Tafuta

Vatican News
2020.07.13-Kanisa la Mtakatifu  Sofia jijini Istanbul kubadilishwa kwa mara nyingine kuwa Msikiti. 2020.07.13-Kanisa la Mtakatifu Sofia jijini Istanbul kubadilishwa kwa mara nyingine kuwa Msikiti. 

Uturuki:maskitiko ya ECC kubadalishwa Kanisa Kuu la Mt.Sofia!

Katika mabadiliko ya namna hiyo yanapunguza bila shaka urithi huu maalum wa jengo ambalo kwa miaka mingi umekuwa ni kama daraja la ulimwengu la kupitia,ambalo linaunganisha Mashariki na Magharibi na ambalo huashiria umoja na amani,maelewano ya pamoja na mshikamano kati ya watu tofauti duniani.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Mabaraza la Makanisa Ulaya wameonesha kusikitishwa kwao, kwa uamuzi nchini Uturuki kubadilika Kanisa Kuu la Mtakatifu Sofia kuwa Msikiti huko Istanbul. Chombo cha Kiekumene ECC kinawakilishwa na Makanisa 114 ya Ulaya ambayo kwa dhati yameonesha kutokubaliana na uamuzi huo katika barua yao waliyoitume kwenye Kamati ya Ulaya na Shirika la Umoja wa Mataifa utamaduni na Elimu Unesco. Kiukweli sehemu hii ni urithi wa Ulimwenguni katika UNESCO na ni makumbusho tangu 1934, lakini uamuzi wa serikali ya Uturuki imefuta hali  hii siku ya Ijumaa iliyopita, kwa mujibu wa barua ya Baraza la Makanisa Ulaya iliyotolewa tarehe 16 Julai 2020.

Jengo la Mtakatifu Sofia lilijengwa 1500

Jengo hilo lilijengwa miaka 1500 iliyopita kama Kanisa kuu la Kikristo la Kiorthodox, na likabadilishwa kuwa msikiti baada ya ushindi wa Ottoman mnamo 1453 na baadaye kubadilishwa tena kuwa jumba la makumbusho na Mustafa Kemal Ataturk. Kwa upande wa Baraza la Kiekumene la Makanisa Ulaya (ECC) kubadilisha Hagia Sophia kuwa msikiti kunaweza kuunda hali halisi isiyokuwa na uvumilivu wa kidini na vurugu. “Katika mabadiliko ya namna hiyo yanapunguza bila shaka urithi huu maalumu wa jengo, kama daraja la ulimwengu la kupitia na ambao linaunganisha Mashariki na Magharibi, na ambalo huashiria umoja na amani, maelewano ya pamoja na mshikamano kati ya watu tofauti”. Patriaki wa Kiekumene Bartholomew, kwamba, “katika karne ya 21, kwa Hagia Sophia ambayo imetolewa kwa 'Hekima Takatifu ya Mungu' na inawaruhusu Wakristo na Waislam kukutana na kushangaa ukuu wake, haina maana kabisa kufanya uamuzi usiofaa na hatari, kwa sababu inaweza kusababisha migongano na migogoro”.

Jumba la Makumbusho la Mtakatifu Sofia libaki namna hiyo

“Kwa roho ya jina la Hagia Sophia, ambayo kiukweli  inamaanisha Hekima Takatifu, tuombe ili kwamba hekima na sababu ziweze kuonekana na Hagia Sophia iweze kutunzwa hali yake ya makumbusho”. Na hatimaye katibu mkuu wa ECC, Jørgen Skov Sørensen, amebainisha kuwa ikiwa uamuzi huo unagusa na kuwa na  athari kubwa kwa Makanisa yanayohusika moja kwa moja, hata hivyo, Makanisa yote ya ECC yanafadhaika na kile tunachoshuhudiwa leo huko Istanbul”.

17 July 2020, 15:20