Tafuta

Vatican News
2020.08.10 Toleo la 26 la kilio cha waliotengwa nchini Brazil. 2020.08.10 Toleo la 26 la kilio cha waliotengwa nchini Brazil. 

Brazil:Kilio cha waliotengwa-Inatosha mateso,chuki na ukandamizaji!

Katika Toleo la 26 lililoanzishwa mwaka 1995 na Maaskofu,maandamano tofauti katika Nchi yanaendelea,lakini kwa sababu ya janga la corona,majukwaa ya kidigitali yanasaidia.Tarehe 7 ya kila mwaka ni siku ya Uhuru nchini Brazil.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Inatosha mateso, chuki na ukandamizaji. Tunataka kazi, ardhi, nyumba na kuweza kujumuishwa. Hii ndiyo kauli mbiu ya toleo la 26 ya “Kilio cha waliotengwa”, inayoendelea leo hii nchini Brazil, ambayo mwaka huu imelazimika kukumbana na vizuizi vinavyo sababishwa na janga la covid-19. Lakini maandamano hayo bado yanaendelea kufanyika shukrani kwa msaada wa majukwaa ya digitali. Kuna mambo mawili mapya la kwanza ni “Siku ya Kilio ambayo itaendelea kufanyika kila tarehe 7 ya kila mwezi kwa maana ya zaidi ya tarehe ya kisheria iliyowekwa  kila tarehe 7 Septemba, siku ambayo wanasheherekea  hata uhuru nchini Brazil; pili  tukio linaloendelea kwenye mitandao ya kijamii kwa ajili ya kuzuia mikusanyiko.

Kitambaa cheusi katika milango na madirisha

Tam tam imeanza nchi nzima kupitia katika mitandao. Mambo mengi yameanzishwa ambayo walipendekeza. Wameanzia kuweka kitambaa cheusi katika milango na madirisha yao ili kuonesha umoja wa maandamano ya kupinga. Japokuwa mambo hayo hayatokei moja kwa moja katika barabara lakini katika mazingira yaliyochaguliwa, kwa kuheshimi kanuni za ulinzi na usalama wa kiafya, kwa mujibu wa Mratibu wa “Kilio cha waliotengwa na Wanahija ya wafanyakazi Bi. Rosilene Wansetto.

Misa katika madhabahu ya Aparecida

Madhabahu ya Kitaifa ya Aparecida ndiyo inakuwa mgeni wa tukio hili na kutangazwa moja kwa moja na Televishini mahalia na mitandao mingine katoliki ya habari. Askofu Mkuu Orlando Brandes amebainisha juu ya  kusali kwa ajili ya kuheshimu hadhi ya binadamu. Kwa mujibu wa Askofu Mkuu huyo amesema “watu ambao wanafanya kazi ndiyo wanazalisha utajiri. Kwa maana hiyo ni msingi kwamba wote wakajenga dunia iliyo ya haki na yenye uwezo wa kuhakikisha ubora wa maisha kwa wote”. 

Kukusanya saini dhidi ya kupunguzwa kwa gharama za huduma ya afya

Mashirika ya kijamii, asasi za kiraia, mashirika kutoka asili tofauti, wanaharakati na hata wabunge watajiunga na Kampeni ya  “Kilio waliotenggwa" kupitia mitandao ya kijamii ili kusaidia kampeni hiyo. Pia tarehe 7 Septemba inawezekana kuanza kujiunga na mkusanyiko wa saini ya kuweza kupinga kwa kupunguzwa kwa rasilimali zitakazotengwa kwa ajili ya afya ya umma. Baraza la Kitaifa la Afya (CNS), likiwa na wasiwasi juu ya hali ambayo Mfumo wa Afya Moja (SUS) unajikuta nao  kutokana na janga la virusi vya Corona, imezindua ombi dhidi ya kupunguzwa kwa rasilimali zitakazotengwa kwa afya. Wazo ni kufikia mshikamano wa  laki moja ili  kuwasilishwa katika  Bunge la Kitaifa, tarehe 9 Septemba 2020.

Tukio la "Kilio cha Waliotengwa" lilizinduliwa  kwa mara ya kwanza kunako mwaka 1995, kama sehemu ya “Kampeni ya Udugu”. Na kunako mwaka 1996, katika toleo lake la pili, ilijumuishwa katika programu ya kichungaji za Baraza la Maaskofu nchini Brazil (CNBB) kwa ngazi ya  kitaifa.

07 September 2020, 14:35