Tafuta

Vatican News
Tutunze mazingira nyumba yetu ya pamoja Tutunze mazingira nyumba yetu ya pamoja  

Celam,Kazi ya Uumbaji:tusali kwa ajili ya uongofu binafsi na kijamii!

Katika ujumbe uliotangazwa kwenye Siku ya kuombea kazi ya uumbaji ulimwenguni kwa mujibu wa shirikisho la mabaraza ya Maaskofu Amerika Kusini(Celam)wanathibitisha jitihada za sala na matendo hai ya utunzaji wa nyumba yetu ya pamoja.Wanawaalika watu wote kusoma Waraka wa Ladato si uliotangazwa miaka 5 iliyopita ili kupata ndani mwake nguvu,matumaini na mwamko wa kufuata utume huo.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Rais wa shirikisho la Mabaraza  ya Maaskofu barani Amerika ya kusini (Celam) Askofu Mkuu Miguel Cabrejos Vidarte, wa Jimbo Kuu Katoliki la  Trujillo nchini Perù katika ujumbe wake uliotangazwa siku ya kuombea kazi ya uumbaji tarehe, Mosi Septemba 2020 unasema “Kwa kuungana na nia za Papa Francisko, Shirikisho la Baraza la Maaskofu wa Amerika ya Kusini tunathibitisha jitihada zetu kwa ajili ya utunzaji bora wa  Kazi ya Uumbaji kwa njia ya sala, pia kuhamasisha mipango mingine ambayo tayari ipo katika bara letu, ili kuhamasisha utunzaji wa kweli wa nyumba yetu ya pamoja .

Katika ujumbe huo uliotiwa sahini hata na Katibu Mkuu Askofu Juan Carlos Cárdenas Toro, askofu msaidizi wa Cali nchini Colombia unasema: “kwa kuchukua fursa ya siku hii, tunashauri kujikita kwa njia ya ishara za dhati ili kufanya kazi pamoja kwa matazamio ya wema wa kazi ya uumbaji na miongoni mwake ni maombi ambayo ni jambo msingi kwa ajili ya kutunza nyumba yetu ya pamoja”.

Ujumbe huo pia unakumbusha tangu kutangazwa kwa waraka wa Laudato Si miaka 5 iliyopita na kuwaalika watu wote wausome wosia huo ili kupata ndani mwake nguvu, matumaini na shauku ya kuendelea kufuatia utume huo. Kwa kufuata ushauri huo Askofu Mkuu wa Peru anakumbusha jinsi gani Papa Francisko amessitiza kuwa Siku hii inayoadhimishwa kila mwaka “inatoa fursa kwa waamini wote na jumuiya zote , kupata muafaka wa kupyaisha kwa dhati juhudi zaidi katika wito wa kutunza kazi ya Muumbji na  huku wakiinua shukrani zao kwa  Mungu kwa maajabu yake ya kazi ambayo ilikabidhiwa kwetu sisi kuweza kuitunza”.

Ujumbe wa Celam kwa mujibu wa Askofu Mkuu Cabrejos unahitimishwa kwa kwa kusema “ tunao utambuzi kuwa mienendo yetu mingi inachangia kuongezeka kwa matatizo. Badala yake kushirikiana katika kutafuta suluhisho la mgogoro wa mazingira ndiyo suala msingi. Kwa maana hiyo tunao uwajibikaji wa kusali, kujiuliza na kutiana moyo kwa nguvu za kiroho, ambazo nguvu  pekee ni Bwana kwa sababu anaweza kufanya uwezekano wa uongofu wetu binafsi na ule wa kijamii kwa kile kiitwacho mantiki ya kiekolojia.

01 September 2020, 16:14