Vatican News
2020.03.16 Msalaba uliochongwa na Donatello 2020.03.16 Msalaba uliochongwa na Donatello  

Papa Francisko:fumbo la maumivu ya Kristo yanaonekana kwa watu wasio na hatia na kuteseka!

Katika ujumbe wa Papa Francisko kwenye mitandao ya kijamii,anashauri kuweka kipaumbele cha mafumbo ya Pasaka katika maisha ili kuhisi maumivu ya majeraha ya Kristo msulibiwa ambayo yumo kwa wote wanaoteseka na wasio na hatia.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Jumamosi tarehe 29 Agosti 2020 Papa Francisko katika ujumbe wake kwa njia ya mitandao ya kijamii anasema “Kuweka mafumbo ya Pasaka katika kitovu cha maisha maana yake ni kuhisi maumimivu  ya majeraha ya Kristo msulibiwa ambayo yumo katika waathiriwa wengi wasio na hatia katika vita, vurugu, waliobaguliwa dhidi ya vitaa, mjanga ya mazingira na umaskini”.

Tafakari fupi kuhusu kifodini cha Mtakatifu Yohane Mbatizaji

Papa Francisko anazungumzia juu ya maumivu na majeraha kupatikana katika watu waathiriwa, wasio na hatima, wanaoteswa, ni linalopata mwangwi katika siku ambayo Mama Kanisa kila tarehe 29 Agosti ya kila mwaka anafanya kumbukumbu kifodini cha Mtakatifu Yohane mbatizaji. Liturujia kwenye Somo la Injili ya Mk 6:17-29 inakumbusha jinsi Mtakatifu Yohane Mbatizaji alivyokatwa kichwa kwa mujibu wa matashi ya mke wake Mfalme Herode kupitia mwanae kutokana na chuki aliyozidi kukuza ndani mwake kwani alichukia sana ukweli uliotlewa na nabii huyo wa Mungu.

Hakika neno la Mungu ni mshale wenye ncha kali kali inayosumbua roho. Yohane Mbatizaji alikuwa ni mwaminifu na alisema ukweli na kutetea haki katika Neno la Mungu, ambalo linazibua duku duku, kwa mfano wa keshi hii ya mke wa Herode ambaye hakupendelea uongofu bali giza hadi kutekeleza tendo hilo baya. Na hii inatuonesha ni jinsi gani mke wa mfalme Herode anavyoiongoza familia ya kifalme hadi kuidumbukiza  kwenye dhambi ya kumuua mtu hasiye na hatia yaani nabii wa Mungu, Yohane Mbatizaji. Ni uonesha wa wazi ambao familia inaweza kuwa mfano mbaya sana katika makuzi ya watoto.

Kuna haja ya kuwa na familia thabiti

Kuna haja ya kuwa na familia thabiti yenye kupinga ushawishi mbaya ndani ya familia! Ushawishi wa Herodia ulifanya kumwondoa  mwenye haki mbele yake. Kwa njia hiyo ushauri ni kuwa Mama ndani ya familia anapaswa kutoa mchango mkubwa wa kujenga familia yake, na siyo kubomoa, kuwafundisha watoto maadili mema na siyo ukatili ambao pia kupitia kwa watoto unaweza kukua kizazi hadi kizazi. Ni lazima kuepuka dhambi na tamaa mbaya. Fundisho hili kwa akina baba pia kwani siyo kila kitu ni kukubali kwa sababu tu umetoa ahadi. Inahitajika kutathimini ni kitu gani  cha kumzawadia mtoto, kwa manufaa gani ya maisha  ya sasa na baadaye ? Tusitawaliwe na tamaa mbaya na baadaye kutelekeza wasio na hatia kama  ilivyomwandamu  Mtakatifu Yohane Mbatizaji.

29 August 2020, 14:09