Watu wengi barani Afrika, Asia, Amerika Kusini na Ulaya ya Mashariki wanahitaji msaada na wanapaswa kutegemea mshikamano wetu wa kidini ulimwenguni Watu wengi barani Afrika, Asia, Amerika Kusini na Ulaya ya Mashariki wanahitaji msaada na wanapaswa kutegemea mshikamano wetu wa kidini ulimwenguni 

Ujerumani#coronavirus:siku ya sala na mshikamano kwa ajili ya wagonjwa!

Kanisa nchini Ujerumani Dominika tarehe 6 Septemba 2020 linajiandaa kufanya Siku ya maombi na mshikamano kwa ajili ya wagonjwa,ambapo Askofu Bätzing anasema mshikamano pia njia ya mazoezi ya kweli.Watu wengi barani Afrika,Asia,Amerika Kusini na Ulaya ya Mashariki wanahitaji msaada na wanapaswa kutegemea mshikamano wa kidini ulimwenguni.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Dominika tarehe 6 Septemba 2020, itafanyika siku ya maombi na mshikamano kwa ajili ya wagonjwa wa virusi vya corona ambapo Kanisa zima katoliki la Ujerumani linajiandaa kufanya hivyo. Ni taarifa kutoka kwa baraza la Maaskofu Ujerumani kupitia matika Tovuti yao. “Wakati watu wanaishi katika tishio na hatari, sula la kichungaji kwa namna ya pekee ni muhimu na sisi kama wakristo hatupaswi kukosa upendo wa dhati”, anaandika barua hiyo Rais wa Baraza la Maaskofu Ujerumani Askofu Georg Bätzing kattika fursa hiyo wale wote ambao walisaidia wengine na kuwafanya wahisi nao matumaini ya kikristo wakati wa miezi mibaya ya mgogoro  wa viruso na ambao wanastahili shukrani kubwa.

Maaskofu wanasisitiza kuwa wakatoliki wa Ujerumani wamejifunza kwa makumi ya miaka sasa kutoa umakini wao hata kwa mahitaji ya sehemu nyingine ulimwenguni. Virusi vya corona vimewakumba maskini kwa ugumu sana,  miongoni mwao wengi ni vigumu kujilinda na virusi, kutokana na kwamba hawana nyenzo na vifaa vya kiafya; zaidi ya hayo, mamilioni na mamilioni ya watu wanatishiwa na njaa kwa sababu hawawezi tena kujipatia riziki yao. “Watu wengi barani Afrika, Asia, Amerika Kusini na Ulaya ya Mashariki wanahitaji msaada na wanapaswa kutegemea mshikamano wetu wa kidini ulimwenguni”.

Parokia na waamini, kwa njia hiyo, wanaalikwa  na Kanisa la Ujerumani kushiriki katika siku ya Jumapili hiyo  kwa sala na mshikamano pia kwa matendo ya dhati: “Ninawaomba kusherehekea siku hii katika parokia zenu, hasa wakati wa Misa. Tuwaombee maskini ulimwenguni kote, walioathiriwa sana na janga hilo.  Tuombe pamoja nao pia tuwaonyeshe mshikamano wetu kwa njia inayofaa, kwa kufanya  kwamba msaada wa siku hiyo na kampeni ya kutafuta fedha inayoambatana na mafanikio”, amesisitiza Askofu Bätzing.

Hata hivyo vifaa mbali mbali kuhusiana na kampeni hivyo na taarifa zaidi unaweza kufungua ukurasa wao wa Tovuti: www.weltkirche.de/corona-kollekte Na namba ya account maalum imefunguliwa kwa ajili ya kampeni ya michango iliyoelekezwa Kanisa huko Ujerumani ambayo itatumika kusaidia kazi zake za kikanisa na zinazohusiana na kimataifa ili kusaidia mapambano dhidi ya virusi vya Corona au covid-19.

04 September 2020, 13:31