Tafuta

Kutoa vipaji nchini Ghana Kutoa vipaji nchini Ghana  

Ghana:Kipindi cha janga lazima kuthamanisha Kanisa la nyumbani!

Katika ujumbe kwa njia ya video, Askofu Mkuu wa Cape Cost mesema kuwa katika kipinid hca janga la virusi vya corona ni muhimu kutahamanisha Kanisa la nyumbani.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Ninasali ili nyumba zetu ziweze kugeuka kuwa kweli Makanisa ya nyumbani, mahali ambamo familia inasali pamoja na kubaki na umoja. Ndiyo sala ya kina ya Askofu Mkuu Cape Coast, nchini Ghana, Askofu Mkuu  Charles Palmer-Buckle, katika ujumbe wake kwa njia ya video, uliotangazwa katika ukurasa wa Facebook wa Baraza la kiaskofu mahalia.

Kubaki ndani ya nyumba inawezekana kuwa Kanisa la nyumbani

Kwa mujibu wa Askofu Mkuu Buckle anasema, katika kipindi cha virusi vya corona, kubaki ndani ya nyumba inaweza kweli kuwa ngumu kwa watu wengi, lakini ndiyo kipindi hasa cha kufanya familia ziweze kuishi kama Kanisa la nyumbani, mahali ambamo upendo, amani, furaha na ushirishano vinatawala.

Salini na familia ili kushinda kila aina ya changamoto

Askofu Mkuu Palmer-Buckle aidha amegeukia upande mwingine kuhusu vitendo vya  ya kutumia nguvu na ambavyo vimekuwa hatari zaidi inayoongezeka katika nchi kwa sababu ya kulazimishwa kubaki karantini, kutokana na hili amesema: “ kwa wale ambao wanatabia ya kusababisha migogoro na kutumia nguvu ninawambia:salini pamoja na familia zenu, ili Mungu aweze kuwasaidia kushinda kila aina ya changamoto”.  Katika ushauri wa Askofu Mkuu wa Cape Cost amesem: “ kula pamoja chakula, kusoma pamoja Maandiko Matakatifu, kujua kwa pamoja ya kwamba  Yesu yuko katikati yenu” kwa sababu kama isemavyo Injili ya Matayo “mahali palipo  na wawili au watatu waliounganika kwa jina langu, mimi niko kati yao” (Mt 18, 20).

Askofu mkuu amewatia moyo

Askofu Mkuu Buckle amewatia moyo hata wafamilia wote ili wapokee fursa hii ya kuishi ndani kwa kulazimishwa kwa ajili ya kufanya tathimini ya kina ndani ya dhamiri binafsi  lakini  si tu hata kwa wenzi, kati ya kizazi hiki cha wazazi na watoto katika mtazamo wa upamoja. “Nyumba zetu lazima zigeuke kweli kuwa Kanisa la nyumbani  mahali ambamo yumo Mungu kweli kweli.” Ujumbe kwa njia ya video unahitimishwa kwa baraka yake, akiwa na ishara wazi za mavazi rasmi ya kanuni ya afya za kuzuia maambukizi kwa maana hiyo akiwa na barakoa.

Maambukizi nchini Ghana bado yanaendelea

Ikumbukwe tarehe Mosi Agosti nchini  Ghana imethibitishwa  kesi 35.501 za  Covid-19, wakati wagonjwa waliopona ni 32.096 na vifo ni 182. Maadhimisho ya kiliturujia kwa uwepo wa waamini, yameanza tangu  tarehe 7 Juni 2020, mara baada ya miezi 3 ya kusitishwa, lakini kwa mujibu wa kanuni za usalama, ni lazima kutumia barakoa, kusafisha mikono, umbali kijamii na uwepo wa watu wachache wasiozidi 100 katika Makanisa. Hivi karibuni kwa mujibu wa maombi ya Kanisa Katoliki, Rais wa  Nchi Nana Akufo-Addo ameweza kuruhusu kuongeza muda wa ibada kutoka lisaa limoja kwenda masaa mawili!

01 August 2020, 14:35