TANZANIA-MINING/TANZANITE TANZANIA-MINING/TANZANITE 

Afrika-Baraza la makanisa Afrika upo uhitaji wa kukomesha ufisadi na deni!

Wito kutoka kwa Baraza la Makanisa barani Afrika(Aacc)ni kufanya kazi kwa bidii kuhamasisha idadi ya watu wenye dhamana juu ya muktadha wa rushwa na deni.Tunataka Makanisa kujitoa kuangazia shida hii.Lengo ni kuunda umoja thabiti barani Afrika ambao unaweza kushawishi nchi za bara kusuluhisha maswala ya deni na ufisadi.AACCimependekeza mpango wa kusindikiza Makanisa mahalia kupitia utafiti na utoaji wa data.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Wito wa kuchukua hatua, ili rushwa na kuongezeka kwa mgogoro wa deni la nje viweze kumalizika haraka iwezekanavyo katika bara lote la Afrika. Ndiyo uliozinduliwa hivi karibuni na Baraza la Makanisa ya Afrika yote (Aacc), kiungo cha kiekumene kilichoanzishwa mnamo 1963 na kilichopo katika nchi 42 za Kiafrika, kwenye fursa ya mkutano wao kwa njia ya mtandao. Rushwa na deni la nje ni shida zinazounganishwa ambazo zimeingiza mataifa ya Kiafrika katika aina mpya ya utumwa na kunyimwa uhuru, kwa mujibu wa maelezo yao  wakati wa kazi hiyo, ambayo ilihudhuriwa na wawakilishi zaidi ya 70.

Kwa mujibu wa katibu mkuu wa AAC, Mchungaji Fidon Mwombeki amesema Mwaka 2000 nchi nyingi za Kiafrika ziliona deni lao limefutwa, lakini sasa ninaona kwa wasiwasi mkubwa kwamba sasa baadhi yao yana madeni makubwa kuliko ilivyokuwa miaka ishirini iliyopita. Kulingana na takwimu za mwaka 2019 za Shirika la Fedha Duniani, kiukweli, kati ya 2015 na 2018, nchi za Kiafrika zilikuwa na wastani wa ongezeko la deni sawa na asilimia 20 ya Pato lao, wakati maslahi yanaongezeka, kiasi kwamba "Katika miaka miwili iliyopita, serikali za Afrika zimelipa zaidi ya dola bilioni 84 kwa riba kwa wadai wa kigeni."

Kwa baadhi yao anasema linamaanisha kutumia zaidi ya asilimia 45 ya mapato ya kitaifa". Na hii yote ni kwa hasara ya vizazi vijavyo. “Wakati ujao wa watoto wetu umewekwa rehani alisisitiza  Mchungaji Mwombeki kwamba "Hawa hawataweza kushiriki katika maendeleo makubwa kwa sababu ya uzito tunauweka mabegani mwao, hata kabla hawajazaliwa” . Kwa mujibu wa katibu mkuu wa(AACC) amesema pia kengele dhidi ya utumiaji wa deni la nje kama chombo kipya cha mapigano barani Afrika ni wazi. Serikali mahalia zinaacha rasilimali muhimu za eneo hilo, kwa gharama ya raia wao, kwa sababu wanashikiliwa kama mateka kutoka mataifa mengine.

Kwa mjibu wa mchungaji Mwombeki amesisitiza kwamba isitoshe, kulikuwa na kulaaniwa kwa ufisadi na utawala mbaya barani, sababu ambazo zinaongeza mgogoro. Kwa  maana hiyo ndiyo wito kutoka kwa Makanisa barani Afrika ya kufanya kazi kwa bidii kuhamasisha idadi ya watu wenye dhamana juu ya muktadha huu kwamba: Tunataka Makanisa kujitoa kuangazia shida hii, amesema. Lengo ni kuunda umoja thabiti barani kote Afrika ambao unaweza kushawishi nchi za bara kusuluhisha maswala ya deni na ufisadi. Kwa kuzingatia hili, Aacc imependekeza mpango wa kusindikiza Makanisa mahalia  kupitia utafiti, utoaji wa data, kampeni za habari na ukuzaji wa mipango inayoweza kushughulikia changamoto hizi.

Naye Karimi Kinoti, mkuu wa sekta ya msaada wa wakristo barani Afrika,  shirika la misaada na maendeleo ya Makanisa ya Kikristo nchini Uingereza na Ireland: amesema ingawa Afrika imeokolewa na utabiri wa vifo kutokana na  Covid-19 – lakini wote wanajua changamoto za kiuchumi zinazosababishwa na janga na kutengwa kwa jamii. Kwa sababu hii, kutatua mgogoro wa deni la nje ni muhimu sana.  Isabel Apawo Phiri, naibu katibu mkuu wa Baraza la Makanisa Ulimwenguni (Wcc), pia alizungumzia suala hilo ambayo ilitakamabadiliko ya kimfumo katika afya, elimu na ulinzi wa jamii kwa Afrika, wakati wote wa janga hilo na baadaye. “Wakati tunashughulikia ufisadi katika afya, ​​lazima pia tujiulize maswali juu ya jinsi ya kurekebisha na kubadilisha mifumo ya afya na elimu ili iweze kuwanufaisha watu wengi wa Kiafrika."

28 September 2020, 17:03