Tafuta

Vatican News
2019.03.12  makambi ya vizuizi,magereza ya wakimbizi na wahamiaji 2019.03.12 makambi ya vizuizi,magereza ya wakimbizi na wahamiaji  

Italia-Jumuiya Mt.Egidio:Tujibu wito wa Papa na mikondo ya kibinadamu!

Katika misa ya Papa Francisko katika kikanisa cha Mtakatifu Marta Vatican wakati wa kumbukizi la miaka 7 tangu atembelee Lampedusa,amesema wazi juu ya hali halisi ambazo wanaishi wafungwa huko Libia.Taarifa zinazotolewa zimemechuljwa kutoka hali halisi mbaya sana,alisema.Mauro Garofalo Mhusika wa masuala ya uhusiano kimataifa wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio anayo ya kusema kuhusiana na hilo.

Na Sr.Angela Rwezaula;-Vatican.

Kizuizini, mahali ambamo watu wameshikiliwa ambao walikuwa na tumaini la kuvuka bahari. Maneno ya Papa Francisko yanaangazia kile ambacho kimekuwa kikiendelea kwa muda mrefu nchini Libya ambapo kando kando  ya  vituo rasmi vya kuweka watu vizuizini, ambao wanawakamata wakiwa wanavuka bahari  kuna vituo vingine vya  kizuizini visivyo rasmi, vilivyomo mikononi mwa wanamgambo wa Libya. Ni karibu miundo thelathini ambapo, kwa mujibu wa makadirio ya UNHCR, na  Kamati Kuu ya  UN ya Wakimbizi, wanathibitisha kuwa inawezekana ni wakimbizi 48,000 na wanaotafuta hifadhi. Idadi kamili ni ngumu kuipata kwa sababu ni vigumu kabisa kuingia katika vituo hivyo.

Mikondo ya kibinadamu ni muhimu

Wale ambao waliweza kutoroka wanazungumzia  juu ya hali mbaya sana  ya kiafya, wimbi la watu kama 600, wanakosa chakula na maji ya kunywa ni shida. Jambo la uhakika ni kwamba, kulingana na shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji, wanasema hapo kuna  ukiukwaji wa kutisha,mivutano na mizozo kibao na zaidi katika kukosa kutengua mfumo unaochochea biashara na usafirishaji haramu wa binadamu. Kwa maana hiyo Jumuiya ya Mtakatifu Egido inatoa wito kwa serikali kwamba katika eneo hilo wanaishi wanaume, wanawake na watoto ambao wanapaswa waokolewa kwa haraka. Bwana Mauro Garofalo, Mhusika wa mahusiano ya kimataifa ya Jumuiya ya Mtakatifu Egidio akihojiwa na Vatican News, amebainisha kwamba maneno ya Papa yanaelekeza  njia ambayo tayari imefanya kazi kwa wakimbizi wa Siria. Na njia hiyo ni mchakato wa mikondo ya kibinadamu. Maneno ya Papa Francisko yote yanatukumbusha ukweli dhahiri kwamba kilomita chache kutoka ukingo wa Italia kuna mahali, ambapo yeye mwenyewe alikuita  kuzimu, ambapo mamia ya maelfu ya watu wanateseka, ni wafungwa, wanapata kila aina ya ubaya. Hii haiwezi kutokea bila sisi kugundua.

Uhamasishaji wa kibinadamu Italia na Ulaya

Papa alizungumzia juu ya kuchakachua taarifa za ukweli na  labda tumesahahu lakini haiwezekani kusahau ukweli anasisitiza mhusika wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio. “Papa ametualika wote kuwa makini mbele ya hili kwa utambuzi wa uso wa Yesu katika maskini”.  Hata hivyo ameongeza kusema kiukweli ni ngumu, kusuluhisha sura ya kisiasa na kijeshi ya Libya, lakini hii haiwezi kusimamisha  hataua za kutafuta suluhisho kwa haraka sana. Kuna suluhisho zinazowezekana na kwamba anaamini kuwa uhamasishaji wa kibinadamu, lazima ufanywe nchini Italia na kwa nchi zote za  Ulaya.  Mfano huo kwa hakika ni  tayari upo  ambao ni mikondo ya  kibinadamu ambayo imeleta mafanikio makubwa.

Mantiki ya ustaarabu wa Ulaya

Bwana Bwana Mauro Garofalo ameongeza kusema juu ya jambo moja ambalo Papa Francisko alisema, nalo ni changamoto sana kwa wazo la mantiki ya ustaarabu wa Ulaya. Ulaya lazima itafuta njia za kuokoa maisha ya watu hawa ambao walitaka kuja Ulaya na ambao wamehatarisha kila kitu yaani hadhi, mali ya mtu binafsi na  afya. Tunahitaji kupata jibu, ambapo mfano tayari upo pale, lakini inawezekana na lazima tutoe wito wa ukarimu kwa kila mtu. Hapo zamani, amesema “tumetuma misaada katika kambi hata katika  kambi nyingine zisizo halali, lakini ni ngumu sana kwa sababu hali ya kisiasa hairuhusu uingiliaji wa kweli katika muundao. Watu hawa lazima wachukuliwe vinginevyo watachukuliwa mateka na wanamgambo, vikosi vyenye silaha, wafanya biashara wa madawa ya kulevya,  wasaliti, na suala ambali haikubaliki, amesisitiza Bwana Garofalo.

10 July 2020, 13:25