24 Novemba 2019 kutoa heshima kwa waathirika wa bomu la atomiki Nagasaki 24 Novemba 2019 kutoa heshima kwa waathirika wa bomu la atomiki Nagasaki 

Marekani:Siku ya maombi iliyoandaliwa na maaskofu katika maadhimisho ya miaka 75 ya bomu la atomiki

Katika fursa ya madhimisho ya miaka 75 tangu kulipuka kwa mabomu ya nyuklia ya Hiroshima na Nagasaki huko Japan,Maaskofu wa Marekani wanawaalika wakristo na watu wenye mapenzi mema kusali tarehe 6 na 9 Agosti na kuomba ili kusitishwa kwa silaha za kinyuklia na kwa ajili ya amani.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican

Katika fursa ya maadhimisho ya miaka 75 tangu kulipuka mabomu ya nyuklia ya Hiroshima na Nagasaki, mnamo tarehe 6 na 9 Agosti, maaskofu wa Marekani wanawaalika Wakatoliki wote na watu wote wenye mapenzi mema kushiriki, Jumapili tarehe 9 Agosti 2020, katika siku maalum ya maombi, tafakari na kujikita katika kuchukua hatua dhidi ya kusitishwa kwa silaha za kinyuklia. Siku hiyo itaadhimishwa sambamba na Siku kumi za Maombi kwa ajili ya Amani. Ni tukio la kila mwaka lilioanzishwa na Kanisa huko Japan tangu mwezi 1981.  Karne ya XXI inaendelea kushuhudia mzozo wa kijiografia na watendaji wa serikali na wasio wa serikali wakitumia silaha za kisasa na mmomonyoko wa mfumo wa kisheria wa kimataifa juu ya udhibiti wa silaha, wanaandika katika barua kutoka Tume ya Kimataifa ya Haki na Amani ya Baraza la Maaskofu wa Marekani (Usccb).

Wito wa Papa dhidi ya utumiaji na silaha za nyuklia

Maaskofu wa Marekani kwa mara nyingine tena wanasisitiza wito wao kuhusu shinikizo dhidi ya kuongezeka kwa nyuklia, kwa maneno mazito yaliyosemwa na Papa Francisko huko Nagasaki na Hiroshima wakati wa ziara yake ya kitume ya Japan kunako tarehe 24 Novemba 2019. Nafasi hiyo iliwekwa wazi tena mwezi Februari na Tume hiyo hiyo ya Baraza la Maaskofu wa Marekani ambayo ilizindua tena wito wa Papa dhidi ya utumiaji na silaha za nyuklia. Jukumu hili la uwajibika, walikuwa wamesisitiza Tume ya Haki na Amani, kuwa inatoa uzito wa dhamiri kwa mataifa ambayo yana silaha za atomiki, kama vile Marekani ambayo lazima zichukue hatua ya kupunguza,na mataifa yale ambayo hayana  na ambayo lazima yaachane na jaribio la kutaka  kuipata ili kifungu VI cha Mkataba usio na Nyuklia uwe ndiyo chombo bora cha kuondoa kabisa.

Miaka kumbukizi la miaka 75 ya kulipuka kwa bomu la atomiki

Japan inajiandaa kukumbuka miaka 75 tangu bomu la kwanza la kinyuklia kudondoshwa Hiroshima, kisa kilichoilazimisha Japan kusalimu amri na kumalizika vita vikuu vya pili vya Dunia. Katika Hospitali nchini Japan bado mpaka leo hii zinawatibu maelfu ya wahanga walionusurika na shambulio la bomu hilo la nyuklia. Tarehe 9 Agosti bomu jengine la nyuklia huko  lilidondoshwa karibu na mji wa bandari wa Nagasaki, watu 70 elfu waliuawa. Mashambulio hayo mawili ya mabomu ya nyuklia ndiyo ilikuwa chanzo cha kusalim amri Japan tarehe 15 Agosti 1945 na kumalizika vita vikuu vya pili vya dunia.

Papa aliomba kuacha kabisa sihala za atomiki

Papa Francisko alipotembelea nchi hiyo aliitaka dunia kuachana kabisa na silaha za atomiki wakati wa  hotuba yake mjini Nagasaki Japan, mji  ulioshambuliwa kwa mabomu ya nyuklia mwishoni mwa vita vikuu vya pili vya dunia ambayo haitasahulika kamwe! Katika hotuba yake aidha Papa Francisko akiwa katika eneo la uwanja wa kumbukumbu ya  mabomu ya  atomiki mjini Nagasaki huku  mvua ikinyesha alisema: “Eneo  hili linatufanya kutambua maumivu na maovu ambayo sisi binadamu tunaweza kufanyiana”. Kabla ya hotuba yake, Papa Francisko alitoa heshima zake kwa wahanga wa shambulio la Marekani la  bomu la kinyuklia mwaka 1945 katika mji huo wa kusini magharibi  nchini  Japan, na kuwauwa  watu wapatao 74,000, ikiwa ni  pamoja  na maelfu ya  wakatoliki.

Kuwa na silaha za maangamzi siyo  suluhisho

Akiendelea na hotuba yake  alisema: “Hapa katika mji huu ambao ulishuhudia kwa hakika tukio la maafa ya kibinadamu na mazingira kutokana  na  shambulio la nyuklia, juhudi zetu kuzungumzia dhidi  ya mashindano ya silaha hazitatosha. Moja kati ya kile ambacho moyo wa binadamu unachopenda zaidi ni usalama, amani na uthabiti. Kuwa na silaha za nyuklia na silaha nyingine za maangamizi siyo jibu la hisia hizi katika moyo wa binadamu unavyopenda, kiukweli kila mara binadamu anajaribu kuzuwia hilo”. Amani na uthabiti wa kimataifa hayalingani  na  majaribio  ya kujenga juu  ya hofu ya uharibifu  wa  pamoja  ama  kitisho cha maangamizi ya  jumla alisema  Papa Francisko. “Nikiwa naamini kuwa dunia bila silaha za kinyuklia inawezekana na ni muhimu, nawataka viongozi wa kisiasa kutosahau kuwa silaha hizi haziwezi kutulinda kutokana na kitisho cha hivi sasa katika  usalama  wa  kitaifa na  kimataifa. Tunahitaji kutafakari athari  ya  maafa ya uwepo wake, hususan kutokana na mtazamo  wa  kiutu na mazingira, za  na  kukataa kuongeza  hofu  ya  kimazingira, kutokuaminiana na  uhasama unaochochewa  na  nadharia  za  nyuklia.”

Bado wanahakati wa kupinga silaha za kinyuklia wanaendelea

Papa alifanya mkutano Hiroshima kwa ajili ya amani pia akakutana  na wahanga  wa tetemeko  la  ardhi  la mwaka  2011, tsunami na  maafa  ya  nyuklia  kaskazini  mashariki mwa  Japan. Ziara yake  ilikuwa  ya  kwanza kufanywa  na  Papa  nchini  Japan baada ya  muda  wa  miaka  38. Mwaka 1981, Papa John Paulo II alikwenda Hiroshima, Nagasaki na Tokyo. Papa Francisko alikuwa  miongoni mwa  watu  wa kwanza  kutia  saini  na  kuidhinisha  mkataba wa kuzuwia  silaha za  kinyuklia, ambao  uliidhinishwa na mataifa 122 mwezi  Julai 2017.  Mkataba huo hata hivyo bado haujaanza kutumika kwa kuwa haujaidhinishwa na mataifa 50 ambayo  yanatakiwa  kutia saini. Wanaharakati wa kupinga silaha  za  kinyuklia  bado wanaendelea kuitaka  Japan, ambayo ni nchi pekee iliyoathirika  na  mashambulizi ya  silaha  za atomiki, kutia  saini na kuidhinisha  mkataba  huo  haraka iwezekanavyo.  Shambulio la mji wa Nagasaki tarehe 9 Agosti 1945, lilikuja siku tatu baada  ya  shambulio  la  kwanza  la  bomu   la  atomiki lililodondoshwa na ndege  ya mashambulizi  ya  B-29 ya Marekani na kuripuliwa katika mji wa Hiroshima na kusababisha watu 140,000 kuuwawa.

14 July 2020, 15:00