Vatican News
Damu Azizi Takatifu ya Yesu inatusaidia kuishi katika imani thabiti ya kikristo na inatujenga katika mitazamo sahihi ya kikristo kadiri ya mafundisho ya Yesu mwenyewe. Damu Azizi Takatifu ya Yesu inatusaidia kuishi katika imani thabiti ya kikristo na inatujenga katika mitazamo sahihi ya kikristo kadiri ya mafundisho ya Yesu mwenyewe. 

Nchi Takatifu:maadhimisho ya Misa katika Kanisa kuu la Getsemani

Katika kilele cha Siku kuu ya Damu Azizi ya Yesu Kristo,Ibada ya misa imeadhimishwa katika Kanisa kuu ya Mateso ya Yesu Kristo.Damu Azizi Takatifu ya Yesu inatusaidia kuishi katika imani thabiti ya Kikristo na inatujenga katika mitazamo sahihi ya Kikristo kadiri ya mafundisho ya Yesu mwenyewe.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Damu Azizi ya Kristo ni zawadi inayomwilisha maisha yetu hapa duniani na kutufanya tuwe na uwezo wa kufuata nyayo za Yesu. Ndiyo alivyosisitiza Msimamizi wa Nchi Takatifu Padre Francesco Patton, ambaye tarehe Mosi Julai huko Yerusalem ameongoza Ibada ya Misa Takatifu katika Kanisa kuu la Mateso kwenye bustani ya Getsemani, katika kilele cha Siku Kuu ya Damu Azizi ya Yesu Kristo. Damu yake ambayo Yesu alitoa kwa mara moja daima ni zawadi ambayo inaendelea kutolewa kwetu sisi, amefafanua Padre Patton ambaye ni ndugu Mdogo wa Kifransiskani.

Damu ya Kristo inatusindikiza maisha yote

Damu ni zawadi ambayo sisi mara zote tunaalikwa kuikaribisha na kuipokea (...); inasindikiza maisha yote ya kikristo na siyo tu katika maadhimisho ya ekaristi, amefafanua Msimamizi huyo.  Liturujia hiyo ya Misa ilifunguliwa kiutamaduni kwa kuweka mawaridi mekundu juu ya jiwe au mwamba uliolala chini ya Kanisa Kuu, ikiwa na maana ya kukumbusha uchungu na damu iliyomwagika ya Yesu siku ya Alhamisi Kuu katika mwamba huo huo. Katika mahubiri ya Padre Patton ameendelea kusisitiza kuwa damu ya Yesu na  maisha yake yaliyotolewa ndivyo binavyobadili maisha yetu, ni kile ambacho kinatimilizika kiukweli na utimilifu  wa uhuru wa kila mmoja wetu na katika ubinadamu wetu wote!

Miito ya Kanisa inabubujika kutoka katika damu ya Yesu

Damu Azizi ya Yesu ni mahali ambamo miito mbali mbali ya Kanisa inaweza kuishi tu kiwa inamwilisha daima katika zawadi hiyo yapekee ambayo Yesu aliifanya na ambayo inajionesha katika zawadi ya damu yake. Kwa maana hiyo ni vema kufanya kumbu kumbu, kuadhimisha na kupokea, maneno matatu msingi ambayo yalimwongoza Padre Patton katika kutafakari Injili. Kuadhimisha ni tendo ambalo linafanya kumbukumbu iwe ya sasa na inachukua nafasi ya kazi ambayo inaruhusu waamini kuwapo katika karamu ile ya mwisho ya Pasaka, sadaka ya msalabani na ufufuo. Na kupokea ni tendo ambalo linakumbusha wakati ule wa kuweka wakfu,  siku hiyo Yesu aliposema “ twaeni mle wote na mnyweni nyote". Kwa hakika Damu Azizi Takatifu ya Yesu inatusaidia kuishi katika imani thabiti ya Kikristo na inatujenga katika mitazamo sahihi ya Kikristo kadiri ya mafundisho ya Yesu mwenyewe.

Kupokea zawadi hiyo ni kuwa tayri kujitoa kwa wengine 

Leo hii tufanye kumbu kumbu, tuadhimishe na kupokea kwa imani, Damu Azizi ya Bwana wetu Yesu Kristo,. Kwa kuhitimisha Padre Patton amesema kupokea zawadi hii ina maana lakini kuwa tayari kuwa zawadi ya maisha na kupokea damu ya Kristo kama matokeo kwetu  sisi katika  kumwaga damu wakati wa  kutoa upendo kwa ajili ya wengine. Baada ya maadhimisho hayo kama utamaduni, watawa na waamini wachache waliokuwa Kanisani wamekusanya mawaridi kutoka katika  mwamba wa uchungu  ili kupeleka nyumbani kama ishara ya kwenda na maadhimisho ya siku hii.

Maadhimisho hayo yaliwekwa na Papa Pio X

Maadhimisho haya ambayo kwa mujibu wa utamaduni wa zamani kabla ya mataguso yalianzishwa kunako Mosi Julai 1849 na Papa Pius X, baada ya kuwa na mazoea ya ibada kuu ya waamini katoliki duniani kote. Na katika mabadiliko ya muundo wa kalenda ya kiliturujia ya 1970, siku kuu hii ilibadilishwa kuwa Siku kuu ya 'Corpus Domini', yaani 'Mwili na Damu ya Yesu' katika kalenda zote, isipokuwa ya ‘Hierosolymita’ yaani tawi la shirika la kijeshi la kizamani la kidini la Mtakatifu Yohane Mbatizaji huko Yerusalem,  lililoanzishwa  katika  kipindi cha machafuko yaliyozinduliwa na Kanisa Katoliki kwa ajili ya  kukomboa Kaburi Takatifu kutoka udhibiti wa Uislamu na ambayo hadi sasa inahifadhi ibada ambayo inahusika sana na mahali pa uchungu na mateso ya Yesu.

 

02 July 2020, 13:51