Tafuta

Vatican News
Watu wa asilia nchini Mexico wanatumia dawa za jadi katika kukabiliana na covid-19 Watu wa asilia nchini Mexico wanatumia dawa za jadi katika kukabiliana na covid-19  (@Cimi)

Maskofu nchini Mexico waelezea juu ya watu wa asilia kukabiliana na covid-19!

Kanisa la Amerika ya Kusini ilinajitahidi kuwa karibu na watu Asilia kwa kuwasaidia kianzisha mambo kama vile ya mafunzo,uchumi na kiroho.Katika taarifa ya Baraza la maaskofu msaada wao shukrani kwa utamaduni wao wa kutengeneza madawa za jadi na utamaduni wao umewawezesha watu hawa kuweza kupambana vema na janga hili la virusi.

Na Sr. Agela Rwezaula -Vatican

Nchini Mexico watu wa asilia, wakitumia hekima ya mababu zao, dawa za jadi na kurudi katika njia za kiuchumi kama vile kubadilishana, wanapambana na  Covid-19, kwa mujibu wa maelezo ya taarifa iliyotolewa na Baraza la Maaskofu ya nchi hiyo. Kwa mujibu wa taarifa hiyo inasisitiza kuwa  Janga limesababisha jamii hizi kurudi kwenye mifumo yao ya afya ya kijamuiya yaani kijadi, kwa  kutumua aina fulani ya uchumi wa mababu zao na kujipanga kusonga mbele katika mapambano na covid-19.

Kanisa mahalia hata hivyo limeendelea kufuatilia na kuongozana na watu hawa, huku wakijaribu kuimarisha nguzo sita katika maisha yao yaani: eneo mahalia, kazi ya jumuiya, lugha ya mama, mikutano, mamlaka ya jumuiya na mantiki ya maadhimisho  na kiroho. Katika mantiki ya  shughuli za kichungaji kwa watu wa kiasili na Waafrika wa Mexico, kiukweli, katika eneo hilo, limefanya kazi ya kuhamasisha na kukuzwa kwa vitendo vinavyolenga kutetea na kulinda wilaya za jamuiya zinazotishiwa na kuhamasisha  kampeni za uhamasishaji wa utunzaji wa dunia mama. 

Kuhusu kazi ya jamuiya, imeshirikiana kuhamasisha kilimo cha bustani za familia na jamuiya na kuhamasisha kubadilishana biashara, ambayo jamuiya nyingine zimeanza hata kuona kama aina ya uchumi mbadala na unaosaidia na kusaidia mifumo ya afya na lishe ya jamuiya zenyewe. Kadhalika waliandaa timu ya watafsiri ili kupeleka habari muhimu katika lugha ya jamuiya  hiyo na kujaribu kudumisha umoja na mawasiliano kuhusu maamuzi kadhaa ya kichungaji, katika muktadha wa janga la covid-19, shukrani kwa mikutano iliyofanyika.

Hatimaye Kanisa limeandaa mikutano kwa njia ya video kuwajuza watu juu ya haki zao za kiafya na za kazi na kujitunza katika katika muktadha wa maadhimisho na kiroho, walihamasisha siku kwa ajili ya za sala, ambayo wanaifanya kila tarehe 12 ya kila mwezi, kumwaomba  Bikira wa Guadalupe aombe kutisitishwa kwa janga hilo. . Hata kwa upande wa waafrika waMexico, walioathiriwa na shida ya kiafya na kiuchumi , na wametumia dawa ya kienyeji kujitibu majumbani mwao na wamefaulu, shukrani pia kwa kuambatana na msaada wa mipango ya kichungaji.

16 September 2020, 12:48