Tafuta

Vatican News
2019.09.05 Ziara ya Papa Francisko nchini Msumbiji, Madagascar na Mauritius 2019.09.05 Ziara ya Papa Francisko nchini Msumbiji, Madagascar na Mauritius 

Afrika Kusini na mshikamano na Msumbiji:mateso yenu ni uchungu kwa wote!

Katika kushirikishana mshikamano,maaskofu wa Afrika Kusini wanawashuri Kanisa Katoliki nchini Msumbiji kubaki kidete katika jitihada za kupeleka mbele utume mgumu katika hali halisi inayo wazunguka na matumaini kwa Mfalme wa Amani.Ni katika Ujumbe wao kuonesha ukaribu,kutokana na kipindi kirefu cha migogoro kadhaa ambayo yamesababisha wathirika wengi na maelfu kulundikana katika mkoa wa Cabo Delgrado.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Baraza la Maaskofu katoliki wa Afrika Kusini (Sacbc) katika taarifa yao kwa maaskofu na waamini nchini Msumbiji wanaelezea mshikamano wao na ukaribu, kutokana na kipindi kirefu ambacho wamekumbwa na migogoro kadhaa  na mapigano ambayo yamesababisha idadi ya wathirika wengi na maelfu ya wazalendo kulundikana kwa namna ya pekee katika mkoa wa Cabo Delgado. Katika taarifa hiyo wanasema, “vurugu, mateso na vifo vinavyosababishwa na migogoro ya kisilaha inayoendelea ni uchungu wetu sote”.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotiwa sahini na Askofu  Sithembele Sipuka, ambaye ni Rais wa Baraza la Maaskofu Afrika Kusini (Sacbc), wanasisitizia utume wa Kanisa kuwa ndiyo  mkondo wa amani ya Mungu na siyo kupunguza juhudi zozote katika kuhimiza na kusaidia michakato ya kukuza utamaduni wa upatanisho. Kadhalika kufanya kazi kwa ajili ya amani wanakumbusha “ni jukumu ambalo tunasubiliwa sisi sote na kama Baraza la Maaskofu wa Afrika Kusini (Sacbc) tutajitahidi kushirikiana na nyinyi katika kufanya haki, amani na upatanisho vinakuwa hali halisi katika nchi yenu”. Kwa mujibu wa Maaskofu wa Afrika Kusini pia ni matarajio yao kwamba inawezekana kutimiza hivi karibuni ziara yao ya mshikamano nchini Msumbiji.

Katika taarifa ya inakumbusha pia roho ya udugu na mshikamano ulioonesha na Papa Francisko kwa watu wa Cabo Delgado,  iwe katika Ujumbe wa “Urbi et Orbi”,  tarehe 12 Aprili mwaka huu wakati wa Dominika ya Pasaka na kwa njia ya simu aliyopiga tarehe 19 Agosti kwa Askofu wa Jimbo la Pemba, Askofu Fernando Lisboa. Kwa kushirikishana mshikamano huu, maaskofu wa Afrika Kusini kwa maana hiyo wanawashuri Kanisa katoliki nchini Msumbiji kubaki kidete katika jitihada za kupeleka mbele utume  huu mgumu katika  hali halisi inayowazunguka na matumaini kwa Mfalme wa Amani.

09 September 2020, 17:36