Tafuta

2020.05.11 Zambia-Wajesuit katika harakati za mapamano dhidi ya covid-19 2020.05.11 Zambia-Wajesuit katika harakati za mapamano dhidi ya covid-19 

Zambia#coronavirus:Wajesuit waipongeza Serikali kutenga mfuko wa dharura ya covid-19

Shirika la Wajesuit nchini Zambia wanaipongeza serikali kuchukua hatua ya kutenga mfuko wa dharura ya covid-19.Hii inaongezea hata misaada mingine ambayo tauyari imetolewa na Papa Francisko wa ajili ya mahitaji ya watu katika nchi hiyo.

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican

Mfuko wa dharura, uwe wa pesa taslimu na kwa njia ya vifurushi vya chakula, ili kupunguza athari za janga la Covid-19 kwa familia zilizo hatarini zaidi ndiyo mpango uliotangazwa nchini Zambia na serikali ambayo inatafuta kwa njia hii, kurekebisha athari za kiuchumi zinazosababishwa na dharura ya kiafya kwenye sehemu dhaifu za watu. Pongeza za uamuzi uliochukuliwa na mtendaji zimeoneshwa na Jumuiya ya Kijesuit hasa katika  Kituo cha Kitaalimungu cha cha Wajesut (Jctr) katika  taarifa kutoka barua ya mkurugenzi mkuu ya wake, Padre  Alex Muyebe.

Hatua ya kulenga kupunguza mateso ya watu ni nzuri

Hii ni hatua nzuri na chanya zaidi iliyolenga kupunguza mateso ya wale waliotengwa katika jamii na kwa watu ambao wamebaki utupu bila kipato na wasio na kinga mbele ya virusi, anaandika Padre Muyebe. Vile vile anasema kwamba athari mbaya ya janga hili limeleta usumbufu wa kukatiza utoaji wa huduma za kijamii.  Kwa maana hiyo iwe mifumo ya ulinzi imara na isiyo imara  yaani mbadala lakini inabaki kuwa bora na muhimu kulinda usalama zaidi nchini na raia wake.

Uingiliaji kati utaleta matokeo chanya

Kwa upande wa Wizara ya Maendeleo Kitaifa imetangaza kwamba inatazamia kutoa ruzuku ya kila mwezi, yenye thamani ya dola 22 za Kimarekani, na  inatarajiwa kwa kila mnufaika anayepewa haki na kusajiliwa katika hifadhi ya data maalum. Mchango huo ulipewa jina “Covid-19 Transgency Cash Social Transfer” , utakuwa na muda wa miezi sita na utaruhusu wahitaji zaidi kununua chakula na mahitaji ya msingi.  Padre Muyebe ameeleza kuwa “Uingiliaji kati huu, pengine pia utakuwa na matokeo chanya juu ya ubora wa lishe ya watu. Wakati huo huo, mkurugenzi wa Kituo cha Kijesuit JCRT pia anaiomba serikali kuongeza misaada kwa asilimia kubwa ya wananchi, akisisitiza jinsi familia nyingine nyingi  ambazo zilionekana zikiwa vizuri kabla ya janga hilo, kwa sasa wameangukia katika umaskini.

Takwimu ya UN:milioni 2 na nusu ya watu wana njaa

Kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni ya Umoja wa Mataifa (UN), kiukweli, watu milioni 2 na nusu nchini Zambia wanakabiliwa na uhaba wa chakula sugu. Wakati huo rekodi za  maambukizi ya covid-19  ya  tarehe 18 Agosti 2020, zaidi ya kesi 9000 zilikuwa chanya na vifo zaidi ya 250. Itakumbukwa kwamba hivi karibuni Papa Francisko ametoa mchango wake wa euro 100,000 kwa  Baraza la Maaskofu nchini Zambia ili kukidhi mahitaji ya haraka ya idadi ya watu wanaoteseka na njaa nchini humo. Zawadi ya Kipapa ilifika mara baada ya msaada mwingine wa Papa kupitia Ubalozi wa Kitume nchini Zambia wa mashine za kupumulia na barakoa za kujikinga na virusi mwezi Julai.

20 August 2020, 14:48