Tafuta

Vatican News
2020.08.24  wenyeviti wa Mabaraza ya Maaskofu Amerika ya Kusini (CELAM) 2020.08.24 wenyeviti wa Mabaraza ya Maaskofu Amerika ya Kusini (CELAM) 

Maaskofu Amerika Kusini wanaomba mviongozi wa nchi kutafuta suluhisho la pamoja!

Kwa upande Bara la Amerika ya Kusini ili kushinda mgogoro wa kifaya ambo umeshasababisha vifo zaidi ya watu miambili elfu Baraza la Maaskofu Barani huko CELAM wanaomba taasisi kuwa na jitihada za pamoja ambazo zipelekee kutazama wakati ujao ili kuondokana na mateso ya sasa.Mtazamo maalum ni katika suluhisho la kiafya na chanjo ili umakini uwe kwa maskini.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Suluhisho la haraka na kushirikishana ili kuondokana kwa haraka na mgogoro ambao umesababishwa na janga la Corona ndiyo  yaliyomo katika barua ya wenyeviti wa Baraza la Maaskofu Barani Amerika ya Kusini (CELAM) wakiwalekeza viongozi wakuu wa nchi na serikali huko wakiomba jitihada za pamoja ili kuondokana na madhara makubwa ya covid-19 ,lakini wakati huo huo kutazama wakati endelevu kwa sababu ndoto ya taifa kubwa bado iko mbali sana. Kwa ujibu wa Shirika la Afya duniani WHO , linathibitisha kuwa Barani Amerika ya Kusni ni zaidi ya vifo vya watu 200, 000 waliorekodiwa kwa sababu ya virusi vya corona. Inatarajiwa kuwa miezi ijayo kiasi kikubwa cha umaskini kitagusa ambacho hakijawahi kusikika yaani watu  zaidi ya milioni 250 ikiwa ni asilimia 35 ya watu.

Kanisa mahali kwa sababu  ya wasiwasi wake ni kwa watu walio wadhaifu na kuongezeka kwa vurugu na hofu kubwa inayotishiwa watu. Kwa kukumbusha maneno ya Papa Francisko aliyosema tarehe 19 Agosti, maaskofu wa Celam wanasisitiza kwa wingi wao kwa namna ilivyo muhimu kupata chanjo ya kuzuia covid-19 lakini wakati huo huo ni msingi kushinda virusi vikubwa vya ukosefu wa haki kijamii, ukosefu wa usawa na kubaguliwa.

Maaskofu aidha wanatambua jitihada kubwa ya Jumuiya ya kisayansi na wanaomba kuwa chanjo itakayo patikana iweze kuwa salama na siyo ya kudhulu afya ya binadamu ili kuweza kukabiliana na kile kiitwacho magonjwa yasiyoonekana yatokayo katika hali ya kijamii na kiuchumi isiyo sawa, na ni  magonjwa ambayo yanasababisha vifo vingi zaidi ya covid, wanasisitiza. Kwa bahati mbaya janga limeonesha wazi   ukosefu mkubwa wa miundo hasa ya kijamii. Wanauchumi na wanasayanisi wanaalikwa kugundua kinga mpya. Vile vile katika barua yao wanabainisha kuwa kile ambacho kinaendelea kutokea siyo adhabu kutoka kwa labda tunaweza kusema ni matokeo ya dhambi za miundo mbinu na kiekolojia.

Maaskofu wanahitimisha waraka wao wakiomba umakini kwa namna ya pekee kwa ajili ya wanawake na wanaume wa nchi yao. Hasa maskini zaidi, kama namna  wafanyavyo Kanisa hata katika kipindi hiki kigumu ni kujikita katika ujenzi wa kiungo cha kijami cha Amerika ya Kusini na visiwa vya Carribien kuanzia na ulinzi wa maisha.

26 August 2020, 16:04