2019.11.25 Kardinali John Tong Hon 2019.11.25 Kardinali John Tong Hon 

Hong-Kong,Barua ya kichungaji,Kard.Tong:Baki kidete kwa umoja na tumaini!

Ushauri wa Kardinali John Tong Hon,msimamizi wa Kitume wa Hong Kong kwa waamini katoliki nchini humo katika brua yake ya kichungaji anasema wabaki kidete kwa umoja na matumaini katika kipinid kigumu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Mwaliko wa kuwa na tumani na katika mawasiliano na Kanisa ndiyo ufupisho na kiini cha Barua ya kichungaji iliyotangazwa tarehe 21 Septemba na Kardinali John Tong Hon, Msimamizi wa Kitume wa Hong Kong. Kwa mtazamo wa maneno yake  unaonesha kwamba Nchi ambayo kati ya mwaka 2019 na 2020 imeona machafuko ya kijamii na kuishi kwa uzoefu wa janga la Covid-19. Katika ujumbe wake wa kichungaji ulipewa jina “ katika muungano na Kanisa, Kardinali anawatia moyo wakristo wabaki kidete katika imani hasa katika kipindi hiki cha majaribu na matatizo kwa utambuzi kuwa Mungu anabadili mateso kuwa baraka. Kwa namna ya pekee Kardinali Tong anawapa ushauri waamini wake kufuata “ Mafundisho jamii ya Kanisa kwa ajili ya ustawi wa wema wa pamoja na wa jamii huku wakiende mbali na hisia za chuki, kiburi kwa sababu kuwatendea wengine kama adui na kupigana ni kinyume na imani ya kikristo.

Msimamizi wa kitume  Hong Kong vile vile amebainisha juu ya umuhimu wa demokrasia kwa maana ya mchakato unaondelea ambao unahitaji uvumilivu kama anavyoandika Papa Francisko katika Waraka wake wa kitume wa  “Evangelii gaudium”, yaani ‘Injili ya furaha’  kuwa “ kugeuka kuwa watu inahitaji mchakato wa kuendelea bila kukoma (…). Ni kazi inayokwenda taratibu na ambayo inahitaji utashi fungamani na kujifunza kufanya hivyo hadi kuongeza utamaduni wa makutano na maelewano kati ya wengine” (220). Kardinali katika barua yake anaadika: “Katika kuchangia kwenye katiba ya jamii, amani, haki na udugu, vina nafasi mbili za kujikita nazo kama vile ‘unabii’ na ‘watumishi’ . Ni lazima kufanya mang’amuzi ya ishara za nyakati na lazima kutenda kama chumvi ya dunia na mwanga wa ulimwengu , na chachu ya ubinadamu kijamii. Tunatakia kujikita katika matendo kwa kile ambacho Yesu anafundisha katika Heri”.

Mafundisho jamii ya Kanisa kwa hakika “hayajawahi kuonesha kuwa chuki na kutumia nguvu ni kama njia za kupata amani” na “ Kristo msalulibiwa ni mfano kwa watu wote wakristo. Kila aina yoyote ya migogoro ya kusuluhisha, upendo, msamaha na mapatano lazima daima vipewe kipaumbele ikiwa tunataka kufikia haki na amani kwa sababu hatima hajawahi kuwa sababu kufaa. Kwa upande wa makuhani, Kardinali anawahimiza waangazie waamini na mafundisho jamii ya Kanisa ili waweze kuunda dhamiri zao, na kuwahimiza kushiriki kwa bidii katika maisha ya Kanisa na ya jamii, kulingana na kile kilichoidhinishwa na Mtaguso Pili la Vaticani. Wakati huo huo, Wakatoliki wenyewe wamealikwa sana kubaki katika muungano na wachungaji wao, na hivyo kuhifadhi umoja wa kikanisa.

Akiwaelekea wale wanaotazamia siku za usoni katika hali ya kutisha kwa sababu walitegemea maoni yao juu ya kutokuwa na uhakika wa kisiasa na athari mbaya ambayo janga la Covid-19 limekuwa nayo katika uchumi na njia za kupata mafao ya kitaifa, Kardinali Tong katika waraka wake anamwalika kila mtu kwa dhati kuweka tumaini kwa Kristo, Bwana wa historia ya wanadamu, kwa sababu hii ni tumaini lisilotikisika . Uthabiti  huo huo diyo matarajio yake hata kwa Wakatoliki wote ambao wameona Imani yao ikiyumba kwa sababu ya hali ya sasa nchini, na  kwa wote, Kardinali anaomba msaada ili waweze kuona moto wa  imani unafufuliwa kwa Mungu

Kwa upande mwingine, anahitimisha Msimamizi wa Kitume wa Hong Kong, kuwa "wakati huu, ingawa unaonekana kuwa wa kufadhaisha na mgumu unaweza kuwa baraka kwetu kwa sababu unaweza kutufanya tujue zaidi ukweli kwamba Mungu ndiye ufunguo wa hatima yetu, binadamu, tunaohitaji mshikamano zaidi kati ya wajumbe wote wa familia ya wanadamu na kwamba ni muhimu kudumisha umoja wa Kanisa, hata katika utofauti. Machafuko ya kijamii ya 2019 na janga la 2020, anahitimisha Kardinali kwamba yamekuwa na athari kubwa kwa Hong Kong na kwa maana hiyo wanaweza kutarajia changamoto mpya ya utume wao wa kuinjilisha, na ambao ni kukabiliwa kwa nia moja na moyo mmoja.

28 September 2020, 16:35