Tafuta

Vatican News
Waamini nchini Pwani ya Pembe mbele ya sanamu ya Bikira Maria wakisali. Waamini nchini Pwani ya Pembe mbele ya sanamu ya Bikira Maria wakisali.  (AFP or licensors)

Pwani ya Pembe:Baraza la Maaskofu kujikita na mada ya mgogoro wa kiafya,kijamii na kisiasa!

Huu ni mkutano maalum kwa ajili ya uchanguzi maaskofu ambapo watachagua Rais wa Baraza la Maaskofu nchini humo na kuendeleze hata kwa uchaguzi wa Rais wa Tume ya maaskofu ikiwa lazim na Sekretrietu ya utendaji wa Tume ya Maaskofu.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican

Mgogoro wa kiafya unaondelea, na changamoto zake za kiroho, kichungaji, kiuchumi, kijamii na kisiasa, ndiyo mada iliyojikita katika Mkutano wa 116 wa Baraza la Maaskofu wa Katoliki wa Pwani ya Pembe, iliofunguliwa tarehe 26 Julai 2020 katika kituo cha Yamoussoukro, hadi tarehe 31 Julai 2020.

Mkutano huo ulikuwa umepangwa kufanyika mwezi Mei katika jimbo la Yopougon lakini kwa sababu ya janga la Covid-19, uliahirishwa. Huu ni mkusanyiko maalum kwa ajili ya uchanguzi maaskofu ambapo watachagua Rais wa Baraza la Maaskofu nchini humo na kuendeleze hata kwa uchaguzi wa Rais wa Tume ya maaskofu  ikiwa lazima na Sekretarieti ya utendaji wa Tume ya Maaskofu.

Wakati wa Mkutano huo watasikiliza pia ripoti ya Rais mstaafu wa Baraza la Maaskofu na hata ripoti nyingine za tume ya maaskofu na pia masuala mengine ambayo wayaweza kuwenye mjadala wa kuunda Taasi ya Elimu, na tathimini ya hali halisi ya kiafya, kijamii na kisiasa nchini humo.

Wakati huo huo kuhusu uchaguzi Mkuu wa rais unaotazamia 2020, Kanisa katoliki na jumuiya za kidini zinaalikwa kutoa mchango mkubwa wa kitaifa wakati huo mivutano ya kisiasa  haioneshi kupungua. Maaskofu daima wamezidi kuhamasisha amani, mapatano na maelewano ya kijamii.

29 July 2020, 14:07