Tafuta

Vatican News
2018-06-16 Gniezno, Poland 2018-06-16 Gniezno, Poland 

Poland:Ask.Mkuu Gądecki-Umoja wa Ulaya haupo hadi kuwepo roho moja ya kijumuiya!

Baada ya kuanguka kwa ukuta unaoonekana wa Berlin sasa ukuta usioonekana na ambao unagawanya bara la Ulaya uko wazi.Ni ukuta ambao unapitia ndani ya mioyo ya binadamu.Ni wa hisia na ambao umetengenezwa na wasiwasi na uchokozi.Umejengwa ndani ya ubinafsi wa kisiasa,kiuchumi na ni hisia dhaifu juu ya thamani ya maisha ya mwanadamu na juu ya hadhi ya kila mwanadamu.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Inabidi kurudia kuamini kutoka kwa Mababa waanzilishi wa Umoja wa Ulaya ambao walikuwa wanataka kuwa wakati ujao uwe na msingi juu ya uwezo wa kufanya kazi kwa pamoja ili kushida migawanyiko na kuhamasisha amani na umoja kati ya watu wa bara hili. Katika kitovu cha mpango huo wa kisiasa, kulikuwa na imani katika mtu na si tu kama mzalendo au kitovu  cha kiuchumi, lakini kama mtu mwenye kuwa na hadhi itokanayo na muumba. Ndivyo anathibitisha Askofu Mkuu Stanisław Gądecki, Rais wa Baraza la Maaskofu nchini Poland (Cep), katika hotuba yake tarehe 18 Julai 2020 kwenye Mkutano wa nne wa kimataifa wa Vyama vya Kikristo Ulaya na Ulimwenguni (Europa Christi - Mundus Christi) uliohitimishwa Jumapili 19 Julai 2020 katika Monasteri ya Wigry.

Askofu Mkuu amesema “Baada ya kuanguka kwa Ukuta unaoonekana wa Berlin sasa ukuta usioonekana na ambao unagawanya bara letu bado unaooneka wazi. Ni ukuta ambao unapitia ndani ya mioyo ya binadamu. ukuta huo ni wa hisia na ukuta huo umetengenezwa na wasiwasi na uchokozi (...)”. Umejengwa  ndani ya  ubinafsi wa kisiasa na kiuchumi na ni hisia dhaifu juu ya thamani ya maisha ya mwanadamu na juu ya hadhi ya kila mwanadamu , amebainisha Askofu Gądecki na ambaye anaona wazi wazo kwa mara nyingine tena, kwamba Ulaya imegawanywa kwenye “Mfuko wa Kuokoa”, ambao ni mfuko wa  kuweza kusaidia mara baada ya Covid-19.  Kwa maana hiyo amesisitiza kwamba “Bado kuna njia ndefu ya kufikia  kuungana kiukweli katika bara la Ulaya”.

Hakutakuwa na umoja Ulaya hadi iwe jamuiya  moja ya kiroho, ameongeza kusema rais wa Baraza la Maaskofu nchini Poland (Cep), aliyenukuliwa na shirika la habari Katoliki la Kai, huku  akikumbuka maneno yaliyosemwa na Mtakatifu Yohane  Paulo II huko Gniezno wakati wa ziara yake ya kitume nchini  Poland mnamo 1997, ambapo Papa Kipoland alisisitizia ukosefu wa  uwezekano wa kujenga umoja wa kudumu ikiwa watakata mizizi ya Kikristo ambayo mataifa na tamaduni za Ulaya zimekulia.

Akikumbuka juu ya  mafundisho ya Papa Francisko na Papa Mstaafu Benedikto XVI katika hotuba yake, Askofu Mkuu wa Poznań, amesisitizia hata nafasi msingi ya familia katika mchakato wa kuunganisha Ulaya. Familia ya umoja, yenye rutuba na isiyotengenishwa  huleta pamoja mambo msingi ya kuweza kutoa matumaini kwa siku zijazo. Bila uthabiti huu, ina maana ya kujenga kwenye mchanga na matokeo yake ni athari kubwa za kijamii. Kwa upande mwingine, amesisitiza, umuhimu wa familia na siyo kusaidia kutoa mtazamo na matumaini kwa vizazi vipya tu, lakini pia kwa  watu wengi wazee, ambao mara nyingi hulazimika kuishi katika hali za upweke na kuachwa, peke yao”, amesema Askofu Mkuu Gądecki.

20 July 2020, 12:49