Tafuta

Vatican News
2019.01.10 Kutoa sadaka 2019.01.10 Kutoa sadaka 

Afrika Kusini:Bajeti ya sadaka ya Kwaresima:waamini wapongezwa kwa ukarimu!

Baraza la Maaskofu nchini Afrika Kusini wamepongeza waamini wao kwa ukarimu mkubwa waliouonesha katika kipindi cha janga la virusi vya corona au covi-19 kwa mchango wao wa sadaka ya kipindi cha kwaresima 2020.

Na Sr. Angea Rwezaula -Vatican

Janga la Covid-19 halijazuia ukarimu wa waamini Wakatoliki wa Afrika Kusini kwa mujibu wa taarifa ya Baraza la Maaskofu wa Afrika Kusini(Sacbc)ambapo unabainisha hayo katika barua ya wazi, ambayo inaonesha bajeti ya makusanyo ya kwaresima 2020 na kutoa shukrani zao kwa wengi ambao wamechangia kwa ukarimu na moyo.

Katika barua hiyo maaskofu wanaandika “huu umekuwa mwaka wenye shughuli nyingi kwetu sote kiukweli kwa zaidi ya siku 150 za kuwa karantini katika ngazi nyingi. Na hiki kilikuwa ni kipindi kigumu sana kwenu ninyi walei ambao umebidi kukubaku na kuzoea hali halisi ilivyokuwa hasa ya matumizi ya teknolojia za digitali pia kushiriki katika Misa Takatifu”. Kwa sababu hii, Baraza la Maskofu Afrika Kusini (Sacbc)linawashukuru waamini wote kwa kujitolea na kujitoa kukaa karibu na Kanisa kwa ukarimu wakati wa janga hilo. Kwa kufafanua zaidi hasa, makusanyo ya sadaka ya Kwaresima ilileta karibu randi milioni 4(sawa na euro elfu 197) ambazo zitakwenda kusaidia maskini na wahitaji zaidi katika siku hizi ngumu. Mipango mingine zaidi itahusu msaada kwa seminari na programu za mafunzo ya makasisi na mashemasi wa kudumu, pia misaada kwa parokia.

Makusanyo ya 2020 wanakumbuka maaskofu yalikuwa ni sawa na asilimia 39 ikilinganishwa na ya awali, lakini maaskofu bado wanasema wana bahati sana kwa msaada walioupokea. Ikumbukwe kwamba Afrika Kusini Covid-19 imesababisha visa 628,000 kwa jumla, na watu 550,000 walipona na vifo vya watu 14,000.

04 September 2020, 12:15