Tafuta

Umaskini wa kijamii Umaskini wa kijamii 

Makanisa ya Kikristo:uundwe mfuko wa fedha ulimwenguni ili kuondokana na mgogoro!

Makanisani ya kikristo kwa pamoja wametoa wito wa kubadilisha mfumo wa sasa wa fedha ulimwengu na kuhamasisha zaidi katika kipindi baada ya Covid-19,ambacho kinahitaji mfumo mpya wa kiuchumi ambao uwe na usawa na endelevu.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Baraza la Makanisa Ulimwenguni(WCC), la mageuzi ya makanisa (Wcrc), shirikisho la Kilutheri ulimwenguni(Flm)na Baraza kwa ajili ya utume ulimwenguni (Cwm), kwa pamoja wametoa  wito ili kutafuta namna ya  kubadilisha mfumo kwa kina wa sasa wa  fedha ulimwengu na katika kuhamasisha  kufuta madeni katika kipindi baada ya Covid-19, ambacho kinahitaji  mwamko mpya  wa kiuchumi na ambao uwe na usawa na endelevu. Katika barua ya pamoja ya mihimili hii ambayo inawakilisha karibu waamini wakristo milioni 500 ulimwenguni, wanaonesha wasiwasi mkubwa kufuatia na mkutadha wa madhara ya kiafya yaliyosababishwa na covid-19 na kiuchumi, vitu ambavyo kwa hakika vinaendelea kufuta maisha ya wanadamu kila mahali, lakini pia kuhatarisha maisha ya mamilioni ya watu. Kwa mjibu wa waraka huu, wito wa nguvu kuhusiana na kufutwa kwa deni la nchi maskini umetolewa tarehe 13 Julai  2020 kwa viongozi wa mataifa makubwa au  G-20, kwa Benki ya Dunia, Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) na wadau binafsi pia na maaskofu wa Uingereza katika barua yao ya wazi iliyosainiwa pamoja  viongozi wa kidini wa Uingereza na kuchapishwa kwenye tovuti na wa Maaskofu wa Uingereza na Wales (Cbcew).

Hadi leo watu nusu milioni wamekufa,ukosefu ajira,madeni na umaskini

Hadi leo kuna vifo  nusu milioni, ukosefu wa ajira mkubwa, kuongezeka kwa madeni, ukosefu wa usawa kwa maskini katika sehemu nyingi za ulimwengu  na wakati maambukizi ndiyo kumeongezea zaidi kuenea, barua hiyo inafafanua. “Wakati huu unatupatia fursa isiyokuwa ya kawaida ya kuchambua utaratibu wa sasa wa ulimwengu na kujenga tena mfumo tofauti unaounga mkono afya, ustawi na utulivu wa jamuiya na sayari kwa vizazi vijavyo”; aidha wanahimiza Makanisa ya Kikristo kwamba “hatua na sera za kuanza tena baada ya Covid-19 ni  lazima zifanane na hatua kabambe za dharura na dhidi ya shida ya tabianchi”.

Mabadiliko yanawezekana kuwa endelevu

Kwa mujibu wa viongozi wa Kikristo wanabainisha kuwa ili mabadiliko haya yawezewezekane na yawe endelevu inahijia majadiliano ya lazima pia yachukue hatua madhubuti chini ya malengo ya Umoja wa Mataifa, ambapo kuna ushiriki mkubwa wa nchi na asasi za kiraia. Kusudi lazima liwe la kugawa rasilimali za kutosha za kifedha kwa afya ya umma na kinga ya uma  kwa mamia ya mamilioni ya watu ambao maisha yao yamepunguzwa sana na janga hilo na hatua zinazohusiana na kukabiliana nalo. Kwa muda mfupi, inamaanisha katika nchi ni katika  kutoa vifaa vya kinga, chanjo ya afya kwa wote, na chanjo itakayopatikana, fedha za  uhakika ya mapato ya chini, fedha za ukosefu wa ajira na msaada kwa biashara ndogo ndogo.

Lazima kufuta madeni ya nje ya nchi zenye kipato cha chini

Zaidi ya yote, kwa mujibu wa  Makanisa ya Kikristo, wanasema kuwa  inahitajika kufuta madeni ya nje ya nchi zenye  kipato cha chini, ambazo tayari zilikuwa zimegubikwa nayo hata  kabla ya mgogoro wa kiafya. Hii itaruhusu serikali kufungua rasilimali wanayohitaji ili kukabiliana na ugonjwa huu kwa ufanisi na hivyo kuweza kuwafanya kuwa  uvumilivu wa jamuiya.  Aidha inahitajika kuruhusu kuanza tena misingi mpya ambayo ni muhimu na ulazima hata wa marekebisho ya mfumo wa ushuru wa ulimwengu.

15 July 2020, 10:14