Tafuta

Vatican News
Watoto wanahitaji kupata haki na ulinzi wao Watoto wanahitaji kupata haki na ulinzi wao  (AFP or licensors)

Afrika Kusini:Haki na amani vilinde na kutetea janga la watoto wanaotunza familia!

Ripoti ya haki na amani ya Baraza la Maaskofu nchini Afrika Kusini inabaini hatari kubwa ya watoto wanaotunza familia.Kwa mujibu wa Ripoti iliyotolewa tarehe 28 Agosti 2020 inabainisha kwamba hawa ni watoto wanaoteseka sana kutokana na kwamba ni yatima wanaachwa peke yao,wanakata tamaa kihisia,wanabaguliwa,wanatelekezwa,na kuachwa na upweke kijamii.

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican.

Ripoti yenye kurasa 18 ya Tume ya Haki na Amani(JPC) ya Baraza la Maaskofu nchini Afrika Kusini inaonesha ushuhuda wa hali halisi ya matatizo ya watoto wanaolazimika kutunza familia au wamebaki yatima au wameachwa peke yao na wazazi wote wawili au ni watoto waliotelekezwa na baba zao. Kwa mujibu wa Ripoti iliyotolewa tarehe 28 Agosti 2020Hawa ni watoto wanaoteseka sana kutokana na kuachwa peke yao, kukata tamaa kihisia, ubaguzi kutelekezwa, kuachwa na upweke kijamii, 

Katika ripoti hiyo inasimulia ushuhuda wa watoto kwa mfano wanaaandika:“Baba anarudi nyumbani wakati wa sikukuu ya kuzaliwa kwa Bwana tu. Anatununulia chakula cha kutosha kwa wiki mbili tu na baadaye kwa upya anatuacha peke yetu. Na sisi tunakufa kwa njaa kwa kipindi chote cha mwaka”.

Kwa kubaguliwa na jamii ambayo haiwafikirii kama wazalishaji, watoto hawa mara nyingi wako hatarini hata mikononi mwa ndugu zao wenyewe ambao baada ya kifo cha wazazi wao, mara nyingi  wananyang’anywa hata urthi wao. Na zaidi Tume ya Haki na Amani inabainisha jinsi gani watoto wanaotunza familia wanaonesha hata dalili za kujionea huruma na kutojijali, kiasi kwamba wanaamini kuwa hawastahili kuthaminiwa na jamii.

Kwa maana hii Kanisa nchini Afrika Kusini, limependekeza mpango maalum kwa ushirikiano na Serikal na asasi za kiraia  ili kuanza kwa dhati kuwainua kidhamiri na kimaadili, kuwatia chachu ya upya  na maana ya uwajibikaji katika jamii na utashi wa kuwa na  familia iliyo pana ya kutunza  watoto wa ndugu zao waliaga dunia au hawapo kwa sababu mbali mbali.

Kwa mujibu wa ripoti ya haki na amani (Jpc), inasisitza kuwa lazima kuzuia uwepo wa familia zinazoongozwa na watoto, kwa sababu wadogo lazima wakue katika familia ya kawaida. Na wakati huo huo, Maaskofu wa Afrika Kusini wanaomba kuhamasisha na kuongeza nguvu za kulinda watoto dhidi ya unyanyasaji kingoni na ambapo katika kesi hizi ni hatari kubwa iliyobainika. Na hatimaye maaskofu hawa wanatoa wito kwa huduma bora ya uponyaji wa maumivu na majeraha yanatokanayo na kuteseka kwa  watoto ambao wamekuwa yatima au walio katika mazingira magumu zaidi kwa maana ni muhimu sana. 

06 September 2020, 17:00