NIGERIA-Maandalizi ya gwaride ya kijeshi kwa ajili ya sherehe za miaka 60 ya uhuru nchini Nigeria tarehe Mosi Oktoba NIGERIA-Maandalizi ya gwaride ya kijeshi kwa ajili ya sherehe za miaka 60 ya uhuru nchini Nigeria tarehe Mosi Oktoba 

Nigeria:Unahitajika uongozi wenye uwezo wa kuunganisha Nchi huru

Katika ujumbe wa Askofu Mkuu Alfred Adewale Martins,wa jimbo kuu katoliki Lagos nchini Nigeria katika fursa ya Siku ya uhuru wa nchi hiyo tarehe Mosi Okotba,anaandika kwamba ni lazima kuwa na uongozi wa kuunganisha Nchi na kuhakikisha usalama katika nchi ambayo kiukweli imegawanyika kikabila na kidini.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika fursa ya Siku kuu ya Uhuru nchini Nigeria, Askofu Mkuu Alfred Adewale Martins, wa jimbo kuu katoliki Lagos nchini humo ameandika waraka wake kuwa  ni nchi yao yenye uhuru lakini ambayo bado inatafuta kuwa taifa moja ili pasiwepo hata mmoja anayekandamizwa na wote wanayo maana ya kuwa sehemu moja ya nchi.  Katika kutathimini nchi yake  kwenye ujumbe huo alioutoa katika fursa ya  kusheherekea mwaka wa 60 tangu nchi hiyo ipate uhuru wake, tarehe 1 Oktoba, anaangazia hasa wahusika wakuu  wanaoongoza nchi  ya Nigeria ambapo anathibitisha kwamba licha ya kufikisha  miaka 60 lakini bado haijawa na uwezo wa kuimarisha hisia za umoja wa kitaifa katika Nchi. Hii ni kutokana na kwamba kiukweli nchi hiyo imegawanywa na mivutano ya kikabila, kidini na ambayo inatishiwa na ukosefu wa msimamo ambao umesababisha ukosefu wa maendeleo. Kwa mujibu wa Askofu Mkuu anasema nchi ya Nigeria bado inasubiri kupata uongozi wenye sifa za lazima za kuiongoza katika njia ya kuishi kwa amani, matarajio ya kiuchumi na kuhakikisha usalama wa watu na mali zao.

Viongozi wa Nigeria wanalaumiwa hasa kwa kutokana na kuendelea kuwapo ukosefu wa usalama na kulaumiwa  mara kwa mara katika miaka ya hivi karibuni na maaskofu wa Nigeria na makanisa ya Kikristo; aidha ukosefu wa usalama wa kiuchumi ambao janga la Covid-19 limechangia kwa kiasi kikubwa, na kufanya maisha yasiyowezekana kwa wale ambao wamepoteza kazi na maisha yao. Kwa mujibu wa ujumbe huo, unasema maisha yanazidi kuwa magumu kwa Wanageria wengi; Kiongozi huyo pia  anamlaumu kiongozi wa nchi hiyo  ambaye pia anakosoa uamuzi wa serikali hivi karibuni wa kuongeza ushuru mwingi, pamoja na ushuru wa nishati na kumtaka achukue hatua kali za kupunguza uzito ulioko juu ya mabega ya Wanigeria, kuanzia na kupunguza gharama za kisiasa.

Askofu Mkuu Adewale anatoa wito kwa asasi za kiraia na vyama vya wafanyakazi ili kuhamasisha mamlaka kuweza  kutambua shida za idadi ya watu wanaozidi kuteseka. Kwa mujibu wa Askofu Mkuu wa Lagos, shida pia ni mfumo wa sasa wa shirikisho, ambao ni matokeo  tawala za kijeshi zilizopita, ambazo zimetoa nguvu nyingi kwa serikali kuu kupunguza majimbo na serikali za mitaa kwa nyongeza ya Abuja. Kwa hili linaongezewa na ubinafsi na ukosefu wa heshima kwa faida ya wote na ya makabila tofauti yanayounda Nigeria. Yote hayo yamefanya kutoweza kutimilizika ukamilifu wa Jamhuri ya Shirikisho lililozaliwa na uhuru amesisitiza Askofu.  Kwa njia hiyo Askofu Mkuu anahitimisha kwa wito wa kuweza  kurudi kwenye shirikisho la kweli la asili ya kuwa taifa linalotamani kuwa nchi iliyoungana katika utofauti, ambayo hakuna mtu anayedhulumiwa na kila mtu anajivunia kutumikia nchi yao huru.

Nigeria ilipata uhuru wake kutoka kwa ukoloni kwa Uingereza mnamo 1 Oktoba 1960, na kuunda shirikisho la mikoa mitatu (Kaskazini, Magharibi, Mashariki), kwa misingi ya kikabila, kama vile vyama vikuu viliundwa kwa misingi ya kikabila. Kufuatana na tawala tofauti za kijeshi nchi inaendelea kugawanywa na mivutano ya kikabila na kidini, hasa kati ya Wakristo na Waislamu, mivutano ambayo ilizidi kuwa mbaya baada ya kuingia kwenye eneo la tukio, la kigaidi kwa zaidi ya miaka kumi iliyopita, ya kikundi cha Kiislam cha Boko Haram, ambacho vurugu za umwagaji damu zipo tangu 2009 na ambazo zimesababisha wathirika zaidi ya 35,000.

29 September 2020, 11:42