Tafuta

Ndako ya biso maana yake nyumba yetu ni kituo cha kuwapokea watoto wa barabarani ambapo tangu mwaka 2004  nchini Congo DRC Ndako ya biso maana yake nyumba yetu ni kituo cha kuwapokea watoto wa barabarani ambapo tangu mwaka 2004 nchini Congo DRC 

Congo Drc:Utume wa watoto kwa wakati ujao uliobora!

Ndako ya biso maana yake nyumba yetu ni kituo cha kuwapokea watoto wa barabarani ambapo tangu mwaka 2004 hadi sasa wamekwisha wasaidia watoto 2,500 na kuwawezesha kurudi katika familia zao.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tangu 2004 katika utume wa kimisionari wa Ndako ya biso maana yake nyumba yetu huko Lingala nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imewezesha watoto 2,500 wa barabarani kurudi katika familia zao asili. Matatizo ya kiuchumi mara nyingi yanalazimisha familia hizi kuwacha watoto hao. Kituo hicho cha utume wapo  wahudumu 40  wanaowasaidia kuwaandaa  watoto hao ili waweze kurudi baadaye katika nyumba zao na kuwawezesha wawe na wakati endelevu ulio bora na  kwa ajili ya familia zao.

Ukubwa wa nchi lakini pia matatizo mengi ya uchumi na sera za kisiasa

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo  DRC ni nchi ya pili kwa ukubwa katika bara la Afrika na nchi yenye watu wengi sana wanaozungumza lugha ya kifaransa. Tangu mwaka 2016 nchi hiyo imepata pigo kubwa  la mgogoro wa sera za kisiasa na matokeo mabaya ya kuhairishwa kwa uchaguzi wa urais uliokuwa unatarajiwa kufanyika kunako tarehe 20 Desemba. Lengo la wakati huo la Rais Joseph Kabila lilikuwa la kutaka kubaki moja kwa moja madarakani. Kwa maana hiyo yalianza maandamano ya kupinga nchi nzima na mgogoro huo ukazaa kipeo kibaya cha kiuchumi, kushuka kwa uwekezaji na kwa namna ya pekee hasa wawekezaji wa nchi za kigeni.

Makovu ya mgogoro wa kisiasa unaonekana zaidi katika janga

Matokokeo haya mabaya yanaonekana hadi leo  hii na hasa kwa kuongeza zaidi ya  janga la virusi vya corona au covi-19, a mbavyo kwa wastani vimeangusha sana maisha ya kiuchumi nchini humo na zaidi kuwakumbuka hasa watu wanaoishi maisha ya kati. Kwa mfano katika mji mkuu wa kishansa, kwa namna ya pekee mgogoro huu umesikika sana. Katika mji huu mkubwa ambao ni mji wa tatu kuwa na watu wengi barani afrika na ni mji wenye watu wengi sana ulimwenguni kwa kuwa na wakazi  milioni 13,2.  Masuala ya kisiasa na kiuchumi yanahusiana zaidi na mienendo mipya ya kijamii, kwa namna ya pekee ukubwa ambao unapeltkea haya kuvujika kwa familia nyingi. Katika muktadha huo, ni mapambano ya kila siku katika kutafuta namna ya kuishi na ndiyo hali halisi.

Ushuhuda katika Jumuiya ya Chemin Neuf

Haya yamesema na Jean-Pierre Godding, katika mahojiano na shirika la habari za kimisionari Fides. Mwanasheria na mtaalam wa masuala ya kijamii, mwenye asili ya Ubelgiji, tangu  2004  Jean-Pierre Godding anaishi DRC, mahali ambapo yeye ni mhusika kama mjumbe mlei wa Jumuiya ya “Chemin Neuf”  ya utume wa kimisionari ya “Ndako ya biso”, mahalia ambapo wanawakaribisha na kuwasaidia watoto wa mitaani jijini Kinshasa. Kwa mujibu wa maelezo yake anasema, kinachotofautisha “Ndako ya biso” na mahali pengine pa kukimbilia watoto ni kuhusu malengo na mipango yake. Kituo hicho si tu kwa ajili ya  kuweka mahali pa makaribisho ya watoto na kuishia hapo, hapana kazi yao ni  kuwasaidia ushirikishwaji katika familia zao za asili.

Ni karibu watoto 25 na 30 elfu wa mitaani na sehemu kubwa siyo yatima

Kadirio la  hali halisi ya watoto wanaoishi mitaani na barabani ni kuanzia 25 na 30 elfu. Pamoja na hayo jambo la kushangazaa sehemu kubwa watoto hao  yatima, amethibitisha. Baada ya kutorpka kwao au kufukuzwa kwa sababu tofauti  wahudumu  wenye taaluma ya utume huo katika kituo hicho wanafanya kazi ya kubaini familia zao za asili, kuzungumza nao na baadaye kuwashirikisha  ili watoto hao waweze kurudi katika familia zao, na hatimaye wanarudi. Kuhusiana na suala hili, hata hivyo Jean-Pierre Godding hivi karibuni amechapicha kitabu kiitwacho  “Piccoli banditi, piccoli ladri, piccoli maghi”, maana yake “majambazi wadogo, wezi wadogo, waganga wa kienyeji wadogo. Mbinu za msaada na mapatano ya watoto wa barabarani Kishasa”(Cerf, 2019).

01 August 2020, 10:15