2015.09.20 Papa Francisko kukutana na vijana wa Cuba katika ziara yake ya kitume 2015. 2015.09.20 Papa Francisko kukutana na vijana wa Cuba katika ziara yake ya kitume 2015.  

Kumbukizi la miaka 5 ya Papa kutembelea Cuba

Baada ya miaka 5 tangu ziara ya Papa Francisko katika kisiwa cha Cuba kunako Septemba 2015 maaskofu wa nchi hiyo wamemtumia barua ya shukrani,ukaribu na upendo wa Papa kwa Kanisa la Cuba na watu wake.Barua hiyo inaonesha pia matarajio ya Wosia wa kitume wa"Fratelli tutti",utakaotiwa sahini tarehe 3 Oktoba 2020 huko Assisi,Italia.

Na Angela Rwezaula-Vatican

Uzoefu ni mwingi ambao ambao leo hii unaonesha na kushuhudiwa kufanya kumbukizi na upendo mwingi kwa namna ya pekee katika mafundisho ambayo yanasaidia kuimarisha na kukuza matendo ya kichungaji leo hii. Ni maelezo kutoka katika Barua ya Baraza la Maaskofu katoliki nchini Cuba (COCC) kwa kuelekeza kwa Papa Francisko katika fursa ya miaka mitano tangu alipofanya ziara ya kitume katika kisiwa hicho kikubwa kuanzia tarehe 19 hadi 22 Septemba 2015.

Katika barua yao waliyotangaza tarehe 18 Septemba, maaskofu wanasisitiza juu ya ziara yake ilivyokuwa sambamba na mwaka wa Jubilei ya Huruma aliyokuwa ametangaza Yeye mwenyewe na wanathibitisha juu ya huruma aliyoisha nchini mwao wakati wa ziara yake bado inaendelea kuigwa na kuwa mfano nchini humo. Ziara hiyo wanasisitiza iliacha msukumo ambao unaashiria utume wao umuhimu wa kudumu wa kiinjili.

Baraza la Maaskofu katoliki Cuba (COCC) wanazingatia pia msukumo walioupata maaskofu, makuhani na mawakala wa kichungaji kuwa Kanisa katika harakati za mwendo, iliyoongozwa na mahubiri yake katika Kanisa la Madhabauhu ya Mama wa Upendo huko Cobre. Kwa namna ya pekee barua hiyo kadhalika inasisitiza kuwa mkutano wa Papa Francisko na wenzi wa ndoa katika Kanisa kuu la Santiago ya Cuba umetoa uzoefu usiosahaulika na wa kusisimua ambao, ukifuatana na njia na vigezo muafaka vya Baba Mtakatifu, na unaendelea kusaidia  safari ya wanafamilia za Cuba.

22 September 2020, 15:54