Tafuta

2019.09.11 Baraza la Makanisa Ulaya (ECC) 2019.09.11 Baraza la Makanisa Ulaya (ECC) 

Ulaya:Baraza la Kiekumene la Ulaya kwa ajili ya haki na amani

Kushuhudia pamoja matumaini ndiyo kauli mbiu iliyochaguliwa na Baraza la Makanisa ya Ulaya kuongoza kipindi cha mwaka 2019/2023.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kwa pamoja kushuhudia matumaini ndiyo neno ambalo limetoka katika Baraza la Kiekuemene la Makanisa ya Ulaya (Cec) walilochagua kwa ajili ya mpango mkakati kwa kipindi cha mwaka 2019/2023. Hili ni neno ambao linaonesha misingi inayoongoza matendo ya kweli ya Baraza la Makanisa Ulaya karibu kwa miaka 60 sasa ya uwepo wake, katika  kujikita kwenye  tafakari ya kina ya mahusiano ya Makanisa; ushirikiano wa kiekumene barani Ulaya; utashi wa kushuhudia Injili katika moyo wa jamii na siyo tu kwa njia ya kuhubiri juu ya Kristo ambaye anapatanisha ulimwengu kwa njia ya matendo yake na haki, lakini pia shukrani kwa uwepo wa neno la Kanisa katika moyo wa miji na katika changamoto za ulimwengu.

Neno la Kanisa katika taasisi  zote za Ulaya na kutafuta mizizi yake

Haya yote yameandikwa katika utangulizi wa Ripoti ya mwaka ya Baraza la Kiekumene la Makanisa Ulaya (Cec) kwa mwaka 2019 yaliyoelezwa na Rais wake, mchungaji Christian Krieger.  Tangu kuanzishwa kwa chombo hiki  kunako mwaka 1959, anakumbusha kwamba Baraza la Makanisa Ulaya hawakuacha kamwe kuhamasisha amani na mapatano katika Ulaya iliyojeruhiwa na kushambuliwa na mizozo mikubwa miwili, lakini pia kiasi kukubwa hicho cha mandeleo ya kina na ya kudumu katika jamii  kwenye karne hii ya 21,  inafanya kwa mara nyingine tena kuwa na ulazima wa  kuwepo na  neno la Kanisa katika taasisi  zote za Ulaya leo hii ili kutafuta kwa upya mizizi yake ya kina; kutafuta neno moja ambalo Baraza la Makanisa Ulaya linapeleka mbele na kutafuta namna ya kusikika sauti kwa mgurumo ulimwengu kote, amebainhsa Mchungaji Krieger.

Jihada za kuhamasisha amani, haki na mapatano Ulaya

Ripoti hiyo pia imegawanyika katika sehemu kuu tatu ambazo ni sambamba na mantiki tatu zilizomo katika mpango mkakati kwa kipindi cha 2019-2023, kama anavyokumbusha Katibu Mkuu wake Jørgen Skov Sørensen, wakati wa mkutano Mkuu kunako mwaka 2018, uliofanyika huko Novi Sad, nchin Serbia. Kwa maana hiyo katika mada hizo ni kuongeza jitihada za kuhamasisha amani, haki na mapatano barani Ulaya; kuongeza misingi ya udugu kiekumene na kuhamasisha utume wa Kanisa: kueneza sauti ya Makanisa barani Ulaya na taasisi mbali mbali za Ulaya. Pamoja na hayo ripoti mpya inaonesha kazi iliyotimizwa kwenye mwaka 2019 ambayo inatazama hata mada nyingine muhimu na za dhati kama vile uhamiaji, haki za binadamu, ilimu ya viumbe na ulinzi wa mazingira.

Wataalimungu na viongozi wa kidini katika mkutano wa ECC uliofanyika Finland

Kati ya matukio msingi ya 2019, ni Baraza kuhusu amani iliyoandaliwa na (ECC) huko Paris. Watoa mada kutoka madhehebu mbali mbaliwa wakristo lakini pia hata katika utamaduni wa kiyahudu, au waisalma walitfakari pamoja juu mada ya kutathimini michakato ya mikataba ya amani iliyotiwa sahini huko Versailles kunako mwaka 1919. Baraza la Kiekumene la Makanisa Ulaya ( ECC) aidha walihamasisha mazungumzo kati ya Makanisa ya kihistoria na Makanisa ya wahamiaji na makabila ya watu wachache. Mada hiyo ilinyambulishwa na wataalimungu na viongozi wa kidini katika mkutanowa ECC uliofanyika huko Finland.

Thamani za pamoja zinaunda wakati ujao na uwezo wa kuunganisha mataifa Ulaya kwa ajili ya amani ya kudumu

Uwepo wa ECC huko Bruxelles na Strasburg, ripoti inasisitiza kuwa unaruhusu Makanisa kujadiliana na Tasisi za Umma  kwa namna ya pekee ya Umoja wa Ulaya na Baraza la Ulaya. Kunako mwaka 2019 katika Sikukuu ya Ulaya iliyofanyika mnano tarehe 9 Mei, wahusika wa ECC mbele ya viongozi wa Ulaya waliokuwa wameunganika katika Mkutano wao mkuu kuhusu “wakati endelevu wa Bara” huko Sibiu, nchini  Romania, walitumia fursa hiyo kutangaza thamani za pamoja ambazo zinaunda wakati ujao wa Ulaya na zenye uwezo wa kuunganisha mataifa ya Ulaya kwa ajili ya amani ya kudumu.

Toleo la sita la kiangazi la chuo kikuu kuhusu haki za binadamu

Toleo la sita la Chuo Kikuu katika majira ya joto juu ya haki za binadamu, lililofanyika huko Lisbon, lilizungumzia suala la uhuru wa kujieleza katika kipindi hiki cha kinachoongezeka watu. Zaidi ya washiriki 60 kutoka mataifa tofauti, makabila madogo na dini waligundua kwa pamoja njia tofauti za kutetea uhuru wa kujieleza na kupinga hotuba yenye chuki na uhalifu wa kuchukia, kwa namna ya pekee katika mazingira ya kidini. Masuala ya watu na haki za binadamu yalikuwa mada ya mkutano huo wa (ECC)ulioandaliwa huko Malaga nchini Uhispania.

Mchango wa makanisa kwa jamii endelevu.Nini kifanyike na tufanyeje?

Katika Ripoti hiyo aidha inataja mkutano mwingine  uliokuwa na mada juu ya  “Mchango wa makanisa kwa jamii endelevu. Katika kukata tamaa na tumaini, ni nini kifanyike na tunafanyaje?”, ulioandaliwa kuanzia tarehe 25 hadi 28 Mei huko Oslo na Kanisa la Norway kwa kushirikiana na Mtandao wa Kikristo wa Ulaya kwa ajili ya Mazingira (Ecen). Hatimaye  katika mwaka huo, Tume ya Makanisa kwa ajili ya Wahamiaji wa Ulaya (Ceme) imeendelea kuunga mkono nguvu za ulinzi wa wakimbizi, hasa kwa kutoa maoni yao kuhusu Mwongozo wa Tume ya Ulaya  ya kuwarudishi hao wakimbizi makwao.

17 July 2020, 17:39