Misalaba Misalaba  

Polisi waondoa misalaba 15 katika Serikali ya Karnataka nchini India!

Masikitiko katika Kanisa Mahalia kwa ajili ya maamuzi ya Mahakama Kuu ya Serikali ya kuondoa misalaba katika Serikali ya Karnataka nchini India,kwa kizingizio cha kuisimika bila ruhusa.Operesheni kama hiyo ilikuwa tayari imefanyika hata mnamo Machi.Wakristo wanahisi kulengwa kutokana na hisani zinazokusudiwa kukomboa maskini.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tarehe 23 Settembre iliyopita, Polisi wa Serikali ya Karnataka wameondoa misalaba 15 katika vilima karibu na Kanisa Katoliki la Mtakatifu Yosefu wa Susai Palya, Wilaya ya Chikaballapur, kwa kuwashtumu wakristo kuwa walivamia eneo la Serikali na kusimika misalaba hiyo  bila kuwa na  ruhusa.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka shirika la habari za Kanisa, (UCA), wanasema hata hivyo Parokia itaendelea na mchakato wa kisheria wa kutaka kurudishiwa misalaba yao. Kwa kutii agizo kutoka Mahakama Kuu ya Jimbo, polisi zaidi ya 300 na maafisa wa ushuru, katika operesheni ya masaa sita, waliondoa msalaba wenye urefu wa mita 32 na misalaba mingine 14 yenye urefu wa mita saba katika nafasi iliyotumiwa na Parokia ya Mtakatifu Joseph kwa zaidi ya miongo mitano wakati wa kipindi cha Kwaresima kusali Njia ya Msalaba.

Hata hivyo Maafisa wa serikali walifanya kiholela bila ya kutaarifu  kwa mujibu wa, Padre Antony Britto Rajan, akizungumza na shirika la habari (UCA) huku, akielezea jinsi mamia ya waamini wa Kanisa hilo walivyoshuhudia kitendo hiki kwa mshtuko na hofu. Serikali ya chama kinachounga mkono Uhindu Bharatiya Janata Party (BJP), inayoshtakiwa kwa kuunga mkono vikundi vya Wahindu, inawalenga Wakristo kwa makusudi, ikipinga kazi za hisani zinazolenga ukombozi wa jamii ya maskini na waliotengwa.

Katika operesheni kama hiyo mnamo Machi iliyopita, tayari, polisi waliondoa sanamu ya Kristo na misalaba 14 kutoka kwenye eneo la mazishi ya kikristo kwenye kilima cha Mahima Betta wilayani Bengaluru. Pia katika tukio hiyo polisi walikuwa wamesema kwamba Wakristo walikuwa wamevamia eneo la Serikali. Askofu Peter Machado, wa Jimbo kuu la Bangalore, amesema kuwa mwezi Machi walitoa taarifa kuhusiana na   tukio hilo, huku akielezea matumaini kwamba Serikali ya jimbo itatoa maagizo kwa Serikali za mitaa ili waweze kufanya kitendo cha kulipiza mara moja kwa kurudisha misalaba. Lakini baada ya miezi saba, Serikali haikufanya chochote na, badala yake, imeondoa nyingine 15.

29 September 2020, 11:51