Mpambanano dhidi ya adui hasiyeonekana wazi covid-19 Mpambanano dhidi ya adui hasiyeonekana wazi covid-19 

Marekani:Chukueni hatua za haraka kuwasadia wahanga wa covid-19

Tumejipanga kupambana na hili gonjwa la kiulimwengu,huku tukiboresha utendaji kazi wetu na ukarimu wetu kwa wahitaji na tukijikita katika malezi,sala na utoaji wa huduma za kisakramenti kwa jamii ya wakristo.Ndiyo maneno ya Askofu Mkuu wa Los Angeles katika ujumbe aliotumwa kwa aatizoz zote za kitaifa nchini Marekani.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Askofu Mkuu José H. Gomez, Askofu wa Jimbo Kuu Katoliki la Los Angeles nchini Marekani katika ujumbe wake alioutoa kwa njia ya mtandao wa kiaskofu amewataka viongozi wote wa taasisi  katoliki nchini Marekani, taasisi za Caritas, Taasisi za kitaifa za elimu, Chuo kikuu cha Mtakatifu Vincent wa Paulo nchini USA, na Jumuiya zinazotoa huduma kwa wakimbizi, kuchukua hatua za haraka katika kuwasaidia wahanga walio katika mahitaji makubwa yaliyosababishwa na janga la Corona. Waraka huo ulioandikwa na pia kutumwa kwa  Rais wa Marekani Bwana Donald Trump unaelezea matatizo mazito yaliyosababishwa na janga la Corona nchini Marekeni na wenye kutoa wito wa majitoleo ya kipekee kwa taasisi za Kanisa Katoliki ili ziweze kutoa misaada na ushirikiano na malezi ya kiroho kwa taasisi ya Afya.

Katika kutoa wito huo Askofu José Gomez amesema, Taifa Marekani liko katika mahangaiko makubwa huku takribani watu laki mbili wakiwa wamepoteza maisha yao na Wamarekani milioni 30 wakikosa makazi, na wafanyakazi wa Idara ya Afya wakiendelea kupambana na wimbi hilo la Corona. Hivyo, viongozi wanapaswa kujitoa zaidi. Aidha, viongozi mbalimbli wa Kanisa Katoliki nao wameandika kwamba, “Tumejipanga kupambana na hili gongwa la kiulimwengu, huku tukiboresha utendaji kazi wetu na ukarimu wetu kwa wahitaji na tukijikita katika malezi, sala na utoaji wa huduma za kisakramenti kwa jamii ya wakristo”.

Zaidi ya hayo, Shule, Vyuo na Parokia nyingi zilifungwa kwa muda kupisha maandalizi na mikakati ya kupambana na Janga la Corona au covid-19. Katika harakati za kufunguliwa kwa taasisi hizi za kielimu, wito mkuu unaotolewa na viongozi wa Kanisa ni ule wa kuhudumiana.  Takwimu zinaonesha kuwa zaidi ya mamilioni ya watu wamekumbwa na janga la njaa.  Jitihada za kila mmoja zinahitajika kutolewa ili ziwafikie walengwa. Papo hapo, wito kwa vyama na Serikali umetolewa ili kuweka kipaumbele cha kuwahudumia wahitaji waliokumbwa na maafa na kujitahidi ili kila mmoja asipotee kwa kukosa mahitaji yake ya msingi.

30 September 2020, 13:25