Tafuta

2020.05.07 Dada wadodo mbele ya Mahakama kuu Marakani 2020.05.07 Dada wadodo mbele ya Mahakama kuu Marakani  

Marekani:Maaskofu wapongeza mahakama kuu.Ni ushindi wa uhuru wa kidini!

Maaskofu nchini Marekani wapongeza uamuzi wa Mahakama Kuu ya Marekani kwa kwa niaba ya Shirika la Dada Wadogo wa Maskini na mashule mengine mawili katoliki katika mzozo wa muda mrefu juu ya agizo la uzazi wa mpango na uhuru wa dhamiri.Ni ushindi mara mbili wa uhuru wa kidini huko Marekani wanasema Maaskofu.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Mahakama Kuu inakubaliana hoja ya Shirila la Dada Wadogo wa Maskini na shule mbili Katoliki. Kufuatia na hili Maaskofu wanabainisha kuwa ni ushindi muhimu katika uhuru wa kidini na dhamiri. Katika hukumu mbili tofauti, Mahakama Kuu imekubali sababu za Shirika la watawa wa kike na shule mbili Katoliki ambazo zilikuwa zimekata rufaa na kwa wote walikuwa wanatafuta kutambuliwa haki ya kukataa dhamiri katika matumizi ya Sheria ya Utunzaji Nafuu ambayo ni (mageuzi ya afya yaliyotangulia katika Utawala wa Obama ijulikanayo kama Obamacare) na kuheshimu uhuru wa kufundisha katika shule za kidini. Hata hivyo hukumu ya kwanza imekubali sababu ya Shirika la Dada Wadogo wa Maskini, ambao husaidia wazee maskini. Watawa hawa walikuwa wamekata rufaa dhidi ya vifungu vya Obamacare ambavyo vilikuwa vinatoa jukumu hilo, pia kwa taasisi za dini ambazo siyo za ibada, katika kufunika mipango ya bima ya wafanyakazi wao hata katika huduma za utoaji mimba na uzazi wa mpango, chini ya adhabu nzito. Shirika la Dada Wadogo wa Maskini tayari lilikuwa limeshinda ushindi muhimu mnamo 2014, wakati Mahakama Kuu yenyewe ilitambua haki ya kusamehewa kwa suala hili.

Uhuru wa taasisi za elimu za dini kuchagua wafanyakazi 

Dada Wadogo wa Maskini walitoa rufaa ya pili, wakati huu dhidi ya maelewano yaliyoafikiwa na Serikali ambayo ilitoa fursa kwa mashirika ya kidini kukataa bima ya uzazi wa mpango na kinachojulikana kama “kuchagua”, wakati bado wanaruhusu wafanyakazi ambao wanachagua huduma hizi kurudishiwa na serikali. Kwa mujibu wa Dada Wadogo wa Maskini, ahadi hizo bado zilifanya kuwa kweli za kutoa uzazi wa mpango, ambao ni kinyume na kanuni zao za kidini. Uamuzi wa pili uliotamkwa na Mahakama Kuu unahusu uhuru wa taasisi za elimu za dini  kuchagua wafanyakazi wao kulingana na kanuni zao za kidini na kwa maana hiyo bila kuingiliwa kutoka kwa viongozi wa serikali. Katika kesi hiyo, mahakama inatoa mfano wa mwisho wa mfumo wa mahakama ya shirikisho na kutoa uamuzi wa sababu ya shule ya Mama yetu wa Guadalupe na Shule ya Mtakatifu James.

Hatua muhimu mbele ya uhuru wa kidini

Maaskofu wa Marekani kwa hakika wamekuwa na furaha kubwa, ambao wanasema ni hatua muhimu mbele kwa uhuru wa kidini na dhamiri nchini. Matamshi hayo yametiwa saini ya kwanza na Askofu Thomas G. Wenski, Rais wa Tume ya uhuru wa kidini ya Baraza la Maaskofu, Marekani na  Askofu Joseph F. Naumann,  Rais wa Shughuli za maisha ya Baraza la Maaskofu  (Usccb), na ya pili Askofu mwenyewe, Wenki na Askofu Mi Michael C. Barber, S.J. wa Oakland,  Rais wa Tume ya Elimu Katoliki ya Baraza la Maaskofu Marekani Usccb. Kwa mujibu wa  maaskofu, madai ya muda mrefu ya kisheria ya Masista Wadogo wa Maskini, kama ilivyo katika kesi nyingine zinazofanana, yangeweza kuepukwa kwa kuwaachilia mbali wote wanaokataa dhamiri kutokana na dhamana ya bima  kwa uzazi wa mpango. Uzazi wa mpango sio huduma ya kiafya na serikali haina haki ya kulazimisha agizo la kidini kushirikiana na uovu, wanasisitiza kwa nguvu katika taarifa hiyo, wakionyesha matumaini kwamba hukumu hiyo inafunga kabisa kesi hii ya ubaguzi wa serikali dhidi ya watu wa imani na kuwakaribisha kwa hali yoyote kuwa na uangalifu kwa siku zijazo.

Mahakama kuu kutambua usahihi 

Sauti ya maaskofu sawa na hiyo inatazama  juu ya  hukumu inayohusiana na shule hizo mbili za Katoliki. Maaskofu wamesema “Elimu ni sehemu kuu ya utume wa Kanisa. Ni moja ya kazi za roho ya huruma, wanakumbusha katika tamko hilo. Shule za Mama yetu wa Guadalupe na Mtakatifu James zina haki, inayotambuliwa na Katiba, ya kuchagua wafanyakazi wanaofanya huduma hii ya Kanisa na Serikali haina mamlaka ya kuingilia maamuzi ambayo yanahusu wizara hii. Kwa kuhitimisha maaskofu wanaandika kuwa “Uamuzi wa Mahakama Kuu umetambua kwa usahihi kikomo hiki kwa mamlaka ya serikali”.

10 July 2020, 09:31