Tafuta

2019.01.29 Aborto, feto, embrione, vita, interruzione gravidanza 2019.01.29 Aborto, feto, embrione, vita, interruzione gravidanza 

Malawi:Mwenyezi Mungu aliumba ubinadamu kwa kusudi!

Viongozi wa dini Nchini Malawi wameungana pamoja katika kutetea utakatifu wa maisha na kupinga sheria ya utoaji wa mimba.Viongozi hao wanahimiza Raia wa Malawi kutetea maisha tangu mimba na kulinda watoto,pamoja na wale ambao hawajazaliwa,kama ilivyowekwa na Katiba.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Baraza la Maaskofu nchini Malawi na vyombo vingine vya dini likiwemo Baraza la Ushauri la Makanisa Malawi (MCC), Mashirika ya Uinjilishaji (EAM), Vyama vya Kislamu vya Malawi wameeleza wasiwasi wao mkubwa kwa Kamati ya Bunge la Malawi juu ya hali ya  kiafya na mabadiliko ya sheria mpya juu ya utoaji mimba. Haya yamesemwa na Shirika la Habari za kimisionari(Fides) huku wakisisitiza kuwa, kitengo cha kidini kinachosimamia mikakati ya kisheria nchini Malawi kimetoa mapendekezo kadhaa juu ya sheria mpya ya utoaji mimba inayopingana na sheria ya Mungu na kukinzana na utakatifu wa maisha.  

Tamko lililotolewa na Baraza la Maaskofu nchini Malawi na viongozi wengine wa dini limepinga vikali sheria inayo halalisha vitendo vya utoaji mimba huku likisimamia kuwa hakuna Taasisi ikiwemo Bunge na Mahakama zilizo na mamlaka ya kukatisha maisha ya mtu dhidi ya utashi wa Mungu. Hii inatokana na ukweli kwamba maisha ya mtu yana msingi wake katika uumbaji (Mwa 1:27). Imani ya kislamu pia inaamini kabisa kuwa Mwenye Mungu (Allah) amewaumba wanadamu akiwa na malengo yake.

Kwa kunukuu kitabu cha Nabii Jeremia 1-5, makundi haya ya wananchi yanayatazama maisha na kuona utakatifu wake unaohitaji kulindwa tangu kutungwa kwa mimba hadi kufikia kifo kilicho kusudiwa na Mungu. Hivyo kuna haja ya kulinda maisha na hadhi ya watoto wachanga ili nao waweze kufikia wito wanaoitiwa na Mwenyezi Mungu. Viongozi wa dini wameweza kufungua uelewa katika jamii ya Malawi huku wakiwaomba wabunge kutopitisha mswaada wa sheria inayoruhusu sheria ya utoaji mimba ambayo inatafrisiriwa kama mauaji halaiki ya watoto ambao hawajazaliwa. Hii imejitokeza kwa mara ya pili, mswaada wa marekebisho ya sheria ya utoaji mimba kurudishwa tena bungeni huku ikishabikiwa na Shirika la kijamii (OSC) ambalo linadai akina mama wapewe mamlaka ya kutoa maamuzi ya kutoa mimba au la, ili kuokoa vifo vya akina mama wengi wanaokufa kutokana na utoaji mimba usio halali na hatarishi.

Pamoja na hayo, viongozi wa dini wamepinga vikali madai hayo yanayopendekezwa kuwekwa kisheria kwa ngazi ya kitaifa kwa kifungu kilichotolewa mnako tarehe 6 Disemba, 2016 dhidi ya maisha na familia. Sheria ya utoaji mimba nchini Malawi tangu awali imekuwa ikizuia harakati za utoaji mimba kwa akina mama na mabinti na kudhibiti makusudio ya aina yoyote ya kutoa mimba ili kulinda utakatifu wa maisha Kulingana na waendelezaji wake,wanataka sheria kuwapo wanabanisha kuwa itasaidia kupunguza vifo vya akina mama.

Rais Chakwera pia ameeleza akisisitiza kuwa marekebisho hayo yatasaidia Malawi kufikia moja ya Malengo ya Maendeleo Endelevu yaliyowekwa na Umoja wa UN kufikia 2030. Hivi sasa 18% ya vifo vinavyohusiana na ujauzito nchini Malawi vimehusishwa na utoaji mimba wa siri. Lakini hizi ni hoja zote zilizokataliwa na viongozi wa dini wa nchi hiyo ambao wanasisitiza kuwa utoaji mimba ni dhambi na ni uasherati kwa sababu ni kinyume na Amri ya Mungu kwa kuzingatia maisha kuwa matakatifu. Imani ya Kiislam, kwa upande mwingine, inaamini kwamba Mwenyezi Mungu aliumba ubinadamu kwa kusudi.Katika taarifa iliyonukuliwa na tovuti ya Baraza la Maaskofu wa Afrika Mashariki(Amecea),viongozi wa kidini wanahimiza Raia wa Malawi kutetea maisha tangu  mimba na kulinda watoto, pamoja na wale ambao hawajazaliwa, kama ilivyowekwa na Katiba. Mwaliko ni kushinikiza wawakilishi wao katika Bunge wasiidhinishe muswada huo ambao, wanasema, utasababisha kama mauaji ya kimbari ya watoto.

23 September 2020, 17:06