Tafuta

2020.03.08 siku ya sala kwa wanawake nchini Afrika Kusini 2020.03.08 siku ya sala kwa wanawake nchini Afrika Kusini 

A.Kusini-Mwezi wa wanawake:Kuhamasisha nafasi ya wanawake katika Kanisa!

Wanawake lazima wawe na mafunzo ya juu na kuhamasisha nafasi msingi ya wanawake katika Kanisa.Majimbo yangekuwa maskini bila kuwa na uzoefu wao.Amebainisha hayo Askofu Phalana wa Jimbo la Klerksdorp,nchini Afrika Kusini katika fursa ya mwezi wa wanawake nchini humo kwa kukumbuka maandamano ya makubwa yaliyofanywa kunako tarehe 9 Agosti 1956,katika jiji la Pretoria kupinga ubaguzi wa rangi.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Inatakiwa kuhamasisha kwa kiasi kikubwa uwepo wa wanawake katika nafasi msingi za Kanisa nchini Afrika Kusini, hata kwa kutoa fursa kwa wanawake kujifunza masomo ya kitaalimungu. Ndiyo matumaini na utashi mkubwa uliooneshwa na Askofu Victor Phalana, askofu wa Klerksdorp katika ujumbe wake kwa njia ya video, kufuatia na fursa ya “Mwezi wa wanawake” unaoendelea nchini humo. Mwezi maalum unaadhimishishwa katika wiki hizi nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kuwakumbuka kwa namna ya pekee zaidi ya vijana 20,000 ambao mnamo tarehe 9 Agosti 1956 katikati ya kipindi kigumu cha ubaguzi wa rangi, waliandamana kwa wingi jijini Pretoria, dhidi ya wajibu wa “hacha hapite kwanza”,  jambo ambalo lilikuwa linawagusa raia weusi kuwapisha wazungu na kwa maana hiyo mwaka huu kumbukumbu hizi zinaongozwa na mada ya  “usawa wa kijinsia na haki sawa kwa wanawake”.

Kanisa nchini Afrika Kusini bado wanatakiwa kufanya kazi kubwa

Hili ni lengo ambalo kwa upande wa Kanisa la Afrika Kusini bado lazima walifanyie kazi kubwa sana kwa kuzingatia hasa nafasi msingi ya maisha ambayo yanatazama huduma ya jumuiya na ya Uklero katika maparokia na mashirika yote ya kikanisa.  Kwa njia hiyo, Askofu Phalana anabainisha kuwa inatakiwa kuwatia moyo wanawake ili waweze kujongelea mafunzo ya juu, kwa namna ya pekee katika nyanja ya kitaalimungu, sheria na mafunzo ya kibiblia. Kwa mujibu wa Askofu wa Klerksdorp, anasema, nchi nyingine za Afrika ziko mbele zaidi katika muktadha huo. “Bado tunayo kazi nyingi ya kufanya na inawezakana  kuwa tumefikia wakati ambapo sasa Kanisa nchini Afrika Kusini lazima kuanzisha ufadhili wa masomo maalum kwa ajili ya wanawake na wasichana ambao wanataka kuendelea na masomo haya ili waweze kuwa rasilimali ya ziada kwa ajili ya Kanisa la Afrika Kusini. Lazima tuhakikishe kuwa wamejumuishwa ndani ya moyo wa Kanisa ili maisha yake ya kiadili, kitaaluma na kichungaji yaweze kufaidika na kutafakariwa kwa mwanadamu katika ukamilifu wake, awe wa kiume na wa kike”, amesisitiza Askofu Phalana.

Bila wanawake majimbo yangekuwa maskini

Askofu Phalana ametaja hata mfano wa jimbo lake mahali ambapo anasema wanawake wengi wanajikita katika shughuli muhimu kama ile ya ukatekisita, utoaji wa huduma wakati wa liturujia na mahali ambapo Baraza la Kichungaji linaongozwa na mwanamke. Pia wanawake ni sehemu muhimu ya Baraza la kijimbo kwa ajili ya Walei na ya mashirika mengine ya ushauri.  “Wakati nikiwa nina ulazima wa kufanya maamuzi muhimu ninashauriana na mihimili hii. Ushauri wetu ni mzuri sana wa kujenga na hutumika kufafanua mwelekeo na maono ya majimbo yetu”, Askofu huyo alithibitisha huku akionesha pongezi kubwa ya majitoleo, ukarimu na sadaka zao za wanawake katika Kanisa. Kwa mujibu wa Askofu Phalana anasisitiza kuwa ujumuishwaji wa wanawake katika nafasi ya uwajibikaji, haidhoofishi utume wa Kanisa na badala yake anasema: “Majimbo yetu yangekuwa maskini bila kuwa na uzoefu wao” na kukumbuisha kuwa miaka kumi ya mwisho hata jiji la Vatican idadi kubwa ya wananawake wamo katika ngazi mbali mbali ambapo wameteuliwa katika mabaraza ya kipapa hata katika vitengo vya  ofisi za Makao makuu ya Kipapa!

21 August 2020, 13:35