Ziara ya  Kitme ya Papa Francisko nchini Ireland katika Mkutano wa kimataifa wa familia 2018 Ziara ya Kitme ya Papa Francisko nchini Ireland katika Mkutano wa kimataifa wa familia 2018 

Ireland:Ask.O'Neary:Kupalizwa Maria ni kukumbusha kuwa na matumaini!

Katika fursa ya Siku Kuu ya Kupalizwa mbinguni Mama Maria,Askofu Mkuu wa Jimbo kuu Katoliki la Tuam nchini Ireland wakati wa maadhimisho ya Misa Takatifu katika Madhabahu ya Bikira,Mama yetu wa Knock,Malkia wa nchi ya Ireland amesema kupalizwa kwa Maria ni kutukumbusha matumaini katika kipindi kisicho na uhakika.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Yamekuwa ni matumaini yaliyo tuongoza hasa katika wakati huu mgumu wa kipindi cha Covid-19, ambacho kimeona na kufanya kukumbatia mahangaiko, mateso na ukosefu wa uhakika. Uwezo wa kutumia mambo hovyo umewekwa katika majaribu kwenye jamii zetu. Tumehisi wote kuwa kama waathirika, wadhaifu na tumeomba kuwa na kile ambacho kinafaa na kuhitajika katika wakati ujao. Ndiyo sehemu ya mahubiri ya Askofu mkuu O'Neary wa jimbo katoliki la Tuam nchini Ireland wakati wa maadhimisho ya Misa Takatifu katika fursa ya Siku kuu ya  Kupalizwa Bikira Maria mbinguni, kwenye  Madhabahu ya Mama yetu wa  Knock, Malkia wa nchi ya Ireland na madhabahu kuu ya kitaifa.

Tunahitaji chachu ya matumaini

Mbele ya hali halisi hii, Askofu O’Neil amesema tunahitaji kuwa na  sababu ya matumani  hasa  ikiwa tunataka mwenda mbele  na kuzuia kuangukia katika mitindo wa mahangaiko ya ubinafsi ambayo hayazalishi katu nguvu, wala ujasiri na wala uhuru”. Moja ya hatari  kubwa inayoikabili jamii leo hii, amesema askofu Mkuu kuwa kikweli “ni maana ya ukosefu wa nguvu, mawazo ambayo ulimwengu unakuwa nje ya udhibiti na ambapo matatizo yanakuwa makubwa sana  kiasi cha kukosa namna ya kupata suluhisho. Licha ya hayo Mungu ambaye tuna mwamini, amekumbusha Askofu mkuu, ni Mungu ambaye anaruhusu kufanya uzoefu wa matumaini, hasa hasa wakati mahangaiko yanayoonekana kuwa juu zaidi kwa maana wala haishangazi kutokana na kwamba alifanya awe na uzoefu hata Mama yake ambaye ni Mama yetu”, amesisitiza Askofu Mkuu.

Siku kuu ya Kupalizwa inapanua upeo

Askofu Mkuu wa Tuam akiendelea na ufufanunuzi huo  amesisitiza kwamba ndiyo maana ya kina ya Siku kuu ya Kupalizwa mbinguni. “Siku kuu hii inapanua mawazo na maono yetu kwa kile ambacho ni, na ambacho kinawezekana; inazungumza kwa namna iliyo wazi kabisa ya kuwa na matumaini", amesisitiza Askofu mkuu. “Yawe ni mapambano binafsi, ugonjwa mbaya, kifo cha mtu mpendwa sana, ugumu wa mahusiano binafsi ya kibinadamu, wasiwasi wa uchumi, mahangaiko ya wakati endelevu, lakini Mama Maria yuko nasi, na anaelewa na kutoa msaada mkubwa wa upendo”.

Siku zijazo zimefunguliwa wazi na  kuna fursa mpya

Askofu Mkuu akifafanua zaidi  katika mahubiri yake amesema “ Walakini, tumaini sio tumaini la uwongo. Yeye hajapuuzi changamoto tunazokabiliana nazo au vizuizi ambavyo tunavipata na kufanya uzoefu navyo. Yeye anaruhusu sisi kufanya uchambuzi wa kweli na muhimu ya kwamba ni wapi tulipo leo hii. Aidha ameongeza Yeye anatuchangamotisha kuwa na jitihada  za kufuata ukweli na hatatuacha sisi watumwa wa kushindwa kwetu; Yeye anatukumbusha kwamba, siku zijazo zimefunguliwa wazi na kwamba kutakuwa na maendeleo zaidi na fursa mpya", amehitimisha Askofu Mkuu O’Neary.

18 August 2020, 15:13