Serikali ya Uganda imewatia pingu watu kumi na mmoja walioshiriki katika tuhuma za kubomoa Kanisa Anglikan Parokia Ndeeba nje kidogo ya Jiji la Kmapala, hapo tarehe 8 Agosti 2020. Serikali ya Uganda imewatia pingu watu kumi na mmoja walioshiriki katika tuhuma za kubomoa Kanisa Anglikan Parokia Ndeeba nje kidogo ya Jiji la Kmapala, hapo tarehe 8 Agosti 2020. 

Kanisa Anglikan la Mt. Petro, Ndeeba Uganda Labomolewa!

Kanisa la Mtakatifu Petro wa Uganda, huko Ndeeba lilijengwa takribani miaka 49 iliyopita. Kumekuwepo na mgogoro kati ya viongozi wa Kanisa na mfanyabiashara mmoja aliyetambuliwa kwa jina moja tu la Dodovico. Jaji Eudes Keiritima wa Mahakama kuu, aliamuru mwaka 2019 Kanisa hili libomolewe, kwa kuwa lilikuwa limejengwa kwenye eneo lililokuwa linamilikiwa kinyume cha sheria.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda ameamuru watu kumi na moja wakiwemo askari watatu, kukamatwa na hatimaye, kufikishwa kwenye vyombo vya sheria kujibu tuhuma za mashitaka yanayowakabili kwa kubomoa Kanisa Anglikan la Parokia ya Ndeeba, nje kidogo ya Jiji la Kampala, Uganda. Tukio hili limetekelezwa usiku wa tarehe 8 Agosti 2020. Zoezi hili lilisimamiwa na Askari watatu wa Jeshi la Polisi ambao pia wamepigwa pingu kwa uzembe. Serikali ya Uganda kwa sasa imeanza uchunguzi wa kina ili kubaini nyaraka za mmliki halali wa eneo hili ambalo Kanisa la Mtakatifu Petro wa Uganda, huko Ndeeba, lilikuwa limejengwa hapo.

Kanisa la Mtakatifu Petro wa Uganda, huko Ndeeba lilijengwa takribani miaka 49 iliyopita. Kumekuwepo na mgogoro kati ya viongozi wa Kanisa na mfanyabiashara mmoja aliyetambuliwa kwa jina moja tu la Dodovico. Jaji Eudes Keiritima wa Mahakama kuu, aliamuru mwaka 2019 Kanisa hili libomolewe, kwa kuwa lilikuwa limejengwa kwenye eneo lililokuwa linamilikiwa na mfanya biashara huyo.  Kunako mwaka 1981, Eneo hili lilitolewa kama zawadi kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa na limebomolewa wakati wa usiku, hali inayoonesha kwamba, kuna siri kubwa ambayo imefichika bado. Jeshi la Polisi lililopaswa kutekeleza dhamana na wajibu wake wa kusimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao, likageuka na kuwa shuhuda wa zoezi zima la kubomoa Kanisa hili.

Viongozi wa Kanisa wameiomba Serikali kufanya uchunguzi wa kina, ili ukweli uweze kupatikana, haki na amani kurejea tena. Viongozi mbali mbali wa Makanisa, wapenda amani na uhuru wa kuabudu wamesikitishwa sana na kitendo hiki ambacho kimeifedhehesha sana Serikali ya Uganda. Kanisa la Mtakatifu Petro wa Uganda, huko Ndeeba, limekuwa ni kimbilio la faraja kwa waamini wakati huu wa janga la maambukizi makubwa ya homa ya mapafu inayosababishwa na Virusi vya Corona, COVID-19.

Kanisa Uganda
11 August 2020, 14:05