Wiki ya Haki kijamii 2020” nchini New Zealand inaanza tarehe 6 hadi 12 Septemba.Viongozi wa Kanisa  wanaangazwa na Mafundisho ya Kanisa kama Lensi ya kipekee inayoruhusu kutoa maana katika ulimwengu unaobadilika Wiki ya Haki kijamii 2020” nchini New Zealand inaanza tarehe 6 hadi 12 Septemba.Viongozi wa Kanisa wanaangazwa na Mafundisho ya Kanisa kama Lensi ya kipekee inayoruhusu kutoa maana katika ulimwengu unaobadilika 

New Zealand:mafundisho jamii ni lenzi yenye maana katika dunia geugeu!

Maaskofu katoliki nchini New Zealand katika Ujumbe wao kwenye fursa ya Wiki ya haki kijamii wanasema Mafundisho jamii ya Kanisa ni lensi ambayo inatoa maana katika ulimwengu unaobadilika.Wiki hii inaanza tarehe 6 hadi 12 Septemba.Mafundisho jamii ya Kanisa yamekita mizizi katika Maandiko Matakatifu na katika majisterio ya kipapa, ambapo husaidia kutekeleza maadili ya kiinjili kama upendo,amani,haki na huruma

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Lensi ya kipekee ambayo inaruhusu kutoa maana katika ulimwengu unaobadilika ni Mafundisho jamii ya Kanisa kama ilivyoelezwa na Baraza la maaskofu katoliki wa New, Zealand walivyotangaza kwa mtazamo wa “Wiki ya Haki kijamii 2020” itakayoanza tarehe 6 hadi 12 Septemba. “Haijawahi kutokea hadi sasa mafundisho jamii Katoliki kufaa zaidi, sio tu katika nchi yetu, bali pia katika ulimwengu wote. Kuanzia namna ya kutafuta majibu ya janga la Covid-19 kwa utambuzi mkubwa wa uwepo wa ubaguzi wa rangi, dhuluma na tofauti zinazoongezeka za kijamii na kiuchumi, kwa maana hiyo Mafundisho jamii  ya Kanisa hutusaidia kuzingatia wasiwasi wetu juu ya ulimwengu na kutoa maana katika mabadiliko yake”, wanaandika Maaskofu wa New Zealand.

Kwa kufafanua zaidi maana kamili ya wiki hii viongozi hawa wanasema:“Mafundisho jamii ya Kanisa yamekita mizizi katika Maandiko Matakatifu na katika majisterio ya kipapa, ambapo hutusaidia kutekeleza maadili ya kiinjili kama vile upendo, amani, haki, huruma kujibu shida kama vile umaskini, kukosa makazi, njaa, migogoro, uhamiaji, upatikanaji wa bidhaa msingi na utunzaji wa mazingira” .

Hata hivyo Wiki ya haki kijamii itaongozwa na kauli mbiu isemayo: “ni rahisi kama Mafundisho ya Jamii:kutoa vizuizi vya uwezo wa Kanisa”. Hili hata hivyo ni chaguo lisilo la kubahatisha, kwani maaskofu wanasisitiza, wakizingatia wakati wa sasa wa kihistoria!  "Janga la virusi vya corona kiukweli, limefunua udhaifu wa kila mmoja na idadi kubwa ya watu wa New Zealand, waliobaki katika karantini, wameonyesha kujitoa kwao kulinda afya ya mwili wa wote, wanabainisha" wanathibitisha.

Maaskofu vile vile wanaendelea kubainisha kuwa  “Lakini sasa wakati umefika wa kuzingatia afya ya kijamii kwa wote, kwa kufikiria kwanza kabisa juu ya mafao ya pamoja na mahitaji ya wale walio na shida. Mabadiliko ya mtazamo yanahitaji kwanza kukutana na Kristo, na hasa, iwe katika liturujia na katika nyuso za watu walio katika mazingira magumu zaidi, wakiwapa misaada na kushiriki”, maaskofu wanaonesha njia. Pili, maaskofu wanongeza kusema “tunahitaji kujiuliza jinsi gani ya kutangaza Injili na kuifanya iwepo ili kuweza kusonga mbele  pamoja kuelekea ulimwengu ulio na haki zaidi”.

Mshikamano na wema kwa wote ndiyo kwa hakika maneno muhimu yaliyoonyeshwa na Kanisa la New Zealand kuweza kuishi uzoefu na kufurahi vizuri katika “Wiki ya Haki kijamii.  Maaskofu wanahitimisha kwa kusema: “Tukumbuke kile tulichokiishi na kujifunza kwa pamoja” na kwa maana hiyo  tafakari yao ni juu ya uzoefu huu kwa kuzingatia mafundisho ya jamii, kwa sababu “ndiyo njia hii tu tunaweza kuendelea kuishi kwa upendo na kumtunza jirani yetu na ulimwengu”.

03 September 2020, 12:01