Tafuta

Vatican News
2020.01.27 Askofu Mkuu Kaigama wa  Abuja, Nigeria 2020.01.27 Askofu Mkuu Kaigama wa Abuja, Nigeria 

Nigeria:Wakristo na waislamu waungana kusali pamoja

Upendo kwa jirani pasipo kujali kabila au dini ni jambo ambalo Askofu Kaigama amesisitiza na kwamba maumivu na changamoto za Covid-19 zinaweza kufundisha jambo katika maana hiyo.Amewasihi kusali bila kusahau jirani kwani kutokukaribiana katika kipindi cha Covid-19 haimaanishi kuacha kufanya jambo nzuri kwa jirani aliye karibu yako.Amesema hayo katika Kituo cha kitaifa cha Kikristo huko Abuja,Nigeria.

Na Sr. Angela Rwezula- Vatican

Waumini wa dini kuu mbili za Nigeria wanapaswa kupanga mipango chanya mara nyingi zaidi na kutafuta maeneo ambayo wanaweza kufanya kazi kwa pamoja ili kukuza maelewano, maendeleo na utulivu wa amani. Haya yote na mengine yamezungumza katika Kituo cha Kitaifa cha Kikristo cha Abuja na Askofu Mkuu Ignatius Ayau Kaigama wa jimbo kuu katoliki Abuja, ambapo amesisitiza  umuhimu wa mpango huo hususani katika kipindi hiki ambapo kumekuwa na ongezeko la mvutano na tishio la ugaidi wa jihadi la Boko Haram. Dominika tarehe 5 Juni 2020,  Wakristo na waislamu wa Nigeria waliungana pamoja ili kuomba Mungu aweze kusitisha janga la covid-19 na hata kuwaombea wagonjwa na pia roho za marehemu wapumzike kwa amani ambao ni waathirika wa virusi vya corona. Tukio hili liliandaliwa na Baraza la Kidini la Nigeria (Nirec kwa ushirikiano na Shirikisho wa Wakristo wa Nigeria Can, kama inavyooneshwa katika Tovuti ya Recowa-Cerao.

Sala na upendo kwa jirani

Upendo kwa jirani “pasipo kujali kabila au dini” ni jambo ambalo Askofu Kaigama amesisitiza kuwa “maumivu na changamoto za Covid-19 zinaweza kutufundisha jambo katika maana hii”. Kwa maana hiyo  amewasihi kusali bila kusahau jirani. “Kutokukaribiana katika kipindi hiki cha Covid-19” haimaanishi kuacha kufanya jambo nzuri kwa jirani aliye karibu yako. Kwa mujibu wa kipengele hicho cha kusali, amesisitiza kuwa inabidi kuwa na mahusiano na Mungu pasipo unafiki, kwa kukumbuka kuwa inabidi tumkimbilie Mungu sio tu kipindi cha hatari.

Uhusiano na Mungu ni muhimu bila kusubiri majibu

Aidha Askofu Mkuu Kaigama amesisitiza kwamba, katika sala, inabidi kuwa na mahusiano na Mungu kila siku bila kutegemea majibu ya haraka au miujiza bali kumwamini Yeye. “kama waamini tunaweza kujifunza kutoka katika janga hili la kidunia juu ya maisha ya pamoja kama binadamu, juu ya udhaifu wa maisha yetu na kutafuta kile tu ambacho ni muhimu na cha lazima”.

Yesu anaomba tusali mara kwa mara

Katika kuhitimisha kitu cha kuzingatia nje ya dharura yoyote nAskofu Mkuu amesema kwamba: “Yesu anatuomba tusali mara kwa mara”. Sisi ni watu tunaoamini kuwa, sala, mafungo na upendo ni sehemu ya jibu kwa janga hili la kidunia: siyo kitu kidogo kulinganisha na kazi wanayoifanya wale ambao wapo mstari wa mbele katika kutoa huduma ya kiafya au kutafuta chanjo au matibabu.

07 July 2020, 16:13