Tafuta

2019.07.12 Patriaki wa wakaladayo nchini Iraq, Kardinali L Louis Sako 2019.07.12 Patriaki wa wakaladayo nchini Iraq, Kardinali L Louis Sako 

Iraq-Kard Sako:Imani inasaidia kukabiliana na changamoto na ubaya!

Kardinali Sako amezungumzia juu ya jitihada za Kanisa la Wakaldayo katika utume wao na katika kuendelea na mageuzi ya lazima na kutunza utumaduni wa dhati kwa miaka 2000.Amesema hayo katika barua aliyowaandikia waamini na watu wenye mapenzi mema katika siku ya kuadhimisha Siku kuu ya Mtakatifu Thomasi Mtume na msimamizi wa Kanisa lao.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Patriak Sako Louis Raphaël  katika fursa ya Siku kuu ya Mtakatifu Thomas mtume, tarehe 3 Julai 2020  ameandika barua yake kuwa “Kanisa letu na msimamo katika utume wake na huduma yake ni kwa sababu inapeleka mwili wa mateso ya Kristo ambayo yametokana na kuteswa na wafiadini”. Hii ni barua ambayo amewaandikia waamini wakati wa kusheherekea sikukuu ya Msimamizi wa Kania  hilo ambapo amezungumzia juu ya jitihada za Kanisa la Wakaldayo katika utume na katika kuendelea mageuzi ya lazima na kutunza utumaduni wa dhati kwa miaka 2000. Kardinali  Sako amesisitiza kuwa “Kanisa litaendelea kuwa shauku ya wazalendo wake wa sasa katika kukabiliana na hali ngumu  na hasa wale ambao wamebaki nchini Iraq, yaani nchi ya utambulisho wao.

Katika barua yake, Kardinali ameweka umakini juu ya umuhimu wa imani ambayo lazima itambuliwe kwa kina na ambayo inaruhusu kutoa chachu ya matumaini katika mioyo yetu, licha ya hisia za uchovu wa vita visivyoisha nchini Iraq. Kwa mujibu wake amesema inaongeza huduma yao katika kila tatizo na changamoto mbele ya kila aina ya jitihada za nguvu zitokazo katika ubaya na kuchanganyikiwa kwa sababu  wakati mwingine katika  mitandao kijamii. Dhoruba ya babilionia ya wakaldayo haitamuadaa kutoka katika utume wake na huduma yake, kwa uaminifu na uvumilivu amesisitiza. Aidha Kardinali Sako, katika barua yake amewashauri wakristo wa Makanisa yote na kusali na kuzidisha nguvu zao kuwasaidia ili koboresha hali ya wale ambao wamebaki Iraq na kutenda kwa kuheshimu haki zao  na uwakilishi wa usalama wao na msimamo.

Kutokana na hayo ndipo  ametoa wito wake kwa wakristo wa Iraq kuwa na tumaini, ujasiri na kusaidia Chama cha mshikamano wa wakaldayo kilichoanzishwa miaka mitano iliyopita yaani tarehe 3 Julai katika sikukuu hiyo Mtakatifu msimamizi wao. Patriaki katika barua yake anatoa ushauri kwa wakaldayo kushirikiana nao na kusadia kimaadili na kihadhi ili kiweze kuwa chombo cha utume kibinadamu, kijamii na kiutamaduni. Mafundisho ya wakaldayo ni ya katoliki amekumbusha Patriaki, utambulisho wake wa watu ni wakaldayo. Katika barua yake anafunga akifahamisha kuwa sababu ya janga la covid-19  sinodi ya wakaldayo imeahirishwa tarehe. Na kwa maana hiyo ni matumaini ya kuweza kurudia hali ya kawaida. Aidha ametoa hata ujumbe mwingine kwa njia ya Tovuti ya Upatriaki mahali ambapo anakumbsha kwamba changamoto nyingi ambazo zimelazimisha kubaliwa na wakaldayo wa Teheran, wa kwanza  kuwa wahamiaji. Hiyo ni kuwakumbuka  karibu wakaldayo 15,000 waliokuwa katika Jamhuri ya Kiislam awali.

Kwa sasa wamebaki kati ya Waraherani na Waurmia 4000  tu na hivyo  hali hiyo inaleta wasiwasi kwa mujibu wa Kardinali Sako. Ili kufika kusitisha wimbi na kuongeza nguvu  ya hali halisi kuna ulazima wa makleri mahalia ambao wanajua vema watu, utamaduni na lugha  na wakati huo huo kuongeza nguvu ya kukuza miito ambayo ni michache. Wakristo kama ilivyo hata kwa watu wengine, wanahidi sana kutengwa kwa ajili hiyo lazima wafikie wao kama watu. Kwa kuhitimisha, Patriaki  Sako amebainsha kwamba imani yao inatokana na uhusiano wa kina na Injili ambayo inawakilisha kwao kama tunu msingi wa imani. Imani yao ni ya kina na ni ishara muhimu ya matumaini na suluhisho lazima kusibiri na kusali.

06 July 2020, 13:02