Tafuta

Vatican News
Maisha ni matakatifu lazima yalindwe tangu kutungwa kwa mimba hadi kufikia mwisho wa maisha yake duniani. Maisha ni matakatifu lazima yalindwe tangu kutungwa kwa mimba hadi kufikia mwisho wa maisha yake duniani.  

Kenya:Maaskofu waomba serikali kufunga vituo vya afya vinavyohusika na utoaji mimba!

Baraza la Maaskofu nchini Kenya(Kccb)wameomba wahusika wa serikali nchini humo kufunga kliniki zote na vituo vya afya ambavyo vinajihusisha na utoaji mimba kwa hiari na ambavyo ugawa vizuia mimba kwa wasichana balubalu na vijana.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa katika tovuti ya Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Afrika Mashariki, zinabainisha kuwa Baraza la Maaskofu nchini Kenya (Kccb)wameomba wahusika wakuu wa serikali ya Nchi kufunga kliniki zote na vituo vya afya ambavyo vinavyojihusha na utoaji mimba kwa hiari na ambavyo pia utoa vizuizi mimba kwa wasichana balubalu na vijana.

Maaskofu wanafafanua kuwa kukatizwa kwa hiari ujauzito ni uovu na kuelezea juu ya wasiwasi wao kuhusu muswada unaohusu afya ya uzazi ambao nia yao msingi, hata kama imejificha ndani mwake, wanasema ni kuanzisha utoaji wa mimba nchini humo kwa anayeoomba. “Hatuwezi kutarajia Mungu kuwa pamoja nasi ikiwa sisi tunaruhusu uovu wa wengine kutunga sheria za kuua watoto wetu kabla hata hawajazaliwa.” Maaskofu pia wanabainisha jinsi gani idhini ya utoaji mimba inavyokwenda kinyume na kanuni zilizowekwa na Katiba ya Taifa. “Nchi, kiukweli inaamini utakatifu wa maisha na utu wa binadamu na kwa maana hiyo inatia wasiwasi sana kwamba viumbe vingine vinaruhusiwa kueneza itikadi ambazo zinashusha hadhi hiyo hiyo kwa jina la uhuru wa kuchagua”.

Wakigeukia wazazi, maaskofu hawa wanawashauri wazazi wakumbuke jukumu lao msingi, hasa lile la kuuonyesha na kufundisha kanuni nzuri za maadili kwa watoto wao, wakiwapa watoto wao muda wa kutosha. Katika taarifa yao, Maaskofu pia wanafafanua: “Uzazi ni uwekezaji mkubwa zaidi ambao mzazi anaweza kufanya na inahitaji ustadi, juhudi, kujitoa na uvumilivu”. Kwa njia hiyo ni jukumu la maadili ya familia, kuchukua jukumu kamili la kuelimisha watoto wao katika maadili mema hasa kuhusu elimu ya ngono. Hatimaye, viongozi hawa wa Kanisa katoliki la Kenya, wanalaani kitendo cha kufanya fujo dhidi ya familia na itikadi ya kijinsia iliyoenezwa nchini humo na mashirika fulani na ambayo ni kinyume na mafundisho ya Injili.

05 September 2020, 16:58