Marekani:Maaskofu wasema makazi ni haki ya wote na yasiyokiukwa

Kwa mujibu wa barua ilyotiwa Saini na marais watatu wa Tume za Maaskofu wa Amerika Usccb) za Haki za Ndani,Uhuru wa Kidini na Uhamasishaji na utetezi wa ndoa wamesema dharura ya Makazi ni haki ya wote na isiyoweza kukiukwa kwa wote,kwa njia hiyo lazima ihakikishwe zaidi ya yote kwa watu walio katika mazingira magumu zaidi.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican

Baraza la Maaskofu wa Amerika (Usccb), katika barua iliyotiwa saini na Askofu Paul S. Coakley, Thomas G. Wenski na David A. Konderla, wote watatu wakiwa ni marais wa Tume za Maaskofu za Haki za Ndani, Uhuru wa Kidini na Uhamasishaji na utetezi wa Ndoa wamesema:“Makazi ni haki ya wote na isiyoweza kukiukwa kwa wote. Ni lazima ihakikishwe zaidi ya yote kwa watu walio katika mazingira magumu zaidi wanasisitiza.

Kama Wakatoliki tunajitahidi kukidhi mahitaji ya wale wote wanaokuja na kubisha milango yetu, katika kumfuata Yesu ambaye anasema: “Nilikuwa mgeni na mlinikaribisha”.  Uthibitisho huu unafika wakati nchini humo, limetolewa pendekezo la kurekebisha sheria zilizopitishwa na Idara ya Nyumba na Maendeleo ya Mjini (HUD). Kunako mwaka 2016, kiukweli HUD ilikuwa inaomba kwamba nyumba na makazi ya dharura yanapaswa kudhibitiwa kulingana na utambulisho wa jinsia wa mtu huyo.

Hii katika maelezo ya maaskofu haikuwa imepingwa katika sheria yoyote ya Bunge na ilileta shida kwa faragha na usalama wa watumiaji, kwa mfano mama wasiyo na waume. Pendekezo la sasa kinyume chake linaanzisha kama aina fulani ya kubadilika, kwani inaacha nafasi kwa majimbo binafsi juu ya jinsi ya kuweza kukaribisha, kufafanua, kuonyesha au kupunguza utambulisho wa jinsia. Marekebisho yaliyopendekezwa, ingawa siyo kamili na hayajibu masuali yote juu ya dharura ya makazi, hata hivyo inawakilisha, kwa mujibu wa  Baraza la Maaskofu wa Marekani ( USCBB), hatua sahihi kuelekea kuboresha mabadiliko na  kuheshimu haki ya\ watu wote  kwa ajili ya malazi ya dharura.

Sehemu za makazi ya mtu binafsi,  maaskofu wanaongeza hufanya kazi kulingana na hali tofauti, miundo na rasilimali tofauti  na inaweza kuwa na mpango maalum kwa watu walio katika mazingira magumu. Kanuni ya kawaida kwa wote, kwa maana hiyo inaweza kuwa haifai kila wakati. Kinyume chake, ni muhimu kuhakikisha mabadiliko ili miundo hiyo ya dharura iwe na  uwezekano wa kuwa ya faida ya wote, kila wakati na kubaki waaminifu kwa utume

15 September 2020, 14:08