi vya Wakatoliki bado wanavyoweza kupeleka vifaa kwa mamia ya wagonjwa na jamaa zao, lkini yote hiyo ni shukrani kwa msaada wa wafadhili.

Padre Vincent Vu Ngoc Dong, mkuu wa Caritas Jimbo kuu la Ho Chi Minh anawaalika watu wa eneo hilo kutoa misaada wakati wa fursa ya Tamasha la Katikati ya Vuli, ambayo  kwa kawaidi ni siku kuu kubwa zaidi ya kila mwaka kwa watoto, ambapo mwaka huu itafanyika tarehe 1 Oktoba 2020. Katika fursa hiyo Caritas ina mpango wa kuandaa matukio kadhaa kwa ajili ya watoto walio na shida kubwa, hasa wale walioathiriwa na Covid-19.

Hatimaye Askofu Mkuu Joseph Nguyen Nang wa Jiji la Ho Chi Minh amewaalika Wakatoliki kufanya kazi na watu kutoka matabaka yote ya maisha na kutoa msaada wa vifaa na  kisaikolojia kwa wagonjwa na wale wanaoishi katika umaskini. “Tunapaswa kuonyesha kwamba sisi ni mitume wa Yesu, tunatoa misaada kwa ukarimu na tunaelezea mshikamano wetu na wengine”. Kwa maana hiyo amewasihi watu waombee pia ulimwengu ili kushinda janga baya, kwani dini ni roho ya maisha ya mwanadamu na bila hiyo wanaume watapoteza mwelekeo na hawatajua wapi waende.

17 September 2020, 16:55