Tafuta

Vatican News
Vijana wanakusudia kupigania umoja kwa sababu ndiyo njia pekee ya kujibu changamoto juu ya mazingira yanayotokana na ulimwengu unaojilimbikizia mali. Vijana wanakusudia kupigania umoja kwa sababu ndiyo njia pekee ya kujibu changamoto juu ya mazingira yanayotokana na ulimwengu unaojilimbikizia mali.  

Ulaya:Vijana wa Leuca waomba mshikamano wa kimediterranea!

Hivi karibuni umefanyika mkutano wa vijana kwa njia ya mtandao kwa kuhitimisha na hati yao waliyoipa jina"vijana ustambulisho wa leuca 2020",huku wakisisitiza juu ya mshikamano kuhusu masuala ya kimediterranea.Wanakusudia kupigania umoja kwa sababu ndiyo njia pekee ya kujibu changamoto juu ya mazingira yanayotokana na ulimwengu unaojilimbikizia mali

Na Sr. Angela Rwezaula Vatican

Katika hati moja iliyoandikwa na washiriki wa mkutano kwa kuipatia  jina “Carta di Leuca 2020” au utambulisho wa vijana wa Leuca mwaka 2020 wanasema “Tunakusudia kuwa mashuhuri katika kupigania umoja kwa sababu ndiyo njia pekee ya kujibu changamoto juu ya mazingira yanayotokana na ulimwengu unaojilimbikizia mali huku ukiwaacha watu wengi hawana ajira”. Kongamano hili lilikuwa ni toleo la 5 la   vijana kwa ajili ya kuimarisha umoja na mahusiano na kujenga amani katika ukanda wa Mediterranea lililofanyika kwa njia ya mtandao wiki iliyopita. Katika hati yao ya mwisho ya washiriki hao(Cartadileuca 2020) wa Ukanda wa Mediterranea kwa kuundwa na  mtandao kwa ushirikiano wa vikundi vya vijana kwa ajili ya amani wamethibitisha kukazania umoja na amani

Kongamano hili lililoandaliwa kwa umoja wa  Jimbo la Ugento Santa Maria di Leuca na Ushirikiano  wa Tamaduni za mbuga na maeneo ya Miji ya Leuca  nchini Italia lakini hata  wafanyakazi wa kudumu wa  Tamaduni za kimataifa na mahusiano ya kidini, na kwa maana hiyo kongamano hilo limejumuisha mamia ya vijana kutoka sehemu mbalimbali za nchi za kimediterranea.  Katika maazimio ya Kongamano hilo linawataka vijana kudumisha umoja kama ujumbe maalum unaopaswa kupelekwa kwa kila Taifa, kila mila na dini huku wakihamasisha kila kijana kujenga moyo wa umoja, wakiwa na ndoto ya kuboresha maisha yajayo na kujiepusha na hila za ulimwengu wa sasa, kwa kuimarisha ujirani na dhamira ya kuheshimu historia ya mtu na maisha yake ya kijamii.

Hatimaye katika hati ya utambulisho wa Leuca 2020 (Carta di Leuca 2020) inawatangazia  wakazi wote wa Mediterania kuwa na moyo wa ukarimu wenye sura yenye utajiri wa tunu za kiutu, kupokeana na kusaidiana katika kuvuka majanga na changamoto mbalimbali za maisha, wakishirikiana kuujenga moyo endelevu wa umoja unaotafuta mafao ya wote.  Hivyo, wanasisitiza kuwa vijana wasisite kukutana na wenzao katika kuimarisha mahusiano yao na udugu unaovuka mipaka ya ubaguzi na utengano. Kwa umoja wao wanameonesha dhamira yao njema ya kukutana mara kwa mara na kuimarisha mahusiano yanayokuza utu.

02 September 2020, 13:25