Tafuta

Vatican News
Cei: Rais wa Baraza la Maaskofu Italia Kardinali Gualtiero Bassetti Cei: Rais wa Baraza la Maaskofu Italia Kardinali Gualtiero Bassetti  (ANSA)

Italia:Kard.Bassetti katika mkutano Rimini anasema tutazame Mungu kwa mshangao wa manabii!

Katika maadhimisho ya Ibada ya Misa iliyoongozwa na Kardinali Bassetti,Rais wa Baraza la Maaskofu Italia wakati wa kufungua"mkutano wa urafiki kati ya watu" huko Rimini,Italia wazo kuu ni mwendelezo wa mada ya mshangao iliyokita ndani ya Mkutano huo.Mantiki ya mshangao ni njia ya kuchota katika siri za Mungu na kutokata tamaa ya maisha wakati kuna zawadi ya Bwana.Ushauri ni kutazama Mungu kwa mshangao kama manabii.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Leo hii ni kuliko hapo awali ambapo wakristo wanaalikwa kuwa na nguvu ya kujikita kusoma alama za nyakati na kusema maneno ya kinabii, kwa midomo na wakati huo huo ikiambatana na ushuhuda wa maisha. Ni maneno ya Kardinali Gualtiero Bassetti, Rais wa Baraza la Maaskofu nchini Italia (CEI) wakati wa kufunga siku ya mwisho ya mkutano wa 41 wa “urafiki kati ya watu” huko Rimini nchini Italia ambapo alitoa hotuba yake ndefu. Katika tafakari yake  pana kwanza akijikita  juu ya mshangao, kama njia ya kuchota kutoka katika Siri ya Mungu na bila kuachilia maisha ili baadaye kuona nguvu ya zawadi ya msimu mpya wa Kanisa.

Bila mshangao tunabaki viziwi mbele ya ukuu wa Mungu

Mshangao huu pia umejitokeza kwa mujibu wa Kardinali Bassetti kwa namna ya pekee kwenye mkutano huu wa kwanza mara baada ya dharura ya COVID 19 na katika janga, kwa maana hiyo hata bila kuwa na umati mkubwa anaongeza kama ulivyokuwa kawaida katika kila  kipindi hiki cha kiangazi, kwenye mkutano unaondaliwa kila mwaka na Jumuiya ya Comunione na Liberazione ambapo mwaka huu wameongozwa na mada isemayo “kukosa mashangao, tunabaki viziwi mbele ya ukuu”. Kardinali Bassetti katika kujikita kutazama hali halisi ya janga hili la corona ameonesha duku duku lake lakini pia matumaini kwa sababu bila mshangao katika maisha ni kupoteza maana na kuchanganyikiwa.  Aidha amekumbusha mada iliyotokana na kazi ya mfalsafa mmoja wa kiyahudi wa marekani Abraham Heschel.

Mshangao wa Paulo mbele ya mafumbo ya Kristo

Mshangao ni hali ya kifalsafa lakini pia yenye mtindo wa mawazo ya kinabii na ndiyo hasa wakati huu wa kipindi cha kinabii amesema Kardinali Bassetti. Aidha anakumbusha kuwa katika hitimisho la barua ya Mtakatifu Paulo kwa Warumi, anasema “hakuweza kuzuiwa katika mshangao mbele ya hekima ya Mungu ambaye ni kitu kingine kabisa, licha ya kutambua umbali wake na ndiyo maana ya mshangao sasa unaoruhusu Paulo aweze kugundua Yesu Kristo. Kutoka katika mtazamo wake wa kifarisayo kama Sauli unakuwa ni mshangao mkamilifu na upendo uliotambuliwa kwa ukuu wa mafumbo ya Kristo. Hata Mtakatifu Petro ambaye yuko mstari wa mbele katika somo la Injili ya siku, amesisitiza Kardianali  Bassetti kwa sababu ni mara elfu alishikwa na mshangao wa kukaa na Yesu kwa mfano, wakati wa muujiza wa samaki na ndiyo mshahangao  unamruhusu Petro atambue kwa taratibu utambulisho wa Yesu hadi kufikia kukiri kwamba  “Wewe ndiye Kristo”. Kardinali Bassetti amesisitiza kuwa  manabii mara nyingi wanajiachia katika mshangao na wana uwezo wa kutambua uwepo wa Mungu ulimwenguni na katika wakati ambamo tunaishi, na kuelewa hadi mapana na marefu  maana yake na ndiyo maana hata leo hii wakristo wanaombwa kwa nguvu zote kugundua alama za nyakati.

Tujifunze mshangao kupiti kwa mwanabii wako karibu na watu waombezi kwa Mungu

Hii ndiyo kazi ambayo manabii wa Biblia walikuwa tayari nayo, ambao kwa upande mmoja, hawakuogopa kuwaeleza  watu, hasa watawala na viongozi wa dini, kulaani ukosefu wa haki na ukosefu wa uaminifu, lakini pia walijua jinsi ya kutia moyo na kuhimiza wakati mgumu, wakiwakilisha sauti moja ya tumaini wakati wa kukata tamaa. Hii mara nyingi inajitokezaa, Kardinali Bassetti anakumbusha kuwa  hata nabii Ezekieli, ambaye mbele ya uhamisho na mgogoro mkubwa zaidi wa Israeli, aliitwa kutabiri juu ya mifupa kwamba watu watazaliwa upya. Inatokea namna hiyo hata kwa manabii kutazama mambo kama ayaonavyo Mungu na kushangaa, vile vilevile walikuwa na kazi ya kusali kwa ajili ya kuwaombea watu wao na kuingilia kati kuomba msaada kutoka kwa  Bwana kwa nguvu zao na kujiweka tayari kwa maisha ya kujitoa wenyewe.” Bila kuwa na sauti ya manabii ipo hatari kubwa ya kuangukia kwenye udanganyifu katika wakati wa sasa na umilele unaosukana na ubinadamu amethibitisha Kardinali Bassetti. Huo ni mfano wa mwanga kwa kile ambacho wakristo leo hii wanaombwa zaidi na zaidi kuweza kugundua alama za nyakati na kunena maneno ya kinabii kwa  midomo yao lakini wakikumbuka kwa hakika kuambatanisha na ushuhudua wa maisha ya dhati ameongeza kusisistiza zaidi

Mfalsafa Heschel anasema ubinadamu utapoteza dhamiri yake kwa kukosa mshangao

Kardinali Bassetti amerudia kutazama maneno ya mfalsafa Heschel ambaye alisisitiza kwamba maendeleo yanafanya upotezaji wa hisia za kushangaza na kwamba ubinadamu hautapotea kwa sababu ya kukosa habari, badala yake “mwanadamu, aliyejazwa habari, hataweza kutofautisha na mara nyingi angeangukia kuwa mwathirika wa udanganyifu ambao una athari mbaya ya kufadhaika kwake, kwa  madai ya kukombolewa  kutokana na mshangao wa watu rahisi. Na kwa maana hiyo, Heschel alisema, ubinadamu utapoteza dhamiri yake kwa kukosa mshangao, kwa sababu mwanzo wa furaha upo katika kuelewa kuwa maisha bila mshangao haifai kuishi. Amehitimisha Kardinali .

Mada itakayoongoza toleo la 42 la "Urafiki kati ya watu" 2021 ni "Ujasiri wa kusema mimi"  

Hata hivyo  Ujasiri wa kusema  ni “mimi” ndiyo itakayokuwa mada kiongozi ya  toleo la 42 la “mkutano wa urafiki kati ya watu” huko Rimini nchini Italia utakaofanyika kuanzia tarehe 20 hadi 25 Agosit 2021. Mada hiyo imetangazwa wakati wa kuhitimisha mkutano wao, Jumapili tarehe 23 Agosti mbapo katika taarifa yao wanabanisha kwamba inatakiwa “kushirikishana sababu za matumaini yenye uwezo wa kukabiliana na changamoto ambazo tunazisubiri na kujenga wakati endelevu; na kwa kuwa na utambuzi moyoni mwa matarajio ya  kizazi cha vijana”. Kwa hakika  umakini kwa vijana umekuchukua nafasi kubwa katika  mada nyingi za mkutano  japokuwa si kwa kwa sababu ya kufanya mkutano kuhusu shule na juu ya elimu, lakini pia juu ya uchumi na ustawi wa kijamii. Na Ufunguo msingi wa maneno katika Mkutano huo mbele ya hali halisi ya janga linalofanyiwa uzoefu leo hii, la covid-19 umeoneshwa hata matumaini, katika mchango wa hotuba ya Padre Julián Carrón, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Comunione na Liberazione (CL) na ambayo imekita moja kwa moja katika moyo wa matumaini kufuatia na uchunguzi wa asili na sababu zake.

24 August 2020, 12:18