Tafuta

Kanisa la Ecuador linabainisha juu ya haja ya  kulinda haki ya maisha ambayo ni zawadi kutoka kwa Mungu,kwa sababu afya ni haki ya lazima ya mwanadamu. Kanisa la Ecuador linabainisha juu ya haja ya kulinda haki ya maisha ambayo ni zawadi kutoka kwa Mungu,kwa sababu afya ni haki ya lazima ya mwanadamu. 

Ecuador-Maaskofu:Ufisadi ni dhambi kubwa na uhukumu kifo kwa wenye kuhitaji!

Kanisa nchini Ecuador linakemea ufisadi kwa wanabainisha kuwa ni dhambi kubwa na inayomhukumu kifu mwitaji.Kuna haja ya kulinda haki ya maisha ambayo ni zawadi kutoka kwa Mungu,kwa sababu afya ni haki ya lazima ya mwanadamu,wakati leo hii imegeuka kuwa biashara nchini humo.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Ufisadi ni dhambi kubwa sana, haiendani na imani ya Kikristo na inawakilisha uhalifu ambao unahukumu kifo kwa watu wengi wanaohitaji. Ni maelezo makali kutoka kwa Baraza la Maaskofu nchini Ecuador (EEC) katika barua yao wazi kwa waamini ambayo imetangaza tarehe 29 Juni 2020. Katika Hati hiyo inamewadia wakati nchi iliyokumbwa na Janga la virusi vya corona inagongana  ndani ya kukosekana kwa  ununuzi na usambazaji wa madawa, vifaa vya usalama wa mtu binafsi kama vile barakoa na vyakula. Hii inaongeza kashfa za kesi za ufisadi, ambapo maaskofu wanabainisha  kuwa karibu na watu wanaoteseka kwa sababu ya upotezaji wa maisha ya wapendwa wao, kukosa  kazi pia kukosa  tumaini. Licha ya kukemea ufisadi wenyewe, Kanisa la Ecuador pia linabainisha juu ya haja ya  kulinda haki ya maisha ambayo ni zawadi kutoka kwa Mungu, kwa sababu afya ni haki ya lazima ya mwanadamu, na wakati leo hii  wanasema imegeuka kuwa biashara.

Katika muktadha wa mgogoro ambao siyo wa kiuchumi tu, bali pia afya ya kijamii inayotawala nchini humo, wakati masikini wanazidi kunyimwa fursa yoyote, uwazi katika usimamizi wa rasilimali unahitajika, wanasisitiza maaskofu (EEC) nchini Equador na kusisitiza kuwa vita dhidi ya ufisadi isiwe ya ubaguzi.  Kitendo hiki kibaya, kwa hakika kinakuza utamaduni wa kutupilia mbali walio hatarini zaidi na husababisha ukosefu wa haki na kutokujali. Kufuatia na mtazamo huo maaaskofu wanatoa onyo hasa suala la   kutokujali na kutowajibika  kwa wengine na kwa maana hiyo wanasema watu kama hao watawajibika mbele ya Mungu.

Aidha kufutia na ufisadi huo maaskofu wamesema kwamba watafanya uchunguzi  iwezekanavyo ili  kupata fedha  zilizoibiwa na kuzirudisha kwa raia.Watu wenye kustahili hawawezi kujumuishwa katika ufisadi na kuadhibiwa, wanasema maaskofu. Hatimaye maaskofu  wana imani na mfumo wa demokrasia na wanatumaini kuwa watu wa Mungu hawatakubaliana kwa mujibu  na maagizo ya ufisadi. Kila mtu afanye bidii yake kwa ajili ya haki, amani, ustawi wa wote kwa ajili ya maisha endelevu ya nchi.

01 July 2020, 13:13