Tafuta

"Linahitajika ua" ni jina la kitabu kilicho andikwa kutokana uharibifu hadi kufikia utunzaji wa mazingira kwa mujibu wa Caritas Italiana  "Linahitajika ua" ni jina la kitabu kilicho andikwa kutokana uharibifu hadi kufikia utunzaji wa mazingira kwa mujibu wa Caritas Italiana  

Kazi ya uumbaji:Caritas yazindua kitabu kipya cha historia na ushuhuda!

Mwaka huu 2020 kilele cha Siku ya Maombi kwa ajli ya kazi ya uumbaji na kipindi cha kazi ya uumbaji ambacho kitaendelea hadi tarehe 4 Oktoba kwa kuunganishwa na makanisa yote ya kikristo kimejikita katika fursa ya kusheherekea Jibilei ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa siku ya mama Dunia.Caritas nchini Italia katika fursa ya imeandaa kitabu kiitwacho “linahitajika ua:kutokana na uharibifu hadi kufikia utunzaji wa mazingira.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Mwaka huu 2020 kilele cha Siku ya Maombi kazi ya uumbaji na kipindi cha kazi ya uumbaji ambacho kitaendelea hadi tarehe 4 Oktoba kwa kuunganisha na makanisa yote ya kikristo kimejikita katika fursa ya kusheherekea Jibilei ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa siku ya mama Dunia. Kwa ngazi ya kitaifa, nchini Italia, tarehe Mosi Septemba ilikuwa inaadhimisha hata mwaka wa 15 tangu kuanza kwa shughuli ya utunzaji wa mazingira kwa kuongozwa na mada “kuishi kipindi hiki kwa shauku, katika haki na huruma (Tt 2,12). Kwa ajili ya mitindo mipya ya maisha”.

Nchini Italia, mwaka huu maadhimisho ya Jubilei hii yatafanyika katika jimbo la Ferrara-Comacchio siku ya tarehe 6 Setemba 2020. Kwa ajili ya fursa hiyo, baadhi ya shuhuda zimekusanywa katika kitabu kimoja kiitwacho “linahitajika ua: kutokana na uharibifu hadi kufikia utunzaji wa mazingira”. Kitabu hiki ni kati ya mfululizo wa  vitabu vya, kama vile “VivaVoce” yaani sauti hai kilichochapishwa na Edb, kwa kuandikwa na Paolo Beccegato na Renato Marinaro wa Caritas ya Italia, ni kitabu ambacho kitatolewa hivi karibuni. Kitabu hiki kinafuata vitabu vingine 5 ambavyo vikwisha chapishwa na kutangazwa  na waandishi hao: “Ragazzi panchina” yaani Vijana kwenye benchi. Kinahusu historia ya vijana ambao hawasomi na wala kufanya kazi(Edb 2017), “kutengeneza maisha. Historia zaidi ya gereza (Edb 2018); “Kuwa wapole”. Historia ya wahamiaji zaidi ya mahali pa upamoja na fake news” (Edb 2018), “Mfuko wa kujaza”. Historia ya umasikini wa kuelimisha vijana na watu wazima (Edb 2019) na “hata  uwe mdogo ulivyo. Wakati nyumba inageuka kuwa matatizo” (Edb 2019).

02 September 2020, 12:36