Tafuta

Vatican News
na Askofu Mkuu Charles Scicluna, rais wa Baraza la  Maaskofu wa Malta na Askofu Mkuu Charles Scicluna, rais wa Baraza la Maaskofu wa Malta  (ANSA)

Malta:Maaskofu-sheria ya kukomesha ubaguzi inahatarisha uhuru wa mawazo na dhamiri

Hakuna mtu anayepaswa kubaguliwa kwa kabila lake,utaifa,mwelekeo wa kijinsia,ulemavu,dini,umri,itikadi yakisiasa au tabia nyingine yoyote inayomfanya kila mtu kuwa wa kipekee.Ni kwa mujibu wa Tamko la Maaskofu wa Malta kuhusiana pendekezo la sheria za kutokomesa ubaguzi zilinahatarisha kusonga uhuru wa mawazo na dhamiri.

Na Sr. Angla Rwezaula- Vatican

Maaskofu wa Malta wamemua kuwa na  msimamo juu ya miswada miwili mpya unyojikita katika usawa unaozingatiwa kwa sasa na Bunge la Valletta. Katika tamko lao lililosainiwa na Askofu Mkuu Charles Scicluna, rais wa Baraza la  Maaskofu wa Malta, Askofu Anton Teuma, wa Jimbo la  Gozo na Askofu Msaidizi Joseph Galea-Curmwa wa Malta ,wanasisitiza kwamba Kanisa linaunga mkono wa Ndiyo za juhudi zote za usawa na kutokomeza aina zote za ubaguzi. “Ndiyo kwa hatua zote dhidi ya aina zote za ubaguzi, lakini siyo kwa uharibifu wa haki nyingine za msingi na uhuru”.

Hakuna mtu anayepaswa kubaguliwa kwa kabila lake, utaifa, mwelekeo wa kijinsia, ulemavu, dini, umri, itikadi ya kisiasa au tabia nyingine yoyote inayomfanya kila mtu kuwa wa kipekee, wanasema Maaskofu. Wakati huo huo, Kanisa la Malta linaelezea wasiwasi wao juu ya maoni kadhaa ya mapendekezo yanayojadiliwa ambayo yana athari kubwa kwa uhuru wa mtu, hasa uhuru wa mawazo, dhamiri na dini, ambazo zimewekwa katika Katiba ya Malta, lakini pia na Mkataba wa Ulaya na Mkataba wa Kadi ya Ulaya kuhusu  Haki Msingi za binadamu.

Katika tamko lao kwenye  barua hiyo inaomba uhuru wa wazazi ulindwe kwanza kuchagua elimu wanayotaka watoto wao kulingana na imani yao ya kidini na falsafa. Kwa maana hii, ikiwa wanachagua shule ya dini au inayofuata kanuni fulani za maadili,basi lazima ihakikishwe kuwa viongozi wake ni watu wanaolinda na kukuza kanuni hizi. Kwa maana hii, shule za dini lazima ziwe huru kuchagua wafanyakazi wao wa kufundisha ili kufundisha masomo mbalimbali kulingana na maadili na thamani wanayoikiri. “Mtu ambaye hajali au hata ana chuki na maadili ya shule hawezi kutekeleza jukumu hili”, wamesisitiza Maaskofu hao.

Kwa mujibu wamaaskofu wa Malta, wanadai kuwa sheria mpya ya usawa lazima ihakikishe uhuru wa dhamiri ili kwamba hakuna mtu anayelazimishwa kuhamasisha au kushiriki katika shughuli zilizo kinyume na dhamiri, kanuni na maadili yao. Kwa kuongezea, wanasema  hakuna chombo kinachopaswa kuundwa sawa na mahakama ambacho, kwa jina la kuhamasisha  usawa, kinakandamiza haki za wengine. Kuheshimu hoja hizi za kudumu, inaweza kusaidia kuimarisha mapendekezo ya sheria ya usawa na dhidi ya ubaguzi wote, kwa sababu wanakubali utofauti na siyo usawa. “Usawa wa kweli unaheshimu kila mtu, unaruhusu na unathamini tofauti na haziiondoi ”, maaskofu wa Malta wamehitimisha  tamko lao.

17 September 2020, 17:13