Tafuta

Vatican News
 Papa Francisko kukutana na waamini wa Papua  Guinea Mpya 30.07.2019 Papa Francisko kukutana na waamini wa Papua Guinea Mpya 30.07.2019 

Papua Guinea Mpya-Miaka 45 ya uhuru:Uhuru usichanywe na kutengwa!

Kufuatia na mchango na msaada ambao umetolewa kutoka mashirika ya kimaendeleo nchini Papua Guinea Mpya na visiwa vya Solomoni,imedhihirisha wazi ya kwamba uhuru hauna manaa kuchanganya na kutengwa kwa maana Nchi zote zinahitajiana kusaidiana moja na nyingine.Haya yamesema na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Nchini humo wakati wa kuadhimisha miaka 45 ya uhuru wa nchi.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu wa Paua Guinea Mpya na Visiwa vya Solomoni Padre Giorgio Licini, PIME, katika fursa ya maadhimisho ya miaka 45 ya Uhuru wa Nchi katika taarida iliyotolewa kwenye Tovuti ya Baraza hilo ameonesha shukrai kubwa kwa Mungu Mwenyezi kwa sababu ya kuwaepusha na kipinidi hiki kigumu cha janga wazalendo wadhaifu na zaidi walio wazee katika nchi, na kushukuru mashirika ya maendeleo ambao walikuja kuwaokoa na vifaa vyao vya matibabu na utaalam kwa haraka. “ Kwa mujibu wa Padre Licini “ Yote hayo bado yanaonesha kwa mara nyingine tena kuwa uhuru haipaswi kuchanganywa na kutengwa. Nchi zinahitajiana moja na nyingine na lazima kusaidiana hasa wakati wa vipindi vigumu.

Nchi, ambayo ilipata uhuru kamili mnamo tarehe 16 Septemba 1975, ndani ya Jumuiya ya Madola, bado inajitahidi  kupambana katika kuhakikisha haki ya kupata elimu kwa watoto wote, kuboresha mfumo wa afya, kutatua shida za maendeleo na ukosefu wa miundombinu, pamoja na shida ya unyanyasaji wa kijinsia na unyanyasaji wa nyumbani. Migogoro ya kifamilia, pamoja na mambo mengine, inasukuma idadi inayozidi kuongezeka ya watu kwenda mbali na nchi zao. Kwa njia hii, katika vituo vya mijini vimezidi kujaa watu na kushindwa kutoa fursa za kazi na kudhibiti uhalifu mdogo.

Kwa mujibu wa Padre Licini anasema “Inahitaji umoja na ushirikiano ili kushinda changamoto,  huku akitumaini kwamba serikali itakuwa na bidii katika nyanja ya kijamii. “Demokrasia haiishii siku ya uchaguzi tu, baada ya hapo wabunge hawaonekani katika maeneo yao, na mawaziri wa serikali wanajificha nyuma ya milango iliyofungwa huko na kupunguza mwingiliano na umma kadiri inavyowezekana. Kuna mahitaji sana ya uwazi na ushiriki ambao unaweza tu kuweka misingi ya kiwango kipya cha maendeleo ya kitaifa na uhuru, amehitimisha.

16 September 2020, 13:06