Tarehe 22 Novemba 2020 ni matarajio ya kukabidhi msalaba wa Vijana kwa Vijana wa Lisbon Tarehe 22 Novemba 2020 ni matarajio ya kukabidhi msalaba wa Vijana kwa Vijana wa Lisbon 

Ureno:Tarehe 22 Novemba Vijana wa Lisbon watakabidhiwa Msalaba

Itakuwa Jumapili ya siku kuu ya Kristo Mfalme wakati Msalaba wa Siku ya Vijana(WYD)utakabidhiwa hatimaye kwa vijana wa Lisbon.Kwa ishara hii, mbayo kawaida hufanyika Jumapili ya Matawi,lakini mwaka huu imeahirishwa kutokana na janga la covid,kwa maana hio vijana wa Lisbon wataanza kupumua hali nzuri ya Siku ya Vijana Duniani 2023.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Itakuwa ni tarehe 22 Novemba 2020 katika, sherehe ya Kristo Mfalme, hatimaye Msalaba wa Siku ya Vijana Ulimwenguni utakabidhwa kwa  vijana wa Lisbon. Kwa ishara hii, ambayo kawaida hufanyika Jumapili ya matawi na ambayo kwa mwaka huu iliahirishwa kwa sababu ya janga la covid-19, na kwa maana hiyo vijana wa Ureno kwa mara nyingine furaha yao inarudi tena pia wataanza kupumua Siku ya Vijana Duniani. Hata hivyo ilikuwa ni Jumamosi tarehe  5 Septemba 2020, wakati wa kufungua mwaka mpya wa kichungaji, maandalizi ya tukio hili yalianza kwa mara nyingine tena,  siku ambayo iliahirishwa hadi mwaka 2023 kwa sababu ya janga la ugonjwa wa corona. Rais wa Mfuko wa Siku ya Vijana (WYD) mwaka 2023 ni Askofu Américo Aguiar, ambaye amethibitisha kwamba hata Papa Francisko anafuatilia matayarisho ya Siku ya Vijana Duniani kwa  furaha na utulivu.

Akizungumza na wakala wa Kanisa Katoliki nchini Ureno, Askofu  Aguiar pia ameelezea kuwa hadi sasa maandalizi ya Siku ya Vijana duniani WYD yamefanywa kwa kimya kimya, kwa sababu kipaumbele kimepewa mshikamano zaidi wa janga. Katika mkutano wa tarehe 5 Septemba 2020  hata hivyo ulikuwa ni mkutano wa kwanza wa kikundi kinachofanya kazi, kilichoundwa na vitengo  saba kutoka maeneo tofauti, na kiongozi wake ni mlei, kuhani kama msaidizi wa Kanisa na pia kijana ambaye atafanya kazi kama katibu mtendaji. Ni kundi hili ambalo litaanza kufafanua kwa kivitendo hatua zote zitakazo chukuliwa kuandaa vizuri Siku ijayo ya Vijana Duniani.

Kundi hili halianzii mwanzoni kabisa kwa maana mara baada ya tangazo la Papa Francisko kwamba Siku ya vijana (WYD) itafanyika Lisbon, kulikuwa na mikutano mbalimbali na Kamati za kuandaa ya majimbo 20 ya Ureno na  moja tawala la jeshi. Kukabidhiwa Msalaba wa WYD; kama ilivyoelezwa, itafanyika tarehe  22 Novemba. Kiutamaduni mwaka unaofuata, toleo la kimataifa la Siku ya Vijana WYD, Msalaba na Picha ya Bikira Maria vinakabidhiwa na vijana wa majimbo ambapo toleo lijalo la kimataifa hufanyika. Ni utamaduni ulioanza tangu mwaka mnamo 1984, wakati, mwishoni mwa Mwaka wa Jubilei ya Ukombozi, Mtakatifu Yohane Paulo II alipoukabidhi Msalaba wa Jubilei kwa vijana, akiwaomba kuubeba na kuupeleka ulimwenguni, kama ishara ya upendo wa Bwana Yesu kwa wanadamu na watangaze kwa kila mtu kwamba ni katika Kristo tu aliyekufa na kufufuka kuna wokovu na ukombozi.

Picha ya Bikira Maria ni mfano wa Picha ya ‘Maria Salus Populi Romani’, yaani “Maria Afya ya watu wa Roma,  asili yake inasemekana imechorwa na Mtakatifu  Luka na ambayo imehifadhiwa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu  Maria Mkuu Roma. Mtakatifu Yohane Paulo II aliikabidhi picha hii kwa vijana mnamo mwaka 2003. Kwa mujibu wa Askofu Aguiar ameisitiza kuwa hali hiyo ya makabidhiano haitabiriki na wanafanya kazi kwa ushirikiano na Vatican na Panama ambayo inapaswa kuhamisha ishara hizo, kila siku, kwa kusoma nyakati na kuwa na busara. Kwa sasa, ndiyo, wanaendelea kufanya ilimwaweze kweli kushirikiana kwa kazi, wakati wa kuheshimu mahitaji ya vijana.

15 September 2020, 13:53