Tafuta

Vatican News
Uwanja wa Mtakatifu Marco huko Venezia nchini Italia Uwanja wa Mtakatifu Marco huko Venezia nchini Italia  (AFP or licensors)

Moraglia:kugundua fadhila ya tumaini hata katika ishara ndogo

Ugumu wa kuanza mwaka wa kichungaji katika jimbo umekumbwa na mgogoro wa kiafya.Patriaki wa Venezia nchini Italia katika barua yake anaelekeza mapendekezo ya dhati kwa ajili ya kuanza kujikita katika upendo ambao ni kisima cha tumaini.Maneno yake yanawalenga hata wanasera za kisiasa nchini Italia.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Mwaliko wa kugundua kwa upya fadhila za tumani zilizo na msingi wa imani na zinazo jidhihirisha kwa dhati katika upendo ndiyo wito uliotolewa na Patriaki Francesco Moraglia wa Venezia nchini Italia, katika waraka wake uliotangazwa tarehe 27 Agosti 2020 wakati wa fursa ya kuanza mwaka mpya wa kijichungaji katika jimbo lake. “Kuanza kwa upya shughuli za kichungaji  ndani ya kipindi cha sasa kilichosababishwa na Covid-19, ni kuonesha kama vile kupitiwa na jangwa na ambalo  halitakuwa rahisi kulivuka lakini hata kwa ugumu huo ni lazima litufikishe mahali pasipo rahisi kwa kutiwa nguvu na  utambuzi kuwa Yesu mfufuka ahaachi kamwe wale ambao wanamkibilia na kumwamini”, anaandikia Patriaki katika waraka wake.

Kujifanya kuambukizwa na upendo

Ni kwa njia ya mtazamo  wa msingi tu  wa Bwana mfufuka ambaye anaishi katika Kanisa, Yeye anaweza kuwa ishara ya tumaini  katika kipindi hiki cha virusi vya corona. Tumaini mbalo haliwezi kukosa kuanza na mshikamano wa dhati, unaooneshwa na kila siku. Leo hii wazo la kijamii katika Kanisa linasikika sana, kuanzia na mwanadamu ikiwa na maana ya kuanzia na fadhila kimaadili ambayo haiwezi  kutenganishwa na ile ya kitaalimungu, amesisitiza Patriaki Moraglia. Kwa maana hiyo ushauri wake unatoka katika maneno ya Papa Francisko wa “kujifanya kuambukizwa na kama alivyokuwa akisema mtaalimungu wa kijerumani Dietrich Bohnoeffer,  kwamba “siyo kutazama mbali zaidi ya hali halisi iliyopo, bali ni nguvu hai,  nguvu ya kuweza kutumainia wakati wengine wanapokata tamaa.

Kuanguka kwa uchumi kijamii kufuatia na dharura ya kiafya

Katika tafakari ya Patriaki Moraglia wa Venezia, amejikita na mtazamo wa sasa ulio mzito wa kuanguka kwa uchumi kijamii kufuatia na dharura za kiafya za Covid-19 nchini Italia, ambapo kwa kiasi fulani bado unaendelea kugandisha hali halisi, ambayo inakabiliwa na umaskini hasa unaozidi kuwakumba watu walio na kipato cha chini. Hatari kubwa anabainisha ni ile ya kijamii nchini mahali ambapo kunaonesha manung’uniko yaliotanda, na ambayo tayari katika miaka ya hivi karibuni utafiti wa Censii ulibainisha hatari ya kuzuka fujo. Ili kuzuia  fujo hizi waraka unabainisha kwamba wote wanaalikwa kuwa sehemu mmoja. Hii ni pamoja na Umma, watu binafsi, makampuni, asasi za kiraia na kidini, watu wa kujitolea na kwa njia hiyo wanaalikwa wote kuwa katika mtandao mmoja  ili kuzuia malumbano yanayozidi na kuhakikisha wale ambao wana watoto wadogo waweze kulindwa na rasilimali zake pia. Wote lazima kuchangia kugundua kujenga kwa upya kiungo cha kijamii.

Ujumbe wake unawalenga sera za kisiasa

Katika muktadha huu Patriaki  anawageukia kwa namna ya pekee sera za kisiasa na kwamba “kama wakristo na wazalendo, tuombe ili kuwa na siasa zisizo na  ugomvi na malumbano ili kuwa na maamuzi ya dhati yanayotazama nchi, kwa manufa ya wote; aidha kuwa na siasa ambazo zinazungumza kidogo kwa njia ya kijami na kwa njia ya kufanya matendo yenye tija na kujenga;  yenye maana kuliko maneno matupu. Ili kukabiliana na dharura ya kijamii, Patriaki anaushauri jumuiya ya kikanisa mambo mawili yaliyo madogo  sana kama ishara za dhati ambazo zinakwenda sambamba  na mantiki ya kiinjili kwa kutumia  mfano wa mjane ambaye alitoa kile alichokuwa nacho katika hekalu, lakini kikazidi wale ambao walikuwa navyo kwa mujibu uthibitisho wa Yesu.

Kumsaidia mtu mwenye shida kwa manunuzi ya mahitaji muhimu

Katika ushauri huo wa ishara ndogo kwa njia hiyo ishara ya kwanza ni kuchukua mtindo maalum lakini wa kweli wa mtu ambaye kwa hali yake  kijamii haonekani. Mtindo utakuwa tofauti kulingana na uwezo, kwa maana hiyo inawezekana kumsaidia katika kununua mahitaji ya wiki vitu ambavyo ni msingi. Upendo kama huo kwa kutafakari hauwezi kutukosesha lolote bali unavutia baraka ya Mungu kwao amesisitza

Kufungua Parokia kwa ajili ya shule

Ishara ya pili ya dhati ni kufungua miundo ya majengo ya maparokia kwa ajili ya shule ili kuwezesha nafasi zaidi, kwa kufikiria hali ya sasa ya matatizo ya kupokea wanafunzi wote kwa kufuata kanuni ya umbali wa usalama. Kuanza kwa upya katika ulimwengu wa shule, kwa hakika ni suala muhimu la jaribio kubwa katika nchi nzima, kushindwa kwa mantiki hii inaweza kuwa ishara hasi kwa watu wote, anabinisha Patriaki kwa kukumbuka jinsi gani mafundisho ya umbali yameleta adhabu kwa wale wasio kuwa na uwezo kiuchumi, na kiteknolojia.

Kumbukizi la miaka 1600 la Venezia

Kanisa la Venezia linaweza kuchangia kwa namna hiyo kuweka nafasi zake zilizopo kwa ajili ya shughuli za kitaaluma na mafunzo. Barua yake ya kichungaji inahitimishwa kwa kusema kuwa, kumbukizi la miaka 1600 tangu kuanza kwa Venezia iwe kwa muktadha huo wa kuanza upya kijamii na kiuchumi katika fursa ya kupanga wakati wake endelevu wa mji wa aina yake uliozungukwa na maji na kwa pamoja katika mji wa ulimwengiu ambao ni sehemu ya dunia yote.

28 August 2020, 17:03