2019.07.23 Maaskofu wa Shirikisho la Mabaraza ya Afrika na Madagascar, Secam. 2019.07.23 Maaskofu wa Shirikisho la Mabaraza ya Afrika na Madagascar, Secam. 

Kanisa la Afrika kuadhimisha Siku ya Secam tarehe 2 Agosti!

Siku ya Secam inataka iwe fursa kwa ajili ya wakatoliki wa Afrika ili wajue shirikisho hili na utume wake kwa Kanisa mahalia na la ulimwengu ambayo ilianzishwa kunako mwaka 2014.Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Afrika na Madagascar ilifanya jubilei ya dhahabu kunako mwaka 2019.

Na Sr. Angela Rwezaula;-Vatican.

Dominika tarehe 2 Agosti ni Siku ya Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Afrika na Madagascar Secam iliyotangazwa mnano mwaka 2014, wakati wa fursa ya miaka 45 tangu kuanzishwa kwa chombo hiki ambacho kinaleta pamoja Mabaraza ya maaskofu kitaifa  37, na mabaraza 8 ya kanda za Afrika. Siku hiyo uadhimishwa kila tarehe 29 Julai au ikiwa haiendani na Dominika iliyo karibu sana na basi inaweza kusongezwa kwa maana hiyo mwaka huu imeangukia Dominika ya tarehe 2 Agosti.

Fursa ya wakatoliki wa Afrika  kujua shirikisho hili na utume wake kwa Kanisa

Siku hiyo imekusudiwa kuwa fursa ya kuwafanya Wakatoliki wa Kiafrika ili wajue historia, uundaji wa chombo hiki na utume wa shirikisho hilo lakini pia kwa ajili ya  kuliombea Kanisa la Ulimwenguni na kwa namna ya pekee barani Afrika. Kwa kawaida siku hiyo uambatana na makusanyo maalum, lakini kwa sababu ya dharura ya virusi vya corona  mwaka huu kwa taarifa ya   barua kutoka kwa Katibu mkuu, Padre  Terwase Henry Akaabiam, iliyenukuliwa katika blogi ya Mabaraza ya Maakofu wa Afrika Mashariki ya (AMECEA)kwamba makusanyo hayo yameharishwa. Lakini Padre Akaabian amebainisha katika brua yake iliyoelekezwa kwa makatibu wakuu wa Mabaraza ya  Maaskofu wa Afrika  kwa kuwa wale ambao wanataka kutoa mchango wa kifedha au vitu wanaweza kufanya hivyo.

Secam iliundwa mwaka 1969

Makusanyo hayo husaidia kuunga mkono kazi na utume wa Secam na ni njia ya kuwafanya Wakatoliki wote wa Kiafrika ambao ni washiriki kamili kuhisi kuwa sehemu yake ameeleza Padre Anthony Makunde, katibu mkuu wa Amecea. Kunako mwaka 2019 Secam ilifanya sherehe za Jubileo ya dhahabu. Shirikisho hili liliundwa kunako mwaka 1969 na kuzinduliwa na Papa Paulo VI kunako mwezi Julai mwaka huo huo katika fursa ya ziara yake ya kitume nchini Uganda, ikiwa ni kwa mara ya kwanza Papa katika Bara la Afrika.

Kudumisha na kuhamasisha ushirikiano kidugu

Wazo la kuunda muundo wa bara lenye uwezo wa kukuza maono ya pamja ya utume wa Kanisa barani Afrika, lilikomaa  mara baada ya Mtagusi wa II wa  Vatican, wakati maaskofu wa Kiafrika walionyesha mapenzi yao  ya kutenda kwa muungano,kwa  kushinda  tofauti za lugha zao,  kihistoria, na kitamaduni. Lengo kuu maalum la Secama  kwa maana hiyo ni kudumisha na kuhamasisha ushirikiano wa kidugu na ushirikiano wa Mabaraza ya Maaskofu wa Afrika, hasa katika  kujikita na mahusiano ya uwanja wa uinjilishaji, haki na amani na mazungumzo ya kidini.

14 July 2020, 12:54